Wachungaji mnaosema tukiwapa sadaka tutabarikiwa kuwa wateja wa kwenye ma Mall, mnajiona mko sawa?

Yani baraka utakayoipata hapa ni kubwa mno,nataman watu wengi walione hili.
Huwezi kujua hayo yote bila kufundishwa kwanza huyo anakufundisha ndiyo anayekuelewesha nini maana ya baraka ndipo unatoa sadaka kwa maskini yatima na wagonjwa Sasa yule anayekaa akifundisha neno la Mungu siku nzima unataka ale upepo?.
 
Umesahau kuwa hao Watu wanatoa huduma wanatakiwa wale na wao waishi vizuri?.Utahubiri vipi habari za mafanikio wakati wewe huna uhakika wa Kula wala pakulala.Kama unaona kuhubiri injili ni rahisi ingia na wewe ukusanye Mahela.Nakukumbusha kuwa hizo Ni taasisi na zimesajiliwa wizara ya Mambo ya ndani na siyo kampuni ya biashara useme tuangalie mauzo hasara na faida Hivyo Kama umeweza kumuamini huyo Mtumishi kinakushinda nini kumuamini kwenye hicho kihela chako. Hivi kwa yule Mganga huwa unauliza umepata shilingi ngapi?. Hakuna huduma ya kiroho inayoweza kufanikiwa bila sadaka ndiyo maana hata wachawi wanatoa kafara Sasa Kama wewe hutaki endelea kwenda kutoa nyingi kwa waganga kidogo kanisani au usitoe kabisa.
 
1. Almost all people, Waislamu included, wanaamini fika kwamba alikuwepo hapa duniani Nabii historically kwa jina la Yesu bin Mariam Mnazareti. That in itself should send mind-opening shock waves kwa mtu yeyote anayefikiria kwa umakini. Just in itself hii evidence of testimony inatosha kuleta valid conviction.

2. Kisa cha mayai! Please, explain to me nini kiliyaprotect lisivunjike even one, given gari lote lilikuwa nyang'nyang'a, trei la mayai limeshift position yake ya awali very significantly. Take time to think through it, don't just crush over. Kuhusu Tsunami, na matukio mengine mengi tu ambayo ni superhuman, those are additional evidences in support of the fact that God exists and He is in control.

3. Your definition of ^imani,^ I am afraid, is very rudimentary & superficial. Faith is clearly based on evidence. We don't simply believe in nothing; we believe in substance. Jesus told incredulous Thomas: ^Touch and feel My body!^

4. God is never interested in blind faith, but rather active, reasonable faith. He wants us to come close to Him and reason together with Him. A classic example for this is when He confronted Adam in the Garden. They kept talking and exchanged views; and it did not happen just once or twice or three times. It was regular & habitual.

5. God wants us to investigate the evidences for our beliefs, otherwise it would have been literally unthinkable and even pointless for Him to deliver the Scriptures to us. If you read the Scriptures with open-mindedness & under His divine guidance, you cannot but affirm how much He has sufficiently answered all life's troubling questions and mysteries.
 


Sasa kwanini kusiwepo na uwazi?

Kunafichwa nini?

Mbona kwenye Haya makanisa kongwe ya Roman, KKKT, Anglican n.k kuna uwazi?

Inajulikana mhazini anavyopatikana na kuondolewa?

Mbona majina ya account yapo kwa jina la kanisa na siyo ya mapadre au wachungaji au wake zao au watoto wao?

Nijibu kwa hoja!
 
Mi ndiyo wamenichoshaaa sitaki hata kuwasikia, wana mbinu nyingi za kupata hela.
Wanauza magazeti kanisani
Vitabu
Maji wanakwambia ya upako ila ukienda na yakwako wanakwambia hayata pata upako kwasavabu wabaya wameyaona toka unatoka nayo nyumbani, kwahiyo ni vyema ununue ya kwao
Wanauza mafutaa yani wanabiasharaa murua sana tusipo amkaaa tutazidi Kuwa masikini...
Alafu wanaoshikwa sana ni wanawake, akina mama wenzangu mnakwama wapi??
Yesu alivyokuwa anaponya vilema na vipofu aliwadai sadaka au aliwauzia mafuta

Makanisa mengi sasa hivi ni viwanda vya biashara machache mnoo, ndiyo yapo kwaajili ya ibada
 
Narudia Tena hii siyo kampuni ya kutengeneza faida Ni taasisi ya kuendesha injili.Usilazimishe Watu watumie mfumo uliolelewa na Baba yako .Mbona hujiulizi kwanini kwanini kanisani kwenu hakuna ukemeaji wa mapepo na hakuna miujiza yoyote mpaka waamini wanakwenda hayo Makanisa ya Wachungaji wengine na matatizo yao yanapata nafuu.
 
