Wadada, niulizeni kitu chochote kuhusiana na huduma za salon, hair & nails

Wadada, niulizeni kitu chochote kuhusiana na huduma za salon, hair & nails

mimi nimeweka culr ila nataka nihamie kwenye reluxer je dawa gani nzuri itakayofaa kutumia ili nywele zangu zisikatike.cult niliweka lazer curl
 
Wakuu.
Ninauhitaji wa midoli yenye nywele nyingi MAALUM kwaajili ya kujifunzia kusuka.
Nipo ktk harakati za kutimiza ndoto yangu ya kufungua shule ya kujifunza kusuka na urembo wa nywele kwa ujumla.

Ningependa kujua ni maduka gani naweza pata midoli hiyo na bei zake ikiwezekana

Natanguliza shukrani zangu.
 
Mbalu,pole kwa yote na nimekuelewa...ila kwa sasa nitashindwa kukujibu vizuri...maana niko nje ya TZ na niko busy sana. Na mara nyingi ninapowajibu watu huwa natumia PC au Ipad na hivyo vitu vyote hapa siko navyo. So siku nikirudi Bongo nitakupa jibu kiufasaha dada angu.

Kila lenye kheri lisikuponyoke huko uliko. Safiri salama.
 
Pole sana mpenzi…hongera kwa kufuga dread rocks.
Hizo zinakuwa ngumu kwa kuwa hauzi retouch na hauzifanyii hair treatment.
Ushauri wangu kwako jitahidi hata kwa mwezi mara mbili make sure unazipatia hiyo huduma na utafurahia mrejesho wake.

Na kuhusu oil face ningekushauri utafute salon mzuri na inayotowa huduma mzuri ya facial,waambie wakuonyeshe facial product zao kisha chagua kit ambayo itamaliza matatizo yako,patananao bei kisha wakufanyie.
Nitajuaje saluni nzuri?
Nimefanya trials nyingi sana. Nadhani hadi recomendation. Si jengo. Uniforms. Fake cofidence usoni kwwa staff au owner. Machupa na complicated treatment kwny displays. Au mnasemaje?
 
Mkuu MillionHairs nasikitika kuchelewa ingawa nami nitaambulia ukoko. nywele yangu ya asili ni nzito, nene na ni ngumu kama steel wire wasusi huwa nawahurumia kama sina dawa. Nilikuwa natumia dawa ya Revlon ya kopo, IC conditioner na mafuta ya organic, nywele yangu ilivutia kwa muonekano na ilikuwa imejaa na ndefu mpaka mabegani. kutokana na uzito ule nilishauriwa nibadili na kutumia Dark & lovely (beautiful begin), T - Tree condition Parnevu, na T - Tree oil najuta kwani nywele imekuwa nyepesi na inakatika sana. Naomba ushauri wako kwani mwanamke nywele aise.

Okay mbalu...am back

Kwanza pole kwa majanga yaliyotokea kwenye nywele zako maana ni kweli mwanamke ni nywele.
Lakini kabla sijafunguka...ningepeta kujuwa au kukuuliza je baada ya matatizo haya ulijaribu tena kurudia kwenye zile product zako zako za Revlon ya kopo na IC conditioner? Au ujarudia tena? Hebu tuanzie kwanza hapo kisha tuendelee
 
Last edited by a moderator:
Mie nywele zangu ni nyepesi halafu kila dawa nayotumua inaniunguza maana nilikuwa natumia beautiful begin ikanishindwa nikaja olive nayo majanga nikaambiwa nipake brow out hiyo ndo balaa naungua sana sasa hivi napaka easy weve nayo naungua sasa nitumie dawa gani?na nifanye steaming gani ili ziwe nzito?
 
mimi nimeweka culr ila nataka nihamie kwenye reluxer je dawa gani nzuri itakayofaa kutumia ili nywele zangu zisikatike.cult niliweka lazer curl

Kabla ya kuanza kuweka curl...je hapo mwanzo umewahi kuritouch? Kama ndiyo,je ni dawa gani?
 
