Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbalu,pole kwa yote na nimekuelewa...ila kwa sasa nitashindwa kukujibu vizuri...maana niko nje ya TZ na niko busy sana. Na mara nyingi ninapowajibu watu huwa natumia PC au Ipad na hivyo vitu vyote hapa siko navyo. So siku nikirudi Bongo nitakupa jibu kiufasaha dada angu.
Nitajuaje saluni nzuri?Pole sana mpenzi hongera kwa kufuga dread rocks.
Hizo zinakuwa ngumu kwa kuwa hauzi retouch na hauzifanyii hair treatment.
Ushauri wangu kwako jitahidi hata kwa mwezi mara mbili make sure unazipatia hiyo huduma na utafurahia mrejesho wake.
Na kuhusu oil face ningekushauri utafute salon mzuri na inayotowa huduma mzuri ya facial,waambie wakuonyeshe facial product zao kisha chagua kit ambayo itamaliza matatizo yako,patananao bei kisha wakufanyie.
Mkuu MillionHairs nasikitika kuchelewa ingawa nami nitaambulia ukoko. nywele yangu ya asili ni nzito, nene na ni ngumu kama steel wire wasusi huwa nawahurumia kama sina dawa. Nilikuwa natumia dawa ya Revlon ya kopo, IC conditioner na mafuta ya organic, nywele yangu ilivutia kwa muonekano na ilikuwa imejaa na ndefu mpaka mabegani. kutokana na uzito ule nilishauriwa nibadili na kutumia Dark & lovely (beautiful begin), T - Tree condition Parnevu, na T - Tree oil najuta kwani nywele imekuwa nyepesi na inakatika sana. Naomba ushauri wako kwani mwanamke nywele aise.
mimi nimeweka culr ila nataka nihamie kwenye reluxer je dawa gani nzuri itakayofaa kutumia ili nywele zangu zisikatike.cult niliweka lazer curl
Wakuu.
Ninauhitaji wa midoli yenye nywele nyingi MAALUM kwaajili ya kujifunzia kusuka.
Nipo ktk harakati za kutimiza ndoto yangu ya kufungua shule ya kujifunza kusuka na urembo wa nywele kwa ujumla.
Ningependa kujua ni maduka gani naweza pata midoli hiyo na bei zake ikiwezekana
Natanguliza shukrani zangu.
Nitajuaje saluni nzuri?
Nimefanya trials nyingi sana. Nadhani hadi recomendation. Si jengo. Uniforms. Fake cofidence usoni kwwa staff au owner. Machupa na complicated treatment kwny displays. Au mnasemaje?
Mie nywele zangu ni nyepesi halafu kila dawa nayotumua inaniunguza maana nilikuwa natumia beautiful begin ikanishindwa nikaja olive nayo majanga nikaambiwa nipake brow out hiyo ndo balaa naungua sana sasa hivi napaka easy weve nayo naungua sasa nitumie dawa gani?na nifanye steaming gani ili ziwe nzito?
Du! mie niliacha kufanya facials muda, baada ya kuona kila ninachosoma kuhusu ngozi na kushauriwa na wataalamu saluni wanachakachua kiidoooogo, kila napoenda, naona siridhiki. nanunua products =online nafaanya mwenyewe.Kwanza nikiri kwamba jengo zuri,uniforms, na machupa mengi kwenye displays siyo ndio kuwa hiyo sehemu utapata treatment mzuri ya kumaliza matatizo yako...laa hasha. Ni kweli wanaweza kuwa na vitu vyote hivyo lakini wakashindwa kuwa na mtaalamu au wakawa hawana treatment unayoihitaji.
Lakini kabla sijaendelea nina swali moja...je umewahi kufanyiwa facial ya brand gani? Na je ulifanyiwa salon ipi?
Na je,walikupima face skin yako kabla ya huduma? tuanzie hapo kwenye maswali matatu haya kwanza.
Okay mbalu...am back
Kwanza pole kwa majanga yaliyotokea kwenye nywele zako maana ni kweli mwanamke ni nywele.
Lakini kabla sijafunguka...ningepeta kujuwa au kukuuliza je baada ya matatizo haya ulijaribu tena kurudia kwenye zile product zako zako za Revlon ya kopo na IC conditioner? Au ujarudia tena? Hebu tuanzie kwanza hapo kisha tuendelee
Nashukuru kwa ushaur wakk.Pole sana mpenzi! sasa ni hivi,kuna kitu kinaitwa SPECIAL TREATMEN (ni steaming ya nywele.Huu ni mchanganyiko wa baadhi ya steaming kama makopo 7 na vitu vya asili kama bangi,mayai ya kienyeji nk. Pia kuna mafuta yake ya kupaka chini ya ngozi na juu nywele. Nikikuambia eti ukanunuwe vitu hivi na ujifanyie mwenyewe nitakuwa nakuongopea kwani is very very complecated jinsi ya kuvichanganya na kipimo cha wewe kujiweka kichwani alafu kubwa zaidi kuna steamer zake maalum maalumu kwa treatment hii.
Kama uko Dar ningekushauli uende Million Hairs Salon iliyopo mikocheni kwa Mwl nyerere na uanze hiyo tiba
Au uende Sally salon iliyopo pale Benjamin mkapa tower... azikiwe street posta mpya. ila sina uhakika kama kweli na hapo wanafanya special treatment hiyo coz na mimi nilisikia tu. Ila Million Hairs Salon ni uhakika they do it.
Hiyo treatment unaifanya kipindi cha miezi mitatu bila kukosa kwa mwezi unaifanya mara 2 so kwa miezi mitatu utaifanya mara 6. Kama kutakuwa na maelezo zaidi basi ukifika pale utapewa utaratibu wote na hilo tatizo lako la nywele litakuwa historia.