Sidhani kama uko hata serious. Kama una uchoyo na tupesa twako tudogo hutaki kutoa sadaka, just kaa natwo tutazitumia kukutibia, sawa!???
Wewe ni mchungaji?
Halafu sidhani kama kutoa sadaka ni issue hapa. Issue ni michango ya lazima isiyo na kichwa wala mguu, na wachungaji wengine kumuona ili uombewe unatoa fee na ni kubwa mno kwa mtu wa kawaida. Kubali tu kwamba makanisa ya siku hizi mengi ni usanii na kuiba pesa za waumini ili kujinufaisha, na hii inasababisha watu kuacha kwenda kanisani.
 


Kwa hiyo wewe umeona kutoa mapepo ndiyo ishu?
Hujajibu hoja ya msingi!
Utolewaji wa taarifa umuhimu wake ni zaidi ya unavyoweza kufikiri juu ya hilo swala lako la faida.


Watu wameanza kuwastukia [emoji108][emoji108]
 
@Dilek michango si ndiyo sadaka zenyewe hizo!??? Unaweza kuachaje kwenda church [emoji547]️ 7bb ya michango & sadaka, kama siyo kutawaliwa na uchoyo, ubahili, ubinafsi na love of money!??? Hujui nani kakupa hizo pesa, hiyo nyumba, hilo gari na kiwanja unachoringia!??? Uhai huo pia ni mali ya Mungu. Kwa hiyo uwe mpole ili sadaka yako IPANUE huduma, neno liwafikie wengine wengi waliokuwa bado gizani.
 
Perfect!!! Wakati wa matetemeko na magonjwa ndipo haohao watumishi huonekana wa maaaaanaa.

Wakati wa magonjwa na matetemeko wachungaji huonekana wa maana kivipi!

Ni kitu gani wanaweza kufanya kukabiliana na hayo, hakuna kitu ni ujiko tu hupewa na viongozi wa kisiasa... kwa kuamini kuwa wachungaji wanaaminiwa na wananchi wajinga ambao ni wengi.
 
Halafu ni ajabu kweli Yani wakati mwingine kama kunakuwa na viinimacho sijui?!

Yani mtu unatoa kanisani kuliko kumsaidia mzazi wako?! Au nduguyo ?!

Wakati imeandikwa : “asiyewajali wakwao ni mbaya kuliko hata asiye amini”

Swala la kuwajali watu wakaribu yetu limepewa msisitizo mkubwa sana!

Hapana kuna mahali tujitafakali kwa upya!
 
Sikushangai sana kwa sababu najua ni suala la muda tu. Time is almost always the best antidote. But Mungu aepushie mbali.
 
Yaani wewe unaongea as if huna experience na haya makanisa. Kuna makanisa ili uombewe unatakiwa kutoa sadaka ya ukombozi na wameweka amount sio kwamba unatoa uliyonayo, mara ununue mafuta chupa ya Lita moja elfu 50, maji ya kunywa yenye upako nayo ununue, chumvi na mambo mengine ya kijinga.
Kama huna experience na haya makanisa usibishe tu. Natoka zangu home na sadaka yangu ya 2000 lkn nikifika kanisani inakuwa haitoshi. Ipunguzwe michango isiyo na maana. Sadaka inajulikana umuhimu wake.
 
Mimi sikatai swala la kumtolea Mungu ni muhimu sana kwake yeye aaminiye!

Na niandike kwa ushuhuda kabisa hapa na asomaye na afahamu kwamba kumtolea Mungu kunalipa sana!

Hasa mtu ukitoa kwa siri, kwa Imani na moyo wa ukarimu!

Imeandikwa: utoapo mkono wako wa kulia wakoshoto usijue!

Sasa hizi sadaka za matangazo na changizo msingi wake ni nini? [emoji2369][emoji2369]

Siku hizi mnawafata watu mpaka kwenye whassap group?! [emoji15][emoji15]

Lakini ni wazi kuna mahali upande wa waanzilishi wa hizi huduma na makanisa hapako sawa!

Jitafakalini!
 
Hiyo fedha ni kwa lengo la kuimarishia huduma zaidi. Mambo ya rohoni yana gharama yake pia. Ukishiriki kwa kutoa sadaka yako pale kigangoni ama usharikani kiroho safi hapo unakuwa umeokoa nafsi moja kutoka umautini.
 
Watu wameanza kuwastukia !

Mtaanza kukusanya sadaka kwa nguvu kubwa sana maana ni kama vile mlikuwa mnakula na vipofu sasa mkajisahau mkawashika mikono!
 
Nadhani ni wajibu wao kufanya hivyo na kutusisitiza kwa kutumia njia na teknolojia zote zilizopo, ikiwamo Whatsapp, maana mioyo ya wengi wanadamu imeshikwa kutu ya dhambi sugu, na haiwezi kutoa bila kusukumwa kidogo sometimes.
 
Kimsingi inapaswa watu wakishatoa zile sadaka zao za kawaida za ibada kwa kila kila Jumapili makusanyo yanayopatikana yaendeshe shughuli za kanisa mbalimbali.

Lakini chakushangaza uwazi wa hizo sadaka hautolewi, halafu mbali na hizo sadaka bado michango chungu nzima hadi kuchosha!

Na kwa kule kutokuwa na uwazi ndiyo wengi huchukulia huenda ni nyingi sana Ndiyo maana hazitangazwi ili zisijestua watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…