Wachungaji mnaosema tukiwapa sadaka tutabarikiwa kuwa wateja wa kwenye ma Mall, mnajiona mko sawa?

Wachungaji mnaosema tukiwapa sadaka tutabarikiwa kuwa wateja wa kwenye ma Mall, mnajiona mko sawa?

Sadaka hutolewa kwa wenye uhitaji wakiwemo waumini wa kawaida na maskini. Inawezekana kabisa mchungaji naye akawa na miradi ya kumsaidia na kuwasaidia waumini wake.

Pamoja na haki ya mchungaji kupata chochote toka kwa waumini, lakini ni vema asiwalemee. Ajipatie mapato yake, aanzishe miradi ya kumpatia chakula na fedha.

Mtume Paulo hakutaka kuwanyonya waumini, hakula chakula cha bure kwa yeyote, alitafuta mapato yake ikiwemo kushona mahema na kuwasaidia wengine. Hiyo inapendeza! 2 Wathesalonike 3:7-9
 
Umeeleza vizuri sana. Zamani 10% ilikuwa kwa ajili ya makuhani Walawi. Na kwa sasa kila amwaminiye Kristo na kuokoka ni kuhani. Aidha, utoaji ni suala la hiari ya moyoni pasipo mashinikizo. Hata ukitoa vyote au 90% ni sawa tu.
Swali: "Biblia inasemaje juu ya kutoa fungu la kumi?"

Jibu: Kutoa fungu la kumi ni jambo ambalo wakristo wengi hung’ang’ana nalo. Katika makanisa mengine kutoa fungu la kumi imesisitizwa kupita kiasi. Wakristo wengi pia hukataa kutii agizo la kutoa sadaka kwa Bwana. Kutoa fungu la kumi au sadaka inahitajika kuwa ni kitendo cha furaha na baraka. Lakini sivyo katika makanisa ya sasa.

Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale. Hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5). Wengine huchukulia ya kuwa fungu la kumi, katika agano la kale ilikuwa kama sehemu ya ushuru uliokuwa ukitolewa kwa ajili ya makuhani na walawi. Agano jipya haiamrishi wala kupendekeza mfumo halali wa kutolea fungu la kumi. Paulo asisitiza kuwa waumini watenge sehemu ya mapato yao kwa ajili ya kusimamia kanisa (wakorintho wa kwanza 16:1-2).

Agano jipya halielezi kiasi cha pato ambacho ni kitengwe kwa ajili ya kusimamia kanisa. (wakorintho wa kwanza 16:2). Kanisa la kikristo leo limechukua kile kiwango cha fungu la kumi kutoka kwa agano la kale na kukisisitiza kuwa ndicho kiwango cha chini cha mkristo kutoa. ijapokuwa agano jipya haitoi kiwango cha kutoa, inaelezea umuhimu na manufaa ya kutoa. Ni watoe sawa na uwezo wao “ kulengana na pato lake.” Wakati mwingine ina maana ya kutoa zaidi ya fungu la kumi, na mara nyingine kichache kuliko fungu la kumi. Yote hutegemea uwezo wa mkristo mwenyewe na mahitaji ya kanisa. Kila mkristo sharti aombe na kutafuta hekima kutoka kwa Mungu juu ya swala hili (Yakobo 1:5). “ kila mtu niatoe kile alicho azimia kutoa kutoka ndani ya moyo wake, si kwa manung’uniko wala kulazimishwa, kwa kuwa Mungu hupenda kwenye kutoa kwa moyo mkunjufu” (wakorintho wa pili 9:7).
 
Silijui kanisa kutoka nilipopata kipa imara, lakini Mungu kaniinua sana,ili kufanikiwa si lazima utoe sadaka kwa matapeli au makanisani,sadaka haimuinui mtu,sadaka kazi yake ni kusaidia kutoa huduma za kanisa kama vile kulipa mishahara,kulipia anakara mbalimbali lakini hawa akina Fekero huzifanya sadaka za wajinga ndio mtaji wao wa maisha ya kifahari na wapambe wao, na si akina Mwingira tu bali hawa matapeli wamejaa duniani kote,wanatumia ujinga au shida za waumini kujitajirisha,dini ishakuwa biashara,wakati mwingine naona wenzetu Waislamu angalau wanamuogopa Mungu kuliko sisi Wakristo ambao kila kukichwa huwadanganya binadamu kwa kumtumia Mungu.Ni sisi wakristu ambao sasa tumeanza hata kuhalalisha ndo za jinsia moja,si ajabu Waislamu wanatuita makafiri kutokana na tabia zetu za hovyo.
Well said!
 
