Tetesi: Wachezaji watano wa Simba wasimamishwa kupisha uchunguzi kwa kichapo kikali cha goli 5 kutoka kwa Yanga

Huyo Prisca ni mmbea mbea tuu..
Ndo maana Manara wakati yupo Simba alimtusi
 
Hebu tuache uswahili Tanzania!!
1. Chama anayetuhumiwa si ndo amepiga faulo ambayo ilizaa kona na baadae goli la simba?
2. Inonga amefanyaje?
3. Ukitazama magoli yote matano simba wanapokwa mipira/intercepted passes watu wanaenda kufunga
Kama ni kweli viongozi wa Simba wamewasimamisha wachezaji basi anatafutwa tu mbuzi wa kafara badala ya kufanya utafiti wa kitaalam kuangalia Simba ilizidiwa wapi. Na mpira ni mchezo wa wazi hao viongozi waache uswahili na kuokoteza maneno halafu wanaamua kuwafungia wachezaji badala ya wao kuwajibika kwa uzembe wao mkubwa wa kusajili baadhi ya wachezaji bila kuangalia mahitaji ya timu na kuajiri kocha wa viungo asiyelingana na hadhi ya Simba. Wa kwanza wa kuwajibika ni hao viongozi kabla ya kuwatuhumu hao wachezaji.

Kwa mtu aneyefahamu mpira kwa undani huwa inatokea siku boli linakataa sasa kwa upuuzi huo wa viongozi wa Simba basi kuna wachezaji watakuwa wananonewa. Hapa waliozembea ni benchi la ufundi iwapo mchezaji hakuwa sawa walipaswa wamfanyie sub basi sio kuja kuwapa kimeo wachezaji.
 
Na kama ipo hivyo, kocha yeye kafukuzwa kwa kosa lipi?
Kocha ni kama mbwa asiye na mmliki, hawezi kosa sababu ya kutupiwa jiwe. Sababu inaweza kuwa yoyote ile:

1. Aina ya mpira usio wa falsafa ya Simba
2. Maelewano katika vyumba vya kubadilishia nguo
3. Kutolewa mapema AFL etc etc

Kufungwa si tatizo, tatizo ni kufungwa na Yanga goli nyingi. Hapa lazima apatikane mtu/watu wa kuwajibishwa. Mara nyingi wa kwanza na rahisi kumuondoa huwa ni kocha.
 
Kama ni kweli viongozi wa Simba wamewasimamisha wachezaji basi anatafutwa tu mbuzi wa kafara badala ya kufanya utafiti wa kitaalam kuangalia Simba ilizidiwa wapi...
Hii habari si rasmi, ila tukiweka assumption kuwa ni rasmi basi Kama wameonewa watashtaki. Mambo si marahisi hivyo kuwa utoke tu huko usimamishe wachezaji na kuchafua taswira yao bila ushahidi. Wakisimamishwa halafu wakakubali na kukaa kimya kuna uwezekano ni kweli.
 
Unadhani watasimamishwa bila ushahidi?
Bila hata kupata ushahidi wa ziada,Baleke alionesha wazi hahitaji kuifunga yanga.


Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Bila Simba kurudishwa utamaduni wa kusoma kisomo cha ALALBADIR BAYANA kabla ya mechi itaendelea kuhujumiwa kila siku.

Muwe na utaratibu wa kusoma kisomo kwa wasaliti wa timu.
Muwalishe yamini wachezaji wote na viongozi wote kama wafanyavyo Yanga.

Muone kama Kuna atakayehujumu timu.
 
Unadhani watasimamishwa bila ushahidi?
Bila hata kupata ushahidi wa ziada,Baleke alionesha wazi hahitaji kuifunga yanga.


Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Alionyeshaje mkuu??
Simba walitengeza nafasi ngapiii??
Huyo Baleke ukiacha Ile Nafasi moja aliyopata na kugongesha besera,Kuna nyingine..Me naona wasikurupuke,hata Mchezaji kama Chama ni ngumu kupokea pesa,Nachoona kwake ni kiwango kinekua duni na pia ameshajiona mfalme ndani ya timu.
 
Simba rudisheni utamaduni wa kusoma ALALBADIR BAYANA kabla ya mechi ili kulishana yamini kwa wachezaji na viongozi wote wasaliti.

Zamani Simba na Yanga ilikuwa lazima wazee wasome visomo kwa ajili ya wasa.
Nani aliyefuta utaratibu huu.

Wenzetu Yanga bado visomo vinasomwa kwa wasaliti wa timu kabla ya mechi kubwa na muhimu kwa timu.
 
Mateso huko ni mengi, wakihisi mtu hana bahati πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 

Watatu waliobaki ni akina nani katika hao watano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…