Wachina wamejipiga pini kwenye vita ya ushuru, Soko kubwa dunia nzima lipo Marekani

Wachina wamejipiga pini kwenye vita ya ushuru, Soko kubwa dunia nzima lipo Marekani

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
933
Reaction score
3,051
Vita inayoendelea ya kupandishiana ushuru kati ya Marekani na China (ongeza niongeze) imekula kwa China, wamejipiga pini kwa kuona ni sifa kubwa kusifiwa sio waoga lakini Marekani inazidi kufurahia hii vita, Marekani wapo tayari hata kufikia hatua ya kuongeza ushuru wa China kuwa asilimia 400, Lengo ni kumtia adabu China kwa kumbania soko, Marekani ndio soko linalomtajirisha China kuzidi soko lolote hapa Duniani

Mchina kaja kustukia mchezo baadae sana, kwenye kupandishiana ushuru ghafla Marekani kaziruhusu nchi nyingine kuingiza bidhaa zao kwa asilimia 10 tu. Mchina anaingiza pesa nyingi zaidi kupitia soko la Marekani, kilichofanya na Marekani ni kuwafungia China na kuruhusu nchi nyingine kulifaidi soko lake, hili ni teke zito katikati ya mapaja ya China.

Hii ni zaidi ya drafti, hii ni chess, China kafungiwa kwenye soko la Marekani, meanwhile nchi nyingine zinaenda kulionja soko tamu la Marekani kwa ushuru wa 10% tu huku China wanatozwa 125 % waliyojipandishia wao kwa kunogewa na mchezo wa pandisha nipandishe, nchi nyingi zinaombea ushuru wa China uongezeke zaidi ili wao wale mema ya soko la Marekani.

Marekani kaona China anatajirika sana kupitia soko lake, hii ni mikakati ya kumdhibiti mchina kwa kuziwezesha nchi nyingine ziteke baadhi ya masoko yaliyokamatwa na China, hii ni plan imeundwa kimkakati kabisa.

China imekuwa ikishikilia soko la bidhaa zake nchini Marekani kwa wastani wa takriban dola bilioni 500 kila mwaka (shilingi trilioni elfu moja na bilioni 300). Hivyo basi, kama China itapoteza baadhi ya masokko ya Marekani kwasababu ya Ushuru, soko likapungua hata kwa dola bilioni 200, hilo litakuwa pigo kubwa kwa China.

Kampuni nyingi zimeanza commitment ya kuhamishia viwanda nchi zingine au kurudi Marekani, Kutengenezea bidhaa China ni kulikosa soko kubwa zaidi duniani.


Katika hii process soko la hisa la China limeshuka kwa kiwango kibaya zaidi tangu mwaka 2008
 
Marekani anatutoza Tanzania ushuru wa 10% kwa sababu gani, tumemkosea nini? Kitu gani Marekani ametaka auze Tanzania tukamkatalia?

Trump hana huruma, Tanzania ni mojawapo ya nchi masikini zaidi Duniani, hakuna huruma hata kidogo?
 
Vita inayoendelea ya kupandishiana ushuru kati ya Marekani na China (ongeza niongeze) imekula kwa China, wamejipiga pini kwa kuona ni sifa kubwa kusifiwa sio waoga lakini Marekani inazidi kufurahia hii vita, wao wapo tayari hata kufikia hatua ya kuongeza ushuru wa China kuwa asilimia 400, lengo kuu ni kuwadhibiti wachina,

Mchina kwa upande mwengine kaja kustukia mchezo baadae sana, kwenye kupandishiana ushuru ghafla Marekani kaziruhusu nchi nyingine kuingiza bidhaa zao kwa asilimia 10 tu.

Kilichofanya ni zaidi ya drafti, hii ni chess, China imejitafutia sababu ya kufungiwa kwenye soko la Marekani kwa wao kunogewa na mchezo wa ongeza niongeze, meanwhile nchi nyingine zinaenda kulionka soko tamu la Marekani kwa ushuru wa 10% tu,

Kampuni nyingi zimeanza commitment ya kuhamia nchi zingine au kurudi Marekani, Kutengenezea bidhaa China ni kulikosa soko tamu duniani.

