Wachawi wanavyoiba nyota za watu wanafanyaje?

Wachawi wanavyoiba nyota za watu wanafanyaje?

Sidhani kama Kuna mtu anaweza kuiba nyota ya mtu maana nyota ni kiongozi au malaika kutoka kwa Mungu anapatikana siku mtu anapozaliwa iwapo ataitwa akuongoze ndani ya zile siku 40 mtoto anapozaliwa waisraeli wanatumia uvumba kumuita na kumkaidhi mtoto kama mtoto Emmanuel au Yesu alivyopelekewa uvumba wa nyota yake au Malaika wake, nachojua kinachoharibiwa ni akili ya mtu, bahati na afya Bora mtu mbaya akijua vitu hivyo ndo anakuharibia na mpaka uwe naye au mtu anayejua Kila kitu chako hivyo ogopa mtu anayekuwa anapeleleza habari zako kwa Nia mbaya na upo naye karibu ni rahisi kukuangamiza na ndo maana maandiko yanasema mchawi auwawe Ili asiangamize wengine kwa hila zake na husuda.
malaika wa ulinzi hayupo muda wote, malaika ni watakatifu, hawakai na uchafu, kama ingekuwa hivyo basi hata ukienda kuzini guest house, malaika angekuwa pembeni anakusubiri umalize kufunga magoli muongozane kukuongoza hadi home kwako. Malaika wa Mungu wanakulinda au kuwa pamoja na wewe wakati ule unapoishi maisha matakatifu, ukiwa wa Mungu utalindwa na Mungu, ukiwa wa shetani utakuwa na wa shetani. kama ingekuwa kila mwanadamu analindwa na hao malaika basi hata wachawi na waganga wa kienyeji manake wana malaika? nuru na giza tangu lini vina urafiki? Okokeni, acheni dhambi ili mpone na wachawi. na sio hivyo tu, mkaurithi ufalme wa Mbinguni na kuepuka jehanum ya moto wa milele.
 
mkuu binadamu ameumbwa kama ilivyo computer, ana hardware(utu wa kimwili) na software(utu wa kiroho) hivo wachawi/waganga kwa msaada wa mashetani wakifanikiwa kuudukua utu wako wa kiroho wanaweza kufanya chochote walichokusudia kwako, mfano kukusababishia maradhi, ajali, kuharibiwa nyota/kuibiwa na nk..
Ni sawa.

Lakini Nyota inaharibiwaje?

Wanaifanyaje?
 
Ni sawa.

Lakini Nyota inaharibiwaje?

Wanaifanyaje?
Inaibiwa kwa msaada wa majini,na waganga uiza kwa wenye pesa wahitaji.
Nyota ni biashara kubwa Sana kwa waganga na uwapatia pesa nyingi Sana.Nyota ni kipawa kipaji alichokuwekea Mwenyezi Mungu ,kwa maana kila anaezaliwa tayari Mungu ana mpango naye, wakati huo Mungu kampa mwanadamu akili ya kuchagua mema na mabaya maana Mungu sio dikteta.Ukimuacha Mungu nae anakuacha,ukimuita nae uitika,so unachagua nani awe boss wako.
 
Uchawi upo na kweli mtu anaweza kuiba nyota yako kwa kupitia alama za kiganja chako

Umewahi kujiuliza watu wanaoenda kwa waganga kwanini huwa wanaangaliwa viganja vyao?

Ni kwa sababu akiona una bahati anakuibia na usiniulizi kivipi maana mimi sio mchawi na ninayapuuza sana ingawa yapo

Wengine huwa wanakuwa na mikosi na mambo yao hayaendi kwa sababu wako karibu na watu wenye husda na jicho la husda kwani kila unapofanya kitu kinaharibika

Kuanzia biashara, Kazi, Ndoa na hata safari basi ujue kuna mnafiki wa karibu unaemuona ni mzuri kumbe hakutakii Jema lolote na wewe kila jema lako unamwambia halafu linafeli

Ila siku ukimjua na ukimlamba block kwa kila sehemu hata salamu basi mambo yako yatabadilika

Huyo sio anaiba nyota yako hapana anaichoma kabisa [emoji24][emoji24][emoji24]
Unawaza kujibu ila una uwezo mkubwa wa kujizuia kuongea mengi au hadhari ya ntaonekanaje? Nimejifunza kuhusu alama za vidole na nuksi za ukaribu na wabaya kuwaaamini wabaya pasipo kuwajua Hii inatutafuna wengi sanaaa
 
Unawaza kujibu ila una uwezo mkubwa wa kujizuia kuongea mengi au hadhari ya ntaonekanaje? Nimejifunza kuhusu alama za vidole na nuksi za ukaribu na wabaya kuwaaamini wabaya pasipo kuwajua Hii inatutafuna wengi sanaaa

Kweli kabisa hili la kuwaamini wabaya bila kuwajua anaweza kuwa hata ndugu yako
Nimeliona hili na roho chafu ipo na wapo wabaya sana
 
Hii sio sayansi unayoijua, ubongo ndio nyota katika ulimwengu wa roho.
Japokuwa najuwa kuwa nyota zinakaa angani tu lkn kwa muktadha wa mada niungane na hadhira kwamba nyota zinakaa ndani ya mtu, sasa basi, nijuavyo ni kuwa kinachoweza kuhamisha nyota (siyo kuiondoa yote) ni zinaa na uasherati.
 
