Wachina wakamatwa wakizalisha vinywaji feki Dar?

Wachina wakamatwa wakizalisha vinywaji feki Dar?

Inasukitisha unawakamata na kutangaza. Wangekuwa wanawaua kimya kimya hii kitu isingekuwepo
 
Chupa tupu za K-Vant zimepangwa nje ya nyumba.

Mzigo wa Moet & Chandon umepigwa picha ndani ya karakana.

Wachina wawili wamepigwa picha pekee yao.

Kwa ufupi, hakuna kiashiria chochote kuwa hapo ni Tanzania.

Tufanye hapo ni USA
 
USHINDANI WA KIBIASHARA.

Hao ni KONYAGI na vinywaji vingine wanataka kuchafua K Vant.

Hizo picha hazifanani wala hazihusiani. Pia source ya hiyo habari ni ipi? Hakuna TV, radio, gazeti, wala mitandao ya kijamii iliyoripoti.
 
Na kwao wameongeza mtoto mmoja hadi watatu, hao wote destination ni Africa......Mama Samia kusema wawekezaji waje na watu wao watakavyo baada ya miaka 5 tutaona mengi, nimefanya kazi na wachina kwa miaka fulani,ni hatari kwa taifa
 
Tangu nimshuhudie mmiliki wa kiwanda cha K-Vant anakunywa Konyagi nilijipiga stop ya kinywaji hicho maybe nae alishakutana na cha mchina kikamfanya kitu mbaya sana 😀😀😀😀😀😀
 
Kama ni mla K Vant na Moet, basi hii ni kwa ajili yako. Yasemekana hao mabwana kutoka Asia ya Mashariki wamekamatwa jijini Dar wakiwa kwenye ‘karakana’ yao la kufyatua kopi za vinywaji hivi murua.

Hivi huwa wanapataje vifungashio visivyotia shaka?

Kwa uchafu wa hayo madumu, huenda yanahifadhia molasses. Na kama ndivyo, ningependezwa kuona mtambo wao na mchakato wa kukopi ladha na harufu za hivi vinywaji. Bado nabaki na maswali kedekede.

Nimestushwa zaidi na hiyo paint roller na rangi kwenye beseni, sijui vina kazi gani Mungu wangu!

View attachment 1899801View attachment 1899802View attachment 1899805View attachment 1899809
Hawa waondolewe nchini warudi kwao mbele ya safari watatumaliza
 
Hizi pombe kali hazifai nyingi hazifai tena sjui kwa vile vinafyatuliwa feki!!! Juzi nimestop pombe kama miezi 2 hivi coz nlikunywa nikapoteza kumbukumbu kabisa hadi home nikapasahau,sa hiyo ni pombe au sumu.hao wachina wapewe adhabu kali
Pombe kali nyingi feki....
Ndomana watu wengi wanapatwa
Na matatizo ya kuona
Mimi ndomana nkitaka kununua pombe zangu
Nikiwa dar mara nyingi nachukuliaga mohans

Ova
 
Kuna kitu kipya kinaitwa Crown100 vodka. Jaribu kiongozi

Kuna Crown100 vodka imekaa vizuri ,haina harufu na itachukua muda kufeki.
Wanasema "kizuri share na wenzako" check out this

16294680444068787337588934920880.jpg
 
Back
Top Bottom