Tetesi: Wachezaji watano wa Simba wasimamishwa kupisha uchunguzi kwa kichapo kikali cha goli 5 kutoka kwa Yanga

Tetesi: Wachezaji watano wa Simba wasimamishwa kupisha uchunguzi kwa kichapo kikali cha goli 5 kutoka kwa Yanga

Inonga, Chama, Kapombe, Kanoute na Baleke.

Hata kama mlikuwa hamumtaki kocha lakini si kwa kuidhalilisha Club kiasi hicho.
 
Bila Simba kurudishwa utamaduni wa kusoma kisomo cha ALALBADIR BAYANA kabla ya mechi itaendelea kuhujumiwa kila siku.

Muwe na utaratibu wa kusoma kisomo kwa wasaliti wa timu.
Muwalishe yamini wachezaji wote na viongozi wote kama wafanyavyo Yanga.

Muone kama Kuna atakayehujumu timu.
Wataisha

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
 
Hata wasipofungiwa kuna umakini wataongeza...
 
UZUSHI NA KUTAFUTA KUWATUPIA WATU LAWAMA.

UONGOZI WA SIMBA NI MCHAFU MNO UNANUKA ZAIDI YA MZOGA.

ANGALIA HAWA WAZEE KWENYE BACKBONE YA SIMBA KIUNGO.

1.Saido mstaafu
2. Ngoma mstaafu.
3. Chama mstaafu.
4. Miquissone mstaafu.
5. Boko mstaafu.
6. Kapombe nampenda sana
7. Shabalala mstaafu
 
UZUSHI NA KUTAFUTA KUWATUPIA WATU LAWAMA.

UONGOZI WA SIMBA NI MCHAFU MNO UNANUKA ZAIDI YA MZOGA.

ANGALIA HAWA WAZEE KWENYE BACKBONE YA SIMBA KIUNGO.

1.Saido mstaafu
2. Ngoma mstaafu.
3. Chama mstaafu.
4. Miquissone mstaafu.
5. Boko mstaafu.
6. Kapombe nampenda sana
7. Shabalala mstaafu
FB_IMG_16993792421909185.jpg
 
Wasiivuruge timu, duniani kote timu kubwa kufungwa goli 5 au zaidi ni kitu cha kawaida
Yaani kweli ujue Simba hawana uongozi pale. Mo sio kiongozi wa taasisi kubwa kama Simba. Yule ameandaliiwa kuongoza biashara zilizo tayari. Tajiri gani anashindana maneno mitandaoni mpaka na wachezaji?. Utoto mwingi.

Halafu ukiangalia hata mwenendo wa kocha ndio mechi ya kwanza anafungwa. Watafukuza sana makocha na kusimamisha sana wachezaji. Kwa YANGA hii bado mechi ya round ya pili watakula tena,wasambaratike tena
 
Kama wana ushahidi wapeleke TAKUKURU ndo tutajua wapo serious na hizo tuhuma kinyume na hapo naona kama tunatafuta kupeana moyo kuwa haikuwa kufungwa kwa kawaida.
Hapo wanatafuta kufurahisha mashabiki. Wakati huo huo wao wakiendelea kuhangaika tayari mashabiki walishaona kitambo UDHAIFU wa timu yao. Pia wajue mpira unachezwa sehemu za wazi mashabiki wao waliiona kila kitu
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Mbuzi wa kafara anatolewa ila tatizo linajulikana...Uongozi wa juu hadi benchi la ufundi


Yanga endeleeni kuwavuruga
 
Inonga kawa hovyo sana siku hizi , hii mechi ya juzi kacheza chini ya kiwango sana...huenda alivuta chake mapema.
Yule mdebwedo tu. Beki gani laini vile?. Beki anajibadiri rangi? Beki uliza Gatuso
 
Ushahidi wa miala ya ya kutisha wote ndani ya muda mmoja like roborted transactions.. Then sijui nani aliruhusu waende disco usiku mmoja kabla ya derby.. hapa mistake ndio ilipoanzia.
Hakuna lolote. Mnajipoteza tu. Hakuna yoyote atakaeleta ushahidi wa namna hiyo.
 

Wachezaji watano wa Simba Sc akiwemo Enock Inonga na Clatous Chota Chama wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yao baada ya kufungwa na Yanga SC mabao 5-1 siku ya Jumapili.

Wachezaji hao wanatuhumiwa kuihujumu timu kitendo kilichopelekea kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao.

Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao cha bodi ya Wakurugenzi ya Simba kilichofanyika jana jijini Dar es salaam.

Chanzo cha uhakika kutoka Simba SC kimeiambia Kishamba Media kuwa uongozi umeshapata ushahidi wa awali kuhusu tuhuma dhidi ya wachezaji hao na sasa imeanza uchunguzi wa kina ili kujiridhisha.

Wachezaji hao watakua nje ya kambi ya timu mpaka hapo maamuzi mengine yatakapofanyika.

Chanzo hicho kimesema huwenda leo klabu ya Simba ikatoa taarifa ya wazi kwa Umma juu ya maamuzi waliyofikia kuhusu wachezaji hao au wasitoe ila wahusika wamepewa taarifa.

Maamuzi mengine yaliyofikiwa na bodi ni kufutwa kazi kwa kocha mkuu Robertinho, msaidizi wake pamoja na kocha wa viungo.

Kishamba Updates
Simba wanahitaji ushauri nasaha, (Counselling)
 
Uongozi wa Simba hamnazo, badala ya kuangalia mapungufu na kuyarekebisha wameingiza uswahili kwa huu upuuzi,mechi imechezwa mchana kweupe watu wameona uhujumu unatoka wapi?

Kiakili ya kawaida ukimuuliza mtu Kati ya Simba na Yanga ipi timu Bora bila kuweka ushabiki atakwambia Yanga ni Bora wamewekeza kwenye usajili na wamefanikiwa kwa hiyo na hizo timu zilizo kula tano zilipewa hela?

Kwa akili hizi Simba haiwezi kufikia levo za kina Al ahly.
 
Chama siku hizi kaanza kuvuta bangi na kutafuna mirungi au kazidisha matumizi
 
Back
Top Bottom