Katika hii process soko la hisa la China limeshuka kwa kiwango kibaya zaidi tangu mwaka 2008
Mbona hizo nchi hazikuuza huko hata kabla ya kuwekewa 10%?
Trump alitegemea china kabla ya leo awe ameomba deal, leo naye kaongeza tariff hadi 125% na kasema baada ya hapa hataongeza tena tariff maana namba kufikia hadi sasa hazimake sense tena ni kama no business at all.
China hataki kupiga magoti maana demands za marekani haziishi. Demand zake zinabadilika.
 
Marekani qnatutoza Tanzania ushuru wa 10% kwa sababu gani, tumemkosea nini? Kitu gani Marekani ametaka auze Tanzania tukamkatalia?

Trump hana huruma, Tanzania ni mojawapo ya nchi masikini zaidi Duniani, hakuna huruma hata kidogo?
Huruma hakuwaonea penguins awaonee wa tz 😀😀 (joke)

Ulitaka upeleke bidhaa bure bila ushuru?
Tanzania mnatoza asilimia ngapi kwa bidhaa ya Us.
 
Mbona hizo nchi hazikuuza huko hata kabla ya kuwekewa 10%?
Trump alitegemea china kabla ya leo awe ameomba deal, leo naye kaongeza tariff hadi 125% na kasema baada ya hapa hataongeza tena tariff maana namba kufikia hadi sasa hazimake sense tena ni kama no business at all.
China hataki kupiga magoti maana demands za marekani haziishi. Demand zake zinabadilika.
Kabla ya hiyo press kuisha kasema milango ya majadiliano iko wazi.
Alimaanisha nini kama hataki kupiga magoti? Why aseme hataongeza tena?
 
Kabla ya hiyo press kuisha kasema milango ya majadiliano iko wazi.
Alimaanisha nini kama hataki kupiga magoti? Why aseme hataongeza tena?
Kasema hawaendi kuomba deal kwa kutishia na bullying, kasema njia hizo hazifanyi kazi kwa china. Angekuwa anataka deal asingeongeza tariff kwa US. Trump ndiye alidhani kwa kuwashushia wengine china atakuja kuomba deal kwaho yake.
 
Vita inayoendelea ya kupandishiana ushuru kati ya Marekani na China (ongeza niongeze) imekula kwa China, wamejipiga pini kwa kuona ni sifa kubwa kusifiwa sio waoga lakini Marekani inazidi kufurahia hii vita, Marekani wapo tayari hata kufikia hatua ya kuongeza ushuru wa China kuwa asilimia 400, lengo kuu ni kuwatia adabu wachina.

Mchina kaja kustukia mchezo baadae sana, kwenye kupandishiana ushuru ghafla Marekani kaziruhusu nchi nyingine kuingiza bidhaa zao kwa asilimia 10 tu.

Hata wewe ungejaa kwenye mfumo, hapo kabla Marekani ilitengeneza script kuonekana inatoza kila nchi ushuru mkubwa, China akaamini wapo kundi moja, Mara paap out of nowhere Marekani anapunguza ushuru kwa nchi nyingine lakini anaendelea kula sahani moja na mchina.

Kilichofanya ni zaidi ya drafti, hii ni chess, China kafungiwa kwenye soko la Marekani, meanwhile nchi nyingine zinaenda kulionja soko tamu la Marekani kwa ushuru wa 10% tu, nchi nyingi zinaombea ushuru wa China uongezeke zaidi ili wao wale mema ya soko la Marekani.

Kampuni nyingi zimeanza commitment ya kuhamia nchi zingine au kurudi Marekani, Kutengenezea bidhaa China ni kulikosa soko tamu duniani.

Katika hii process soko la hisa la China limeshuka kwa kiwango kibaya zaidi tangu mwaka 2008
Marekani hawezi ku survive hii vita kwa sababu anamtegemea sana Mchina kupata cheap products kuanzia electronics mpaka ma toys mpaka nguo.

Watu waliokwishazoea kununua cheap products za kutika China huko Walmart na Amazon.com ukiwauzia vitu hivyo mara tatu ya bei ya sasa wanaweza hata kumuua Trump.

