Wadada muwe waaminifu mnapoazima fedha toka kwetu wanaume

Wadada muwe waaminifu mnapoazima fedha toka kwetu wanaume

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,128
Reaction score
21,885
Habari za wakati huu wakuu,

Kama kichwa kinavyojieleza, natoa rai kwa wadada (wanawake) wote kwamba mnapoazima fedha kwa marafiki zenu wa kiume, muwe waaminifu katika urejeshaji. Kuna dada mmoja ambaye ni colleague wangu kazini, majuzi mida ya saa tano usiku nikashangaa simu inaita kupokea ananisalimia nakuniambia kwamba ana shida moja kubwa sana anahitaji msaada wangu.

Kumuuliza nini tatizo, akaniambia mtoto wake kesho yake anacommence mitihani ila wameambiwa bila kuclear ada anayodaiwa hatoruhusiwa kufanya mitihani. Hivyo alikua anaomba nimuazime kiasi kadhaa cha fedha akalipe mtoto aruhusiwe kufanya mitihani na angenirudishia baada ya siku mbili. Bila hiyana nilimsaidia kwakua naelewa umuhimu wa mtoto kwenda shule na pia naelewa matatizo tumeumbiwa binadamu hivyo yatupasa kusaidiana pale tunapokua tuna uwezo wa kufanya hivyo.

Cha ajabu sasa, yule dada siku mbili zilipita nikaona kimya, zimepita siku takribani 5 sasa naona yuko kimya. Hakuna cha sms, wala hata simu angalau kusema kwamba ametingwa. Nikikutana nae kwa job anajitahidi kunikwepa sana, anakua hana amani anajichekesha chekesha mara azuge nitakuona baadae na mimi nimekaa kimya kwanza nione anavyoact.

Kikubwa, wadada muwe waaminifu, unajua shida hazina mwisho. Leo hii ukikosa uaminifu, siku nyingine utapata matatizo makubwa zaidi na utaona aibu kumfuata mtu ambaye angeweza kukusaidia kwa moyo mkunjufu lakini tayari umeshavunja uaminifu kwake.

Toleka!

1620217941735.png

 
Back
Top Bottom