Wachezaji wa mpira wa miguu anzisheni chama cha kutetea haki zenu

Wachezaji wa mpira wa miguu anzisheni chama cha kutetea haki zenu

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Moja ya mambo ambayo yamekwamisha sana maendeleo ya sekta nyingi nchini ni kuvurugwa au kutokuwepo kabisa kwa vyama vya wafanyakazi.

Hii imesababisha kutokuwepo kwa mikataba inayozingatia haki za wafanyakazi husika. Upande wa waajiri umekuwa na nguvu ya kuamua malipo na mustakabali mzima wa sekta husika.

Leo nitagusia upande wa sekta ya mchezo wa mpira wa miguu. Hivi karibuni kumeibuka mijadala kuhusu maslahi ya wachezaji hasa wazawa. Katika ligi kuu, kuna wachezaji wanalipwa mishahara ya milioni moja kwa mwezi, na kuna wengine wanalipwa milioni 30 kwa mwezi.

Tofauti hizi za viwango ni za kutegemea kwa sababu thamani ya wachezaji inatofautiana ila tatizo kubwa ni kutokuwepo kwa standard zinazotoa mwongozo wa kiwango cha chini cha mshahara, ni vigezo gani vinaamua thamani sahihi ya mchezaji, na haki za marupurupu mengine kama bima za afya, nyumba, nk.

Miaka fulani hivi huko nyuma, vyama vya wafanyakazi kama vya walimu viliingiliwa sana hadi imefika wakati ni kama havipo katika kusimamia haki za wanachama wao.

Ni jambo ambalo linasikitisha sana na kwa maoni yangu serikali kutopenda "kushurutishwa" kunaleta hasara za muda mrefu kuliko faida za muda mfupi. Natambua kuwa kulibadili hili jambo kunahitaji mabadiliko ya fikra hasa kwa wenye mamlaka, jambo ambalo ni gumu sana kufanyika.

Lingine ambalo wengi hawafahamu ni kuwa hawa wachezaji tunaowalipa milioni 30 kwa mwezi, huko kwao walikuwa wanalipwa gharama za kawaida sana, na thamani zao zinakuwa inflated na madalali wanaoenda kuwachukua na kuwaleta hapa.

Hii ina maana tungeweza kuwapata hawa wachezaji kwa kuwalipa standard rates zinazolipika (milioni 5-10) na hivyo kuzipa timu nafasi ya kulipa wachezaji wazawa mishahara ili standard pia badala ya hii tofauti kubwa tunayoiona.
 
Moja ya mambo ambayo yamekwamisha sana maendeleo ya sekta nyingi nchini ni kuvurugwa au kutokuwepo kabisa kwa vyama vya wafanyakazi. Hii imesababisha kutokuwepo kwa mikataba inayozingatia haki za wafanyakazi husika. Upande wa waajiri umekuwa na nguvu ya kuamua malipo na mustakabali mzima wa sekta husika.

Leo nitagusia upande wa sekta ya mchezo wa mpira wa miguu. Hivi karibuni kumeibuka mijadala kuhusu maslahi ya wachezaji hasa wazawa. Katika ligi kuu, kuna wachezaji wanalipwa mishahara ya milioni moja kwa mwezi, na kuna wengine wanalipwa milioni 30 kwa mwezi. Tofauti hizi za viwango ni za kutegemea kwa sababu thamani ya wachezaji inatofautiana ila tatizo kubwa ni kutokuwepo kwa standard zinazotoa mwongozo wa kiwango cha chini cha mshahara, ni vigezo gani vinaamua thamani sahihi ya mchezaji, na haki za marupurupu mengine kama bima za afya, nyumba, nk.

Miaka fulani hivi huko nyuma, vyama vya wafanyakazi kama vya walimu viliingiliwa sana hadi imefika wakati ni kama havipo katika kusimamia haki za wanachama wao. Ni jambo ambalo linasikitisha sana na kwa maoni yangu serikali kutopenda "kushurutishwa" kunaleta hasara za muda mrefu kuliko faida za muda mfupi. Natambua kuwa kulibadili hili jambo kunahitaji mabadiliko ya fikra hasa kwa wenye mamlaka, jambo ambalo ni gumu sana kufanyika.

Lingine ambalo wengi hawafahamu ni kuwa hawa wachezaji tunaowalipa milioni 30 kwa mwezi, huko kwao walikuwa wanalipwa gharama za kawaida sana, na thamani zao zinakuwa inflated na madalali wanaoenda kuwachukua na kuwaleta hapa. Hii ina maana tungeweza kuwapata hawa wachezaji kwa kuwalipa standard rates zinazolipika (milioni 5-10) na hivyo kuzipa timu nafasi ya kulipa wachezaji wazawa mishahara ili standard pia badala ya hii tofauti kubwa tunayoiona.
Unaijua Sputanza au unaandika tu
 
Sputanza Wako Wapi...?

Hawa Wanatakiwa Wamwelekeze Fei Toto.....Ile Pesa Waliyoirudisha Utopolo kwenye Akaunti Yake Achikichie au Akampe Manara airudishe..!
 
Nilikuwa sijui kama kipo ila inaonyesha hawatimizi wajibu wao ipasavyo.
Sasa kama ulikuwa hujui kama kipo, ni vyema ukakaa kimya ili uzi ufe wenyewe, kuliko kuanza kukihukumu kuwa kilikuwa hakitimizi wajibu wake. Wachezaji wenyewe ni wazito kujiunga ili walipe membership fee, hivi hizo gharama za kisheria ni nani atajitolea? Mara zote mchezaji akikutwa na tatizo ndio anawakimbilia SPUTANZA, mfano ni Ramadhani Singano

1672667617304.png
 
Sasa kama ulikuwa hujui kama kipo, ni vyema ukakaa kimya ili uzi ufe wenyewe, kuliko kuanza kukihukumu kuwa kilikuwa hakitimizi wajibu wake. Wachezaji wenyewe ni wazito kujiunga ili walipe membership fee, hivi hizo gharama za kisheria ni nani atajitolea? Mara zote mchezaji akikutwa na tatizo ndio anawakimbilia SPUTANZA, mfano ni Ramadhani Singano

View attachment 2466801
Sasa unataka uzi ufe wakati mwenyewe unakiri kuwa kuna matatizo ndani ya hiko chama chao.
 
Sputanza Wako Wapi...?

Hawa Wanatakiwa Wamwelekeze Fei Toto.....Ile Pesa Waliyoirudisha Utopolo kwenye Akaunti Yake Achikichie au Akampe Manara airudishe..!
Ile hela aile tu. Yanga wana jeuri ya maskini.
 
Nilikuwa sijui kama kipo ila inaonyesha hawatimizi wajibu wao ipasavyo.
Hawatimizi wajibu wao kivipi?! Suala la maslahi ya mchezaji ni la kwake mwenyewe, wakala wake, na mwanasheria wake. Mtu kama Fei, kama aliona hatimae 4M ni kidogo, hapo alitakiwa ku-negotiate na Uto, na endapo Uto ingemkatalia, angeomba kuvunja mkataba. Endapo hapo tena Uto wangekataa, ndipo angeenda SPUTANZA, na wangelaumiwa endapo wasingemsimamia Fei kupata hicho anachodai.
 
Tatizo La UTO wanataka Wamkomoe Dirisha dogo Lipite hawajatoa Ruhusa...Hivyo definitely itabidi abakie hapo hapo.. UTO roho mbaya Sana..!
 
Back
Top Bottom