SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Moja ya mambo ambayo yamekwamisha sana maendeleo ya sekta nyingi nchini ni kuvurugwa au kutokuwepo kabisa kwa vyama vya wafanyakazi.
Hii imesababisha kutokuwepo kwa mikataba inayozingatia haki za wafanyakazi husika. Upande wa waajiri umekuwa na nguvu ya kuamua malipo na mustakabali mzima wa sekta husika.
Leo nitagusia upande wa sekta ya mchezo wa mpira wa miguu. Hivi karibuni kumeibuka mijadala kuhusu maslahi ya wachezaji hasa wazawa. Katika ligi kuu, kuna wachezaji wanalipwa mishahara ya milioni moja kwa mwezi, na kuna wengine wanalipwa milioni 30 kwa mwezi.
Tofauti hizi za viwango ni za kutegemea kwa sababu thamani ya wachezaji inatofautiana ila tatizo kubwa ni kutokuwepo kwa standard zinazotoa mwongozo wa kiwango cha chini cha mshahara, ni vigezo gani vinaamua thamani sahihi ya mchezaji, na haki za marupurupu mengine kama bima za afya, nyumba, nk.
Miaka fulani hivi huko nyuma, vyama vya wafanyakazi kama vya walimu viliingiliwa sana hadi imefika wakati ni kama havipo katika kusimamia haki za wanachama wao.
Ni jambo ambalo linasikitisha sana na kwa maoni yangu serikali kutopenda "kushurutishwa" kunaleta hasara za muda mrefu kuliko faida za muda mfupi. Natambua kuwa kulibadili hili jambo kunahitaji mabadiliko ya fikra hasa kwa wenye mamlaka, jambo ambalo ni gumu sana kufanyika.
Lingine ambalo wengi hawafahamu ni kuwa hawa wachezaji tunaowalipa milioni 30 kwa mwezi, huko kwao walikuwa wanalipwa gharama za kawaida sana, na thamani zao zinakuwa inflated na madalali wanaoenda kuwachukua na kuwaleta hapa.
Hii ina maana tungeweza kuwapata hawa wachezaji kwa kuwalipa standard rates zinazolipika (milioni 5-10) na hivyo kuzipa timu nafasi ya kulipa wachezaji wazawa mishahara ili standard pia badala ya hii tofauti kubwa tunayoiona.