Wachezaji wenye majina makubwa kung'olewa Taifa Stars

Wachezaji wenye majina makubwa kung'olewa Taifa Stars

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio kauli mpya kutoka kwa Serikali ya Tanzania aliyoitoa Waziri wa Michezo Mh Mchengerwa , akiongea na wanahabari amesema kwamba wachezaji wenye majina makubwa (Hakuwataja majina) hawajitumi kwa ajili ya Nchi yao , hivyo hawapaswi kuwemo kwenye Timu ya Taifa.

Bali amesema kwamba tayari wameomba fedha wanazotarajia kuzitumia ili kusaka vipaji vipya mitaani na kukusanya damu mpya itakayounda Timu ya Taifa .
 
Sawa sio vibaya damu changa pia zipewe nafasi ya kuonyesha vipaji
 
Sio suluhisho.

Pamoja na kuhitaji wachezaji wazalendo lakini pia Maslahi (Malipo mazuri) ni muhimu sana kwa wachezaji ili kujituma.

Hakuna mchezaji atajitoa mhanga avunjike uwanjani halafu asipate caring yoyote.

Watajituma kwenye club zao lakini sio kwa timu ya Taifa awe na jina kubwa au dogo.
 
Hii ndio kauli mpya kutoka kwa Serikali ya Tanzania aliyoitoa Waziri wa Michezo Mh Mchengerwa , akiongea na wanahabari amesema kwamba wachezaji wenye majina makubwa (Hakuwataja majina) hawajitumi kwa ajili ya Nchi yao , hivyo hawapaswi kuwemo kwenye Timu ya Taifa.

Bali amesema kwamba tayari wameomba fedha wanazotarajia kuzitumia ili kusaka vipaji vipya mitaani na kukusanya damu mpya itakayounda Timu ya Taifa .

Hawawezi kuwekeza kwenye michezo, hao wachezaji have nothing to lose
 
Hivi vichekesho utavikuta Tanzania pekee.
Naunga mkono hoja ili mkija kupigwa za kutosha mbaki mnalaumiana na warugaruga wenzenu.
 
Stars haitakiwi kuundwa na Simba na Yanga..

Shida iko hapo tuu!!
 
Hii ndio kauli mpya kutoka kwa Serikali ya Tanzania aliyoitoa Waziri wa Michezo Mh Mchengerwa , akiongea na wanahabari amesema kwamba wachezaji wenye majina makubwa (Hakuwataja majina) hawajitumi kwa ajili ya Nchi yao , hivyo hawapaswi kuwemo kwenye Timu ya Taifa.

Bali amesema kwamba tayari wameomba fedha wanazotarajia kuzitumia ili kusaka vipaji vipya mitaani na kukusanya damu mpya itakayounda Timu ya Taifa .
Yale yale...hatujuagi kung'amua nini hasa tatizo.
Kwani hao wachezaji wanajileta wenyewe kwenye timu au ni makocha ndio wanaowaita? Hatupo serious kabisa.
Na je kwa nini hao wachezaji hawajitumi wakiwa timu za taifa na wanajituma wakiwa kwenye vilabu vyao?
 
Sio suluhisho.

Pamoja na kuhitaji wachezaji wazalendo lakini pia Maslahi (Malipo mazuri) ni muhimu sana kwa wachezaji ili kujituma.

Hakuna mchezaji atajitoa mhanga avunjike uwanjani halafu asipate caring yoyote.

Watajituma kwenye club zao lakini sio kwa timu ya Taifa awe na jina kubwa au dogo.
Waingereza wana msemo wao "it is an honor and privilege to play for ur national team, but remember its ur club that pays ur salary"

Tatizo kubwa africa ni kwamba hatuwathamini wachezaji wetu ikija kwenye national teams. Tunakimbulia oh hawana uzalendo. Uzalendo wapi bwana ile ni kazi mbona mawaziri nao tukisema hawana uzalendo itakuwa tumekosea?
 
Sasa yeye mchengerwa ana uzalendo gani? Wasilete hizi siasa zao za kipuuzi kwenye mpira. Let them stay away kabisa....badala aseme anataka achote hela kwa kisingizio cha kusaka vipaji,analeta ngonjera hapa. Huu ni mpira asitake kutugawa.
 
Kweli kabisa....itarudi ile story ya taifa stars maboresho chini ya malinzi🤣🤣🤣🤣
Bongo bwana tunapelekwa kama wendawazimu.
Hakika tanzania ni channel ya comedy huko mbinguni
 
Stars haitakiwi kuundwa na Simba na Yanga..

Shida iko hapo tuu!!
Spain yenyewe inaundwa na wachezaji wengi wa Barcelona na Real Madrid miaka nenda! Ukienda Ujerumani ni Bayern Munich na Borusia Dortimund! Hivyo tatizo siyo simba na Yanga! Tatizo letu kubwa ni ukosefu wa wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuchezea timu ya Taifa. Kiufupi wachezaji wetu wengi ni average.

Ukitaka wachezaji wasitokane na simba na Yanga, basi Waziri anatakiwa kushauriwa kuwekeza fedha nyingi katika timu za vijana, na pia kupeleka vijana wengi kwenye academy za vilabu vikubwa Ulaya, ili baadaye wacheze kwenye hivyo vilabu! Na mwisho wa siku warudi kuja kulisaidia Taifa lao, kama ilivyo kwa nchi nyingi za Afrika ya Magharibi, nk.

Hii story ya kutafuta wachezaji wenye vipaji mtaani, haina tofauti na ule mchakato wa timu ya Taifa Stars ya Maboresho enzi zile! Mamilioni yalipigwa na wajanja, halafu tukaambulia kuwapata akina Mgeveke, na wenzake wengi tu wa kiwango cha kawaida kabisa.
 
Nadhani watanzania wote tunakubaliana waziri Mchengelwa ndio waziri aliyeonesha uwezo mdogo sana tangu hii nchi ipate uhuru wake mwaka 1961.

Pale wizarani hakuna jipya analofanya. Na shida kubwa ni kwa kuwa yeye ni waziri lakini hajui lolote kuhusu mambo anayoyasimamia. Hajui kuhusu sanaa hajui kuhusu michezo hajui kuhusu burudani.

Mama ikikupendeza mtafutie kazi nyingine au kama unashindwa basi mpeleke hata wizara ya uvuvi uko.

Wizara yake inasimamia industries zinazokuwa kwa kasi na zimekuwa mbadala wa ajira zinatoa ajira sana lakini waziri bado anafikiri so 1980s.

Waziri hajui hata timu ya taifa inahitaji nini ili isonge mbele. Anaanza mpaka kupanga kikosi 🤣🤣

Waziri anataka maelezo ya bondia ambaye wizara yake haijawai hata kumnunulia maji ya mia 5 😂😂

Waziri anasikiliza arbitration ya biashara ya muziki anajenga hoja kwa mifano ya mtoto akikuwa anaondoka nyumbani akajitafutie 🤣🤣

Yani hapa mama ulituangusha sana ebu fanya jambo huyu mtu watu wamemchoka si wasanii si wanamichezo wote hawamtaki.
 
Halafu anavyotumiaga nguvu nyingi kupayuka unaweza hisi Yuko serious kumbee
 
Back
Top Bottom