Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona ndo huu au?Naukumbuka huo uzi.
Kumbe ulifutwa! 😳
Kama ni kweli viongozi wa Simba wamewasimamisha wachezaji basi anatafutwa tu mbuzi wa kafara badala ya kufanya utafiti wa kitaalam kuangalia Simba ilizidiwa wapi. Na mpira ni mchezo wa wazi hao viongozi waache uswahili na kuokoteza maneno halafu wanaamua kuwafungia wachezaji badala ya wao kuwajibika kwa uzembe wao mkubwa wa kusajili baadhi ya wachezaji bila kuangalia mahitaji ya timu na kuajiri kocha wa viungo asiyelingana na hadhi ya Simba. Wa kwanza wa kuwajibika ni hao viongozi kabla ya kuwatuhumu hao wachezaji.Hebu tuache uswahili Tanzania!!
1. Chama anayetuhumiwa si ndo amepiga faulo ambayo ilizaa kona na baadae goli la simba?
2. Inonga amefanyaje?
3. Ukitazama magoli yote matano simba wanapokwa mipira/intercepted passes watu wanaenda kufunga
Kocha ni kama mbwa asiye na mmliki, hawezi kosa sababu ya kutupiwa jiwe. Sababu inaweza kuwa yoyote ile:Na kama ipo hivyo, kocha yeye kafukuzwa kwa kosa lipi?
Hii habari si rasmi, ila tukiweka assumption kuwa ni rasmi basi Kama wameonewa watashtaki. Mambo si marahisi hivyo kuwa utoke tu huko usimamishe wachezaji na kuchafua taswira yao bila ushahidi. Wakisimamishwa halafu wakakubali na kukaa kimya kuna uwezekano ni kweli.Kama ni kweli viongozi wa Simba wamewasimamisha wachezaji basi anatafutwa tu mbuzi wa kafara badala ya kufanya utafiti wa kitaalam kuangalia Simba ilizidiwa wapi...
Unadhani watasimamishwa bila ushahidi?Shida kubwa Simba iko kwa Mangungu, hata huyo Robertinho ni bangusilo tu, wale walioshindwa uchaguzi na Mangungu wataihujumu timu hadi aachie nafasi hiyo, Mangungu ananikumbusha enzi za akina marehemu Juma Salum, kabla ya hapo marehemu Jimmy David Ngonya, kulikuwa ni Vita tu ile ya Israel na Hamas ni cha mtoto.Shahidi ni Kassim Dewji vs Juma Salum.
Mangungu sio mtu wa mpira, watu wa friends of Simba hawampendi na hawako tayari kufanya kazi naye, sasa mm najiuliza mbona wenzetu Yanga wamemuachia timu GSM, hamuoni maendeleo hayo.
Haya mambo ya kijinga kijinga ndani ya timu yetu huwa hayaishi na hayataisha, katika mazingira kama haya mjinga gani atakubali kuweka bilioni 20?
Kama huoni tatizo ni Che Malone basi Fanya uchunguzi upya.Ila Inonga ni kama simuelewi siku hz toka aje huyu Chemalone amekua anacheza kizembe zembe...au macho yangu..
Alionyeshaje mkuu??Unadhani watasimamishwa bila ushahidi?
Bila hata kupata ushahidi wa ziada,Baleke alionesha wazi hahitaji kuifunga yanga.
Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Wachezaji watano wa Simba Sc akiwemo Enock Inonga na Clatous Chota Chama wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yao baada ya kufungwa na Yanga SC mabao 5-1 siku ya Jumapili.
Wachezaji hao wanatuhumiwa kuihujumu timu kitendo kilichopelekea kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao.
Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao cha bodi ya Wakurugenzi ya Simba kilichofanyika jana jijini Dar es salaam.
Chanzo cha uhakika kutoka Simba SC kimeiambia Kishamba Media kuwa uongozi umeshapata ushahidi wa awali kuhusu tuhuma dhidi ya wachezaji hao na sasa imeanza uchunguzi wa kina ili kujiridhisha.
Wachezaji hao watakua nje ya kambi ya timu mpaka hapo maamuzi mengine yatakapofanyika.
Chanzo hicho kimesema huwenda leo klabu ya Simba ikatoa taarifa ya wazi kwa Umma juu ya maamuzi waliyofikia kuhusu wachezaji hao au wasitoe ila wahusika wamepewa taarifa.
Maamuzi mengine yaliyofikiwa na bodi ni kufutwa kazi kwa kocha mkuu Robertinho, msaidizi wake pamoja na kocha wa viungo.
Kishamba Updates
Wasiivuruge timu, duniani kote timu kubwa kufungwa goli 5 au zaidi ni kitu cha kawaida
MO ndio anayetakiwa kujiuzulu yeye ndio ameyataka yote aya
Inauma sana itakuwa! 😢5 nyingi jamani