Kuna hadithi moja niliwahi kuikuta mtandaoni kwamba kuna binti mmoja alienda kuwasalimu wazazi wake kijijini akiwa na usafiri wake binafsi.

Siku ya kuondoka, wazazi wake wakamfungashia zawadi za kwenda nazo mjini yakiwemo mayai ya kienyeji kwani wazee walikuwa ni wafugaji.

Wakati anataka kuianza safari mama yake mzazi akamwambia, "mwanangu Mungu akutangulie", kwa kebehi yule binti akamjibu, "mama achana na huyo Mungu wako asiyekuwepo!".

Akawasha gari yake akaondoka. Njiani akapata ajali mbaya sana akafariki palepale, mwili wake haukuweza kutambulika kabisa, lakini cha ajabu YALE MAYAI YALIBAKI SALAMA, HAKUNA LILILOVUNJIKA HATA MOJA. Narudia tena, Mungu hadhihakiwi hata kidogo.

Nakusihi sana mtoa uzi ujitafakari, ukiona inafaa uufute kabisa huu uzi na ukaitubu hii dhambi.
 
Hahah mmenye umekomaa na hiyo mistari...!

Acha tu Mmenye,hawa matapeli kwa kisingizio cha dini wanaudhi sana!! Wanawaibia waamini wao fedha kwa kisingizio cha kuwaponya...wachungaji wenye character kama hizo ndio wawaponye watu? Bora nisali kwenye CHAPEL yetu mwenyewe nipate UPAKO.
 
Mchungaji anasema toa upate baraka, utanyeshewa baraka za kukuinua, hutakua mtu wa magengeni tena, hutakua mtu wa kununua mitumba tena utanunua nguo kwenye ma shoping mall na mahitaji yako yatatoka supermarket.

Hizi hela tulizonazo tungeamua kuwa watu wa manunuzi ya supermarket na shopping malls tusingebaki na hela ya kuwapa nyinyi. Vitu nya magengeni ni fresh zaidi kuliko vya supermarket.

Muwe mnafikiria kabla ya kutoa kakuli zenu. Wenye magenge pia wana familia za kulisha na watoto wa kusomesha.
Shemeji kwa nini unaenda aunkiwasikiliza hawa watu wa hivi?
 
Kuna hadithi moja niliwahi kuikuta mtandaoni kwamba kuna binti mmoja alienda kuwasalimu wazazi wake kijijini akiwa na usafiri wake binafsi.

Siku ya kuondoka, wazazi wake wakamfungashia zawadi za kwenda nazo mjini yakiwemo mayai ya kienyeji kwani wazee walikuwa ni wafugaji.

Wakati anataka kuianza safari mama yake mzazi akamwambia, "mwanangu Mungu akutangulie", kwa kebehi yule binti akamjibu, "mama achana na huyo Mungu wako asiyekuwepo!".

Akawasha gari yake akaondoka. Njiani akapata ajali mbaya sana akafariki palepale, mwili wake haukuweza kutambulika kabisa, lakini cha ajabu YALE MAYAI YALIBAKI SALAMA, HAKUNA LILILOVUNJIKA HATA MOJA. Narudia tena, Mungu hadhihakiwi hata kidogo.

Nakusihi sana mtoa uzi ujitafakari, ukiona inafaa uufute kabisa huu uzi na ukaitubu hii dhambi.
Hii siyo hadithi, ni kisa halisi cha kweli. ^Individuals who Blasphemed God^
 
Mchungaji anasema toa upate baraka, utanyeshewa baraka za kukuinua, hutakua mtu wa magengeni tena, hutakua mtu wa kununua mitumba tena utanunua nguo kwenye ma shoping mall na mahitaji yako yatatoka supermarket.

Hizi hela tulizonazo tungeamua kuwa watu wa manunuzi ya supermarket na shopping malls tusingebaki na hela ya kuwapa nyinyi. Vitu nya magengeni ni fresh zaidi kuliko vya supermarket.

Muwe mnafikiria kabla ya kutoa kakuli zenu. Wenye magenge pia wana familia za kulisha na watoto wa kusomesha.

Wenye magenge pia wana familia za kulisha na watoto wa kusomesha.[/QUOTE]

Na wanatoa sadaka vile vile!? [emoji848][emoji848][emoji16]
 
Mchungaji anasema mimi nimebarikiwa nimeacha kupanda daladala sasa hivi nina Mercedes Benz wakati sisi tunaokupa sadaka zetu tulipanda daladala ili tufike kanisani.
Logic [emoji39][emoji847]
 
Kwahyo kutokuvunjika mayai kuna maanisha nini haswa?