Unaishi nchi gani mkuu?
 
Kasema hawaendi kuomba deal kwa kutishia na bullying, kasema njia hizo hazifanyi kazi kwa china. Angekuwa anataka deal asingeongeza tariff kwa US. Trump ndiye alidhani kwa kuwashushia wengine china atakuja kuomba deal kwaho yake.
Fatilia vizuri, kasema milango ya majadiliano iko wazi baada ya kusema hataongeza tena.
 
Mbona hizo nchi hazikuuza huko hata kabla ya kuwekewa 10%?
Trump alitegemea china kabla ya leo awe ameomba deal, leo naye kaongeza tariff hadi 125% na kasema baada ya hapa hataongeza tena tariff maana namba kufikia hadi sasa hazimake sense tena ni kama no business at all.
China hataki kupiga magoti maana demands za marekani haziishi. Demand zake zinabadilika.
Nchi nyingi hazikuweza kuuza soko la Marekani kwasababu Mchina aliteka soko.

Kilichofaywa ni kupunguza nguvu ya China kwa kuwatoza ushuru mrefu huku nchi nyingine zikitozwa 10% tu

China anapata pesa nyingi sana kupitia soko la Marekani, hiki alichofanyiwa ni teke la Taekondoo katikati ya mapaja
 
Marekani hawezi ku survive hii vita kwa sababu anamtegemea sana Mchina kupata cheap products kuanzia electronics mpaka ma toys mpaka nguo.

Watu waliokwishazoea kununua cheap products Walmart na Amazon ukiwauzia vitu hivyo mara tatu ya bei ya sasa wanaweza hata kumuua Trump.

Unaishi nchi gani mkuu?
Yaani Marekani anamtegemea china? How China ndiyo anamtegemea Marekani
 
Nchi nyingi hazikuweza kuuza soko la Marekani kwasababu Mchina aliteka soko.

Kilichofaywa ni kupunguza nguvu ya China kwa kuwatoza ushuru mrefu huku nchi nyingine zikitozwa 10% tu

China anapata pesa nyingi sana kupitia soko la Marekani, hiki alichofanyiwa ni teke katikati ya mapaja
Jiulize kwanini walishindwa kupambana naye mpaka akawapiku. Si kitu kinatokea over night nchi inakuwa main manufacturer wa bidhaa.
 
Fatilia vizuri, kasema milango ya majadiliano iko wazi baada ya kusema hataongeza tena.
Sio kufuatilia tu dakika chache zilizopita nimetoka kuangalia hotuba yake iliyotafsiriwa kwa kiingereza. Pia nimesikiliza hotuba ya minister of finance.
Jana baada ya pause ya tariff, soko la hisa liliemda poa ila leo baada ya china kuongeza tariff soko la hisa limefunga likiwa chini kasoro India.
 
Yaani Marekani anamtegemea china? How China ndiyo anamtegemea Marekani
Marekani anamtegemea m China kupata cheap labor na cheap products.

Hizo tariffs zikiwa in effect vitu vitapanda bei mara tatu na Marekani watu watashindwa kununua.

Na hata kuhamisha production kutoka China si kitu cha kufanya mara moja.

Wamarekani wakipata arosto ya kukosa bidhaa za bei chee kutoka China kwa mwezi mmoja tu, kutatokea machafuko makubwa Marekani.

Ndiyo maana Stock Markets za Marekani zimeanguka Mpaka Trump kaondoa ujinga wake wa tariffs za ajabu dunia nzima, kabakisha 10% tu na tariff kubwa kabakiza China, na huko China atapunguza mwenyewe.

Ndiyo maana Trump kaanza kuomba kupigiwa simu wayajenge na Mchina.

Wakati Mchina kasema ukimwaga ugali namwaga mboga wala sikupigii simu.
 
Kuna kitu hamkielewi... Laiti mngekielewa basi ingekua ni fursa kwenu

Maisha yanamtaka mtu mwenye macho mengi or mwenye jicho 1 linalozunguka kama dishi la kutazama matrilion ya kilometers
 
Back
Top Bottom