dawa ya mchawi ni ndogo sana, Okoka, mkabidhi Yesu Kristo wa Nazareth awe Bwana na Mwokozi wa Maisha yako, jazwa Roho Mtakatifu na ishi maisha matakatifu. utakuwa unaonekana kama nyota wakiwa mbaliii, wanakujua hata kabla hawajafika kwako kuwa pale sio pa kusogea. pia, kwa waliookoka hata damu ikimwagwa wanajua hawataitumia kwasababu kwenye mambo yao haitafanya kazi, nyota hawataweza kukunyang'anya kwasababu unalindwa kwa Agano la Damu ya Yesu.
Mungu aliingia pamoja nasi Agano jipya, hili ni Agano ambalo Mungu mwenyewe aliamua kuliandika sio kwa kalamu bali kwa Damu ya Yesu Kristo wa Nazareth, hivyo Mungu ameapa, our God is bound by it, iwe iweje lazima Mungu atimize kile alichoapa kwenye Agano Jipya, lililotokana na kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo. Agano hili ni kuu kuliko mikataba au viapo vya kawaida, na linadumu milele. Yesu aliwaambia wanafunzi wangu, baada ya kukitwaa kikombe,
akasema, hii ni Damu yangu ya Agano Jipya (kumbe kulikuwepo agano la zamani), imwagikayo kwa ajili ya wengi, fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Utajapo Damu ya Yesu, Shetani na utawala wake wote wanasambaratika kwasababu ni Damu iliyolipa Deni loooote la ukombozi wa maisha ya Mwanadamu na kumfanya shetani asiwe na haki yeyote kukunyanyasa au kututesa. ukiwa ndani ya Agano hili, unafanyika mtoto wa Mungu na yeye Mungu anakuwa ndiye mlinzi na mkombozi wako. yeye hutuma malaika wake watulinde popote tulipo. hii imethibitishwa kabisa na ex-witches waliokuwa wamekubuhu.
Damu ya Yesu ndio Damu ya kutuondoa dhambi zetu pia, ili tuwe watakatifu na tukubalike mbele za Mungu, bila hii, Mungu hakutambui. ukienda nje ya Yesu Kristo Mungu hakutambui na hakupokei kwasababu umeenda kwake nje ya Agano lake. hii ina maana kwamba, wote wanaomtafuta Mungu kwa njia nyingine yeyote nje ya kupitia Kumkiri na kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao, wote wataenda motoni kwasababu wamefuata njia isiyo sahihi ambayo Mungu hakusema tupitie. huu ni ushauri tu, tafakari na chukua hatua.