Btn kwenye ajali chochote kinaweza kutokea...ndo maana wengine wanakufa wengine wanatoka bila hata mchubuko kwenye ajali ....

Hizi dhana ya kutovunjika mayai....sio exception kabsa
.

Hii siyo hadithi, ni kisa halisi cha kweli. ^Individuals who Blasphemed God^
 
Kwahyo kutokuvunjika mayai kuna maanisha nini haswa?

Btn kwenye ajali chochote kinaweza kutokea...ndo maana wengine wanakufa wengine wanatoka bila hata mchubuko kwenye ajali ....

Hizi dhana ya kutovunjika mayai....sio exception kabsa
.
Pengine hata Mungu hakuhusika kwenye hyo ajali , sema Tu watu wanaunganisha doti ili kutisha watu dhidi ya Mungu , kimsingi swala la dini ni compromise Sana , tatizo there is no clear argument kutoka Kwa Mungu Mwenyewe dhidi ya was was mkuu uliopo , hali inakuwa mbaya Zaid pale kunapokuwa na utitiri wa dini zenye ushindani na kurushiana maneno makali na Kila mmoja anadai Mungu yupo upande wake na anamsaidia , swali linakuja who is right ?? Kama Mungu ni mmoja na Imani moja why kunakuwa na hzi tofauti ?? na hakuna clear explanation toka Kwa Mungu mwenyewe yupo kimya .... Hii issue ina utata Mkubwa Sana
 
1. Hakuna kitu chenye utata kuhusu Mungu

2. Uwepo wa dini mbalimbali is never a counter-argument dhidi ya existence ya Mungu, bali ni proof of His very existence

3. Mungu hayuko kimya. As a matter of fact, He communicates with us every moment, variously.

4. If you want to know, you will know.

5. Kisa hicho kilichoelezewa ni very unique and has no human explanation, unless kama hujawahi kukisikia.
 
Wakatoliki hawalazimishani sadaka, ni Walibi wako kutoa sadaka na fungi la kumi lakini hawaitwi waliotoa watoke mbele.
Mkuu unaamini wewe ndiye mkatoliki pekee humu?

Misa ya last Sunday parokiani niliposali somo lilijikita kwenye utoaji

Watu kuitwa mbele huo ni utaratibu tu, sisi wakatoliki pia tuna namna zetu

Ni checklist ipi inaonesha hiki cha wakatoliki ndicho sahihi ila hili hapa Lutheran's, Adventists etc sio sawa?

Na hao walokole hawajawahi kulazimisha mtu sadaka, ila wanawahimiza

Kama unaamini taasisi ya kidini ambayo ni pure non profit org inaweza endeshwa bila michango ya watu.... you're getting it all wrong.

Mada yako uliileta vizuri sana, ila (in my humble opinion) katikati ya mada umekosa kuonesha lengo lilikua lipi haswa

Umeruka huku na kule ili mradi ujibu comments za wadau mfano stroke na aweso

Kuanzisha thread kusilenge kutafuta ushindi, bali kutafuta kujifunza

Ama nasema uongo ndugu zangu?
 
Walawi walikuwepo Israel enzi hizo sio bongo ya leo.
Kama ni msomaji mzuri wa Biblia utaona kwamba Walawi walikuwa hawafanyi kazi nyingine yeyote ile isipokuwa ya kumtumikia Mungu madhabahuni na walikuwa na sehemu yao maalum ya sadaka kwakuwa walikuwa hawazalishi.

Hivyo si ajabu kwa Mchungaji sasa kukumbushia haki yake ya Kibiblia kwani kazi yake ni madhabahuni pa Bwana.

Sasa unataka Mchungaji akafungue hoteli kubwa halafu muanze kusema kuwa anazungusha sadaka??

Acheni ukaidi toeni mbarikiwe.

Naam kama unauza genge toa Mungu atakubariki utafungua supermarket.
 
Mkuu Mimi sipingi kabisa utaratibu wa kutoa sadaka maana najua Ni mfumo ambao umebeba lugha ambayo Mungu pekee anaweza kuielewa lakini kile tunachohubiriwa kwamba tutoe ili tubarikiwe huwa naona si Sahihi baraka za Mungu kwetu hazitokani na sadaka tunazotoa

Ayubu 41:11 inaonyesha na kuonya juu ya mfumo wa kutoa kwa kutegemea kupokea kingi kuwa si mfumo wa Mungu Ni biashara ambayo mtu afanyaye hivyo hajui kuwa Kila alichonacho kinatoka kwa Mungu.
 
Back
Top Bottom