Wakuu.
Ninauhitaji wa midoli yenye nywele nyingi MAALUM kwaajili ya kujifunzia kusuka.
Nipo ktk harakati za kutimiza ndoto yangu ya kufungua shule ya kujifunza kusuka na urembo wa nywele kwa ujumla.

Ningependa kujua ni maduka gani naweza pata midoli hiyo na bei zake ikiwezekana

Natanguliza shukrani zangu.

Hongera kwa hii ndoto uliyonayo na Mungu akuongoze kufikia malengo haya.

Maduka ya midoli yanapatikana mtaa wa Sikukuu na Mkunguni au maeneo ya mtaa wa Agrey na Sikukuu...kariakoo.
Ila bei zake sizijui.
 
Nitajuaje saluni nzuri?
Nimefanya trials nyingi sana. Nadhani hadi recomendation. Si jengo. Uniforms. Fake cofidence usoni kwwa staff au owner. Machupa na complicated treatment kwny displays. Au mnasemaje?

Kwanza nikiri kwamba jengo zuri,uniforms, na machupa mengi kwenye displays siyo ndio kuwa hiyo sehemu utapata treatment mzuri ya kumaliza matatizo yako...laa hasha. Ni kweli wanaweza kuwa na vitu vyote hivyo lakini wakashindwa kuwa na mtaalamu au wakawa hawana treatment unayoihitaji.

Lakini kabla sijaendelea nina swali moja...je umewahi kufanyiwa facial ya brand gani? Na je ulifanyiwa salon ipi?
Na je,walikupima face skin yako kabla ya huduma? tuanzie hapo kwenye maswali matatu haya kwanza.
 
Mie nywele zangu ni nyepesi halafu kila dawa nayotumua inaniunguza maana nilikuwa natumia beautiful begin ikanishindwa nikaja olive nayo majanga nikaambiwa nipake brow out hiyo ndo balaa naungua sana sasa hivi napaka easy weve nayo naungua sasa nitumie dawa gani?na nifanye steaming gani ili ziwe nzito?

Daah pole sana! Nahisi nywele yako iko sensitive sana...na pia nahisi inaweza kuwa imechangiwa na hatua yako au tabia yako ya kubadili badili dawa mara kwa mara.

Anyway ushauri wangu kwako: kwa sasa usiweke reluxer yoyote...iache nywele yako ikuwe na iwe natural kwa kipindi cha miezi 3 hadi 4. Ila unaweza zifanyia steaming. Nenda salon ambayo unaona Ina huduma mzuri waikaguwe hiyo nywele yako kisha waambie wakuchagulie steaming itakayoendana na nywele yako...ifanye kwa mwezi mara mbili
 
nashukuru kwa elimu unayopatia watu mimi natamani ku dread nywele zangu kwa sasa zina dawa pia sijui ni product gani za kutumia kama itawezekana ku zi dread kwa kifupi sijui nianzie wapi kutimiza azma yangu ya kuwa na dread
 
Kwanza nikiri kwamba jengo zuri,uniforms, na machupa mengi kwenye displays siyo ndio kuwa hiyo sehemu utapata treatment mzuri ya kumaliza matatizo yako...laa hasha. Ni kweli wanaweza kuwa na vitu vyote hivyo lakini wakashindwa kuwa na mtaalamu au wakawa hawana treatment unayoihitaji.

Lakini kabla sijaendelea nina swali moja...je umewahi kufanyiwa facial ya brand gani? Na je ulifanyiwa salon ipi?
Na je,walikupima face skin yako kabla ya huduma? tuanzie hapo kwenye maswali matatu haya kwanza.
Du! mie niliacha kufanya facials muda, baada ya kuona kila ninachosoma kuhusu ngozi na kushauriwa na wataalamu saluni wanachakachua kiidoooogo, kila napoenda, naona siridhiki. nanunua products =online nafaanya mwenyewe.
imani imepotea kwangu mimi binafsi.
kuhusu nywele nimeweka natural. mara chache huwa nashonea weaving, sina imani kabisa na saluni za bei mbaya au nzuri, vyeti ukutani au reception yenye kufanana na hoteli, wahudumu wa kimataifa au wa kitanzania, sio kwa TZ tu, hata nchi chache ambazo nimepita.
Ila ukinirudishia imani ntafurahi sana.
 
