Wadada, niulizeni kitu chochote kuhusiana na huduma za salon, hair & nails

images

Mwaaaa
 
nywele zangu ni nene na nzito
halafu ni ngumu kushika dawa,
niweke dawa gani ziwe zinashika haraka?....maana kila dawa ninayoweka naungua ngozi kabla hazijashika vizuri

Usiweke dawa hizi ni nywele asili za kiafrika wengine tunazipenda zikiwa natural. Wewe paka mafuta ya kawaida tu achana na huyo mzushi.
 
Mkuu nilinyoa sasa hivi bado hazijarefuka sana hivyo hazijakatika sana ndio nataka niziwahi mapema,mimi dawa niliacha kitambo nikiweka ndio zinapukutika kabisa (nywele zangu si nyingi sana ila ni nyepesi kavu halafu zimenyooka unaweza kudhani niliweka dawa ikadunda) Asante nitayatafuta mafuta.
Hapana natoa kwenye nywele zote? Kwani nywele zako zimekatika sana? na je hapo before umewahi kuweka nywele zako dawa?
GRO-76082-2.jpg

Hebu jaribu kutumia mafuta hayo hapo pichani…ni mazuri sana kwa natural hair.
 
Usiweke dawa hizi ni nywele asili za kiafrika wengine tunazipenda zikiwa natural. Wewe paka mafuta ya kawaida tu achana na huyo mzushi.

Mie napenda kuziwekea dawa
Nisipoweka hata kuchana siwezi
 
Dawa gani nzuri yakutolea nywele mwilini? Nywele zangu za mwilini hukua hara siku 14 tuu Kama sijatoa zinajaaa, na nimefanya Kwa sukari inaumaaaa .. Na inawekaa Baka Kama nimetafunwa.. Kuna dawa nzuri au saloon nzuri wanayo fanya vizuri...
 
Mie napenda kuziwekea dawa
Nisipoweka hata kuchana siwezi
Huna haja ya kuweka dawa kuna mafuta unaweza kupaka na kulainisha nywele ili iwe rahisi kuzichana. Hizi dawa zao mimi huwa siziamini kwani nimekuwa nikiwaona kina mama watu wazima waliokuwa mabingwa wa kuweka dawa wakinyonyoka nywele. Sipendi na wewe ikutokee.
 
thanks, mpenzi wangu rangi ya ngoz yake ni maji ya kunde na ina mafuta kidogo maana sometimes hutoka vchunusi vya hapa na pale, je atumie lotion gani ambayo haibadili uasili wa ngozi yake!?

Nimekuelewa mkuu, je hapo kabla amewahi kutumia mkorogo? (Kujichubua mwili?) nijibu then tuendelee kutokea hapo.
 
mwallu, kwanza niambie hapo kabla umewahi kuweka au kutumia dawa gani?...then nitajuwa nikushauri nini.

Mpendwa na mimi nisaidie nywele zangu ni laini na chache kiasi kwa sasa naweka movit ila kuna kipindi niliweka olive nywele haikuwa nzuri ndio nikahamia movit,hivi majuzi niliritachi ila aliyeniweka dawa akaweka mpaka juu! Vikawa vyepesi sana na sasa kila nikichana zinatoka sana! Huwa natumia steaming ya miadi na mafuta yake lkn sina hakika kama inanisaidia,naomba ushauri either nitumie dawa gani ya relaxer,steaming na mafuta ambavyo vitaendana vzr na nywele zangu laini na chache.Je nifanyeje ziache kupukutika ninapochana?nakereka sana
 
Last edited by a moderator:
Dawa gani nzuri yakutolea nywele mwilini? Nywele zangu za mwilini hukua hara siku 14 tuu Kama sijatoa zinajaaa, na nimefanya Kwa sukari inaumaaaa .. Na inawekaa Baka Kama nimetafunwa.. Kuna dawa nzuri au saloon nzuri wanayo fanya vizuri...

Kama sijakosea unaongelea skin waxing...kwa kawaida waxing ya kutengeneza kienyeji ambayo wanatumia asali,ndimu au sukari huwa inachagua ngozi ya mtu. Kuna mwingine inamkubari na kuna mwingine inamkataa. Ushauri wangu kwako jaribu kutumia ready made waxing za madukani na uhakikishe ziwe za kupasha na siyo zile za baridi.

Kuhusu Salon...jitahidi kwenda kwenye salon kubwa kubwa na siyo hizo salon ndogo ndogo. Akili yangu inanituma Salon kubwa kubwa huwa wamejipanga sana na wako makini sana kwenye upande wa skin care treatments.
 
Mpendwa na mimi nisaidie nywele zangu ni laini na chache kiasi kwa sasa naweka movit ila kuna kipindi niliweka olive nywele haikuwa nzuri ndio nikahamia movit,hivi majuzi niliritachi ila aliyeniweka dawa akaweka mpaka juu! Vikawa vyepesi sana na sasa kila nikichana zinatoka sana! Huwa natumia steaming ya miadi na mafuta yake lkn sina hakika kama inanisaidia,naomba ushauri either nitumie dawa gani ya relaxer,steaming na mafuta ambavyo vitaendana vzr na nywele zangu laini na chache.Je nifanyeje ziache kupukutika ninapochana?nakereka sana

Ooh pole sana mpenzi wangu! Noted...nitakujibu mda si mrefu
 
Mpendwa na mimi nisaidie nywele zangu ni laini na chache kiasi kwa sasa naweka movit ila kuna kipindi niliweka olive nywele haikuwa nzuri ndio nikahamia movit,hivi majuzi niliritachi ila aliyeniweka dawa akaweka mpaka juu! Vikawa vyepesi sana na sasa kila nikichana zinatoka sana! Huwa natumia steaming ya miadi na mafuta yake lkn sina hakika kama inanisaidia,naomba ushauri either nitumie dawa gani ya relaxer,steaming na mafuta ambavyo vitaendana vzr na nywele zangu laini na chache.Je nifanyeje ziache kupukutika ninapochana?nakereka sana
Prishaz, pole kwa matatizo ya nywele zako lakini usijari yatakwisha...ni mambo ya kawaida kwenye urembo wa nywele.
Ningekuomba ujaribu kutumia package hiyo hapo chini...am sure itakusaidia tu,ila make sure unaenda kuhudumiwa kwenye professional salon na siyo ilimradi salon. Hizo product utazipata S H Amon pale mjini.

Angalizo: usisuke misuko tata wala kushonea weaving kwa kipindi cha miezi mitatu...dili na hiyo treatment tu.
 
Last edited by a moderator:
image.jpg Prishaz...product ndiyo hizi hapa. Dawa,steaming na mafuta yake.
 
Last edited by a moderator:
Kama sijakosea unaongelea skin waxing...kwa kawaida waxing ya kutengeneza kienyeji ambayo wanatumia asali,ndimu au sukari huwa inachagua ngozi ya mtu. Kuna mwingine inamkubari na kuna mwingine inamkataa. Ushauri wangu kwako jaribu kutumia ready made waxing za madukani na uhakikishe ziwe za kupasha na siyo zile za baridi.

Kuhusu Salon...jitahidi kwenda kwenye salon kubwa kubwa na siyo hizo salon ndogo ndogo. Akili yangu inanituma Salon kubwa kubwa huwa wamejipanga sana na wako makini sana kwenye upande wa skin care treatments.

Asante, na pia nikitia hinaa kwenye mwili inaniwashaa wakati wa kuanza kukaukaa yani Kama nimetiwa pilipili ImageUploadedByJamiiForums1411209010.782022.jpg
 
Back
Top Bottom