22 April Nisaidie Mkuu
Namba zako za bahati ni
2, 4, 6, 11, 20, 29, 37, 47, 56

Nyota yako inaendana vizuri na kazi zifuatazo > mambo yanayohusiana na bustani, vyakula (catering) , muziki, mapenzi , mitindo ya nguo , kazi yoyote ya ubunifu kwa kutumia mikono

Pia una mvuto wa asili

Vyovyote itakavyokuwa lazima uwe na hela sababu ulishapewa hela na asili yenyewe

Una wachawi wengi lakini Mchawi wako mkubwa ni KUPENDA VITU VYENYE THAMANI SANA (LUXURY GOODS)
 
nyota yake ni simba (Leo)...ruled by sun
*Una nyota ya kuwa mtu maarufu hasa kwa upande wa burudani

*Wewe ni kiongozi

*Unaweza kuwa wa kwanza kwenye chochote kama ukiweza kutambua madhaifu yako na kuyatendea kazi

*Mchawi wako mkubwa anayekuloga ni EGOISM

Nikipata muda nitakuandikia zaidi

Weekend njema kwako
 
Sio KILA nyota ya mtu inaibiwa kumbuka hawa wapumbavu sio kwamba wanayo nguvu kubwa kuliko wote,kama unayo nguvu ya Mungu awakusogelei sio wewe tu hata uzao wako ikiwemo hata ulio tumboni,wakisogea tu kutaka kuchezea nafsi yako,mali yako, watoto wako nk upigwa shoti kali kama moto wa gesi na awakugusi tena.
Hawa wapumbavu waganga na wachawi nao ni waoga pia Ili wakuroge ni lzm wafanye test kukupima kwenye radar zao wanapima nguvu iliyomo ndani yako kama ni kubwa kuliko yao hawataki shali na wewe.
Hata kwenye usafiri mfano basi wakitaka kutoa kafara kwa kusababisha ajali ambayo mara nyingi huwa wanaliangusha au kuyagonganisha magari hapa unakuta dereva kaacha njia kamfata mwenzake au wanaifanya barabara inakua moja kwa kuifanya iwe nyembamba mara paa uso kwa uso kama katika basi hilo walilokusudia kuna mtu anayo nguvu ya Mungu uharisha na awaligusi gari hilo maana upigwa shoti hatari.Wanatumia kifaa kinaitwa (icds) asidiizi ni testa za kichawi kupima nguvu aliyonayo mtu kabla ya kumdhuru kichawi.
Nipende kuwatia nguvu hawa wapumbavu hawana lolote wala chochote cha kushinda nguvu aliyopewa mwanadamu na Mwenyezi Mungu wanachoweza ni kutia uoga na hofu, hofu ndio silaha kubwa hawa wapumbavu uitumia kudhuru.
Kama wamepanga kutoa kafara kwenye gari lakini katika mmoja wa wasafiri alimuomba Mungu ailinde safari hio tayari hapo kunakuwa na nguvu ya Mungu kwa vipimo vya radar yao hawawezi lisogelea,na wakishindwa kuliangusha ukumbana na adhabu kali Sana toka master wao yaani shetani ikiwemo kutakiwa kutoa kafara ndugu au mtoto wao au mtu wa karibu,so ukiwa na ndugu, au rafiki mchawi tambua upo kwenye risk ya kutolewa kafara.Wachawi na waganga ni mateka wa shetani wengi wapo kifungoni kwa matishio wakitoka,wakiacha watauwawa na kupelekwa kuzimu kutumika kimateso ambayo wao uyashuhudia, mchawi na mganga wanayo password ya kuingia kuzimu kupokea maagizo.Mchawi na mganga awanywi damu labda kidogo lakini damu utolewa sadaka kwa shetani.
Kwann ulimwengu wa Sasa Siri za giza ziwe wazi,Mungu karuhusu tuzijue siri zao Ili tusiwaogope,ukishamjua adui sio tishio tena kwako.
Nabii na Mtume Kalunya.... umefunua.
 
niangalizie tar 26 / 12
Sawa

Namba zako za bahati ni
1, 4, 8, 10, 13, 17, 19, 22, 26

Kazi nzuri kwako ni zile zinazohusiana na masuala ya hela (finance) na umeneja. Ukiwa meneja kwenye kampuni yoyote lazima hiyo kampuni ifanikiwe

Una wachawi wengi wanaokuloga wakiongozwa na TABIA YAKO YA KUTAKA KUFAHAMU KILA KITU PIA WEWE NI MGUMU KATIKA KUSAMEHE
 
Nyota yako ni Sagitarius (Mshale)

Sayari inayorule nyota yako ni Jupiter ( Luck and expansion planet)

Unapenda adventure sana na ni mtu mwenye energy sana, hupendi kubanwa ....

Huwa unafanya maamuzi ya ghafla pasipo kufikiri mara mbili ambayo baadae huwa yanaleta majuto (impulsive decision)
Na Mimi niangalizie 24.11
 
Back
Top Bottom