Kawaida unatakiwa ku retach nywele mara ngapi atleast kwa mwaka ? Maximum
 
Sayaka, mara nne au imezidi sana ni mara tano...inategemeana na texture ya nywele yako ikoje.
 
Okay mbalu...am back

Kwanza pole kwa majanga yaliyotokea kwenye nywele zako maana ni kweli mwanamke ni nywele.
Lakini kabla sijafunguka...ningepeta kujuwa au kukuuliza je baada ya matatizo haya ulijaribu tena kurudia kwenye zile product zako zako za Revlon ya kopo na IC conditioner? Au ujarudia tena? Hebu tuanzie kwanza hapo kisha tuendelee

Mkuu sirudia product za awali bali hizi za T - Tree na Dark & Lovely ni mwezi wa saba sasa naendelea nazo ingawa nywele yangu imekuwa nyembamba sana.
 
Uzi huu umenikumbusha vipindi vya mhubiri ask.Kakobe katika Tv na hasa kile cha "MAWIGI" katika somo:MAVAZI YA KIKAHABA.
 
Pole sana mpenzi!…sasa ni hivi,kuna kitu kinaitwa SPECIAL TREATMEN (ni steaming ya nywele.Huu ni mchanganyiko wa baadhi ya steaming kama makopo 7 na vitu vya asili kama bangi,mayai ya kienyeji nk. Pia kuna mafuta yake ya kupaka chini ya ngozi na juu nywele. Nikikuambia eti ukanunuwe vitu hivi na ujifanyie mwenyewe nitakuwa nakuongopea kwani is very very complecated jinsi ya kuvichanganya na kipimo cha wewe kujiweka kichwani…alafu kubwa zaidi kuna steamer zake maalum maalumu kwa treatment hii.

Kama uko Dar ningekushauli uende Million Hairs Salon iliyopo mikocheni kwa Mwl nyerere na uanze hiyo tiba
Au uende Sally salon iliyopo pale Benjamin mkapa tower... azikiwe street posta mpya. ila sina uhakika kama kweli na hapo wanafanya special treatment hiyo coz na mimi nilisikia tu. Ila Million Hairs Salon ni uhakika they do it.

Hiyo treatment unaifanya kipindi cha miezi mitatu bila kukosa…kwa mwezi unaifanya mara 2…so kwa miezi mitatu utaifanya mara 6. Kama kutakuwa na maelezo zaidi basi ukifika pale utapewa utaratibu wote…na hilo tatizo lako la nywele litakuwa historia.
Nashukuru kwa ushaur wakk.

Historia ya nywele zangu
Nywele zangu hazina dawa kwa sasa. Zilipokuwa fupi nilikuwa naweke wave ya sofn-free baadae zilivyokua za kushikika nikaacha wave nikawa nazisuka zenyewe. (mabutu ya rasta, weaving n.k ila mara nyingi mabutu) .
Nywele zangu ni kipilipili kilaini na chache sana. (Miez sita sasa toka nimeacha wave)

Shida niliyonayo.
1. Nywele zangu zimekatika sana mbele.
2.Je hii special tretment itanifaa kurudisha nywele zangu za mbele na kuzijaza ?
3. Nikivaa wig kuna wig cap huwa navaa, nilinunua kariakoo sh. 1000. Je itanisaidia ili lisinikate sehemu za mzunguko? -( Nimeamua nipumzike kusuka nina week ya pili nw navaa wig)
 
Back
Top Bottom