Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

Karibu sana. Nakumbuka those days 2002 nilikuwa na kademu pale CBE kakaniomba nikanunulie Motorola ilikuwa maarufu sana kwa jina la T.I.D, nikakaambia sawa. Nakuletea zawadi utakayoweza kununua T.I.D mbili, demu mawazo yake yakamruka, enzi hizo cheni za gold ndio habari ya mjini, basi akajua atapata moja.

Nikamwambia jumamosi asubuhi nakuletea zawadi nikija kunywa supu CBE Club. Ile naingia tu namuona bibie yuleeee, amewaka mwenyewe.

Basi akanipokea kwa lundo la mabusu, hata supu anainywa hainyweki. Basi nilipo maliza kula nikamwambia zawadi yako iko kwenye gari.

Tukaenda kwenye gari Toyota Hilux 12R, model 1982. Ile tumefika tu kwenye gari anaona magunia matano ya mchele, nikamwambia hii ni zawadi yako.


Msichana akaipokea kwa shingo upande sana, basi nikatafuta vijana, wakaushusha ule mchele, wakaupeleka Serengeti chumbani kwa binti.

Nikampa na mzani na mifuko, nikawa namtafutia wateja maofisini binti anafanya delivery, alitengeneza sana hela.

Mwanzoni hakuyasoma mawazo yangu
Dahh! Everyday unani-inspire brotha... kwa mwanamke mwenye akili angejua ndo mwanzo wa kufanikiwa kwake financially na angejua kapata mwanaume makini...

vipi ndo wife huyo saiv au ndo aliishia kuwa sikio la kufa? 🤔
 
Jana wana JF kadhaa wenye club yetu fulani hivi amazing tulikuwa tumekutana The Wine Coutry kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2023.

Wanawake tulikuwa wawili tu, mimi na bidada mwingine na wanaume idadi yao ilikuwa kumi na kitu.

Jamani miongoni mwa mambo ambayo wanaume wanayaona ni kero ni swala la kupiga mizinga.

Wanawake tena mmetajwa kwa majina ambao mnashinda inbox mki zingalaizi. Mara mama anaumwa, mara dada kagongwa na bodaboda, mara nitumie hela ya kusuka nywele mara sina ada ya watoto.

Jamani kwa kweli mnahoyafanya huko PM aibu nimeona mimi. Ukitongozwa ndio usiseme. Hata kama una kazi ya ajira, tena mwajiriwa wa serikali, unaomba kuanzia vocha hadi hela ya chupi.

Wewe uko Dodoma mwanaume yuko Dar hajawahi hata kukulala zaidi ya kuonana mara moja na tena ulikuwa kwenye siku zako.

Nimekutaja wewe dada wa Dodoma sababu umekuwa na tabia ya kuwatongoza wanaume na baadae unaanza kuwa kero kwao na mizinga unayowapiga.

Jamani nawakaribisha Lindi tulime ufuta mbona kilimo poa tu, unapata hela ya kukukimu na huadhiriki.

2023 tubadilikeni jamani
Mdada aliyepo Dodoma anitafute 😎😎😎😎
 
Jipost kwangu
Imeisha hiyo…
6049D0D4-0E0B-42DE-BA8C-7274781496E0.jpeg
 
Kuna siku nilikutana nae kwenye msiba wa mke wa rafiki yangu, walisoma wote pia CBE. Alikuwa amejichubua hadi kawa mwekundu machoni.

Alikuwa kashika chupa ya K Vant mkononi, anaonekana she's living to the fullest. Yaani analewa kadiri atakavyo, na atakuwa anatumika sana.

Nilimsahau, nikasikia mtu ananiongelesha kwa sauti ninayoifahamu, ilinichukua sekunde kadhaa kuvuta picha yake ya zamani na hii ya sasa. Akani hug, akawa ananitambulisha kwa wenzie, aibu naona mimi. Huyu alikuwa mume wangu, kanitompa wee akaniacha eti kisa nimemwita mama yake mchawi.
Hebu fikiria maneno hayo anaongea kwa makelele mbele ya watu msibani
Ahh! Hakuwa na akili na bila shaka yuko frustrated sasa... si ajabu na ngoma anayo maana CBE na IFM miaka ile ilikuwa moto ingawa wake wema walikuwepo na wapo waliobahatika kuoa na kuolewa na wapo salama kwenye ndoa zao mpaka hivi leo.

Ila hatua ya mwanamke kumuita mzazi/wazazi wako wachawi aisee huyo ni penalty tu na redcard juu moja kwa moja
 
Ahh! Hakuwa na akili na bila shaka yuko frustrated sasa... si ajabu na ngoma anayo maana CBE na IFM miaka ile ilikuwa moto ingawa wake wema walikuwepo na wapo waliobahatika kuoa na kuolewa na wapo salama kwenye ndoa zao mpaka hivi leo.

Ila hatua ya mwanamke kumuita mzazi/wazazi wako wachawi aisee huyo ni penalty tu na redcard juu moja kwa moja
Penalty, redcard, na kifungo juu
 
Kila mtu na namna yake ya utafutaji wew unalima ufuta wengine wanalimia mifukoni kwa watu ndio maisha.

Sion haja ya wew kupata tabu. Na hao wanaoombwa kama hamtaki si unamwambia tu mtu mie sitaki kuombwa hela mnaishia hapo. Sio kwenda kulalamika huko kwenye wine nin sijui.
 
Back
Top Bottom