Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

Kuna mambo yanasikitisha sana....
Nasoma comments...
 
Jana wana JF kadhaa wenye club yetu fulani hivi amazing tulikuwa tumekutana The Wine Coutry kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2023.

Wanawake tulikuwa wawili tu, mimi na bidada mwingine na wanaume idadi yao ilikuwa kumi na kitu.

Jamani miongoni mwa mambo ambayo wanaume wanayaona ni kero ni swala la kupiga mizinga.

Wanawake tena mmetajwa kwa majina ambao mnashinda inbox mki zingalaizi. Mara mama anaumwa, mara dada kagongwa na bodaboda, mara nitumie hela ya kusuka nywele mara sina ada ya watoto.

Jamani kwa kweli mnahoyafanya huko PM aibu nimeona mimi. Ukitongozwa ndio usiseme. Hata kama una kazi ya ajira, tena mwajiriwa wa serikali, unaomba kuanzia vocha hadi hela ya chupi.

Wewe uko Dodoma mwanaume yuko Dar hajawahi hata kukulala zaidi ya kuonana mara moja na tena ulikuwa kwenye siku zako.

Nimekutaja wewe dada wa Dodoma sababu umekuwa na tabia ya kuwatongoza wanaume na baadae unaanza kuwa kero kwao na mizinga unayowapiga.

Jamani nawakaribisha Lindi tulime ufuta mbona kilimo poa tu, unapata hela ya kukukimu na huadhiriki.

2023 tubadilikeni jamani
Kuna mdada nilikuwa namheshimu sana mpaka nikaanzisha mahusiano baada ya kumuona kama anajielewa...
Kiruuu mizinga anayopiga sasa duuhh mara mtoto wake hana uniform,mara anataka amtahiri mwanae nk..
Cha ajabu alivyoanza mahusiano na mimi akaamua kutumia family plan ili asizae miaka mitano...sasa mtu hataki kuzaa namimi lkn pesa anaitaka wa nini huyo [emoji23][emoji23]
 
Kuna muda unakutana na mdada mnajenga urafiki kabisa nakuwa naona huyu kwenye kazi zangu atanifaa ngoja niweke mambo Sawa kisha nitakaa nae mezani tuyajenge daaahh kabla hata ya kufka point kuomba pesa kusiko na mpangilio kutaanza daaah kifupi Mnakatisha tamaa wadada na mnatuogopesha sana sisi wazee wa mishe.
Upendo huvumilia yote, upendo hauhesabu mabaya
 
nitakufata kule unitumie kapicha nisaminishe🤣🤣wala Sina makasiriko niko cool
Bado tu unahangaika?😂

Hakikisha unapoomba picha za warembo unatag zulu man ili nikutumie kama wakikataa
 
Back
Top Bottom