Hii post nimeitoa jukwaa la biashara na Uchumi.
BIASHARA 5 UNAZOWEZA KUFANYA BILA MTAJI WA PESA HIZI HAPA;
1. AFFILIATED MARKETING (BIASHARA YA USHIRIKA)
Hii inahitaji mdomo na kili yako tu.
Inafanyikaje?
(a) Unachotakiwa kufanya ni kujua bidhaa zenye mahitaji makubwa kwenye sehemu ulipo,hata kitaifa kwa ujumla.
(b) List bidhaa hizo pamoja na bei zake za mauzo mitaani na mitandaoni.
Mfano; Viatu vya kike labda.
(c) Tembelea maduka ya masupply wakubwa wa bidhaa hizo,jitambulishe kama agent kwa kusupply bidhaa kutoka madukani kwenda mitaani na WAOMBE NAFASI YA KUWA MMOJA YA WASAMBAZAJI WAO.
Na kazi yako kubwa ni kuunganisha wauzaji na watumiaji huku ukipata malipo kwa kinachoongezeka kutoka bei ya jumla kwenda rejareja.
(d)Chukua mawasiliano ya kila supplier , picha za bidhaa zake ,bei za bidhaa na makubaliano ya kukujulisha kila mzigo mpya unapofika.
Mfano kwa maeneo ya Dar es Salaam unatembelea maduka makubwa ya viatu vya kike karikoo.
(e)•Tengeneza account za biashara mitandaoni & Jiunge kwenye magroup mengi kisha anza kutafuta wateja .
NB;Hakikisha uantumia jina la kuvutia wateja usitumie jina lako halisi mfano unaweza kujiita VIATU POA.
•Tembelea wanunuzi wa rejareja waeleze kuhusu bidhaa zenu (Kwani kwa sasa wewe ni sehemu ya maduka yao,usijitambulishe kama mtu binafsi) NB:Tumia identity ya ofisi kuongeza uaminifu.
(f)Unapopata mteja mdirect dukani kwa bei ya rejareja,Utapata commission yako kwa kila mteja bila kutumia hata senti 5.
(g)Muda unavyozidi kwenda utapata uaminifu kwa wenye maduka,utaweza kuchukua bidhaa kwa "Mali Kauli" na kurejesha pesa madukani.
(h)Ukiwa na akili utasave pesa nyingi sana utakazotumia kama mtaji baadae.
Amini nakwambia mjini watu wengi wameanza na kuendeleza maisha kwa mfumo huu.
2. EVENTS PLANNING
Hii haina utofauti mkubwa sana na biashara ya ushirika,Na inakuwa rahisi kama ukipata watu wa karibu mkatengeneza team.
Inafanyikaje?
•Tembelea kila ukumbi wa sherehe na uchukue mawasiliano ya wamiliki na mameneja na bei zao.
•Tafuta list ya watu wanaohusika na mapishi katika masherehe 'Catering Service' na uchukue mawasiliano na bei zao.
•Chukua list ya kampuni zinazohusika na ukodishaji wa magari na uchukue mawasiliano na bei zao.
•Chukua list ya MC wote mitandaoni na uhifadhi mawasiliano yao.
•Chukua list ya wapambaji wa sherehe wote mitandaoni na uhifadhi mawasiliano na bei zao.
ANZA MATANGAZO KAMA MNAHUSIKA NA KUANDAA EVENTS KWA MALIPO YA 30% KABLA YA TUKIO.
Events yenu ya kwanza ndio itakuwa malango wa events na mtaji wa zote zitakazofata.
3. BIASHARA YA MAJANI YA MIFUGO NA VYAKULA VYA MFUGO.
Kwa wanaoishi maeneo ya Dar es Salaam hasa mitaa ya mawasiliano wanaelewa thamani ya hii biashara.
Vijana wengi wa maeneo yale wamekuwa wakitumia fursa wa uhaba ya malisho kwenye jiji ,kwa kukata majani na kulundika pembezoni mwa barabara.
Nilipata bahati ya kuonge ana mmoja ya vijana wale ambapo alinieleza thamani ya majani kwa gari moja ni mpaka 30K na wao wamekuwa wakiuza mpaka gari 5=150000 per day kwa watu 3 kwa siku,MTAJI UKIWA NI UBUNIFU,NGUVU ZAO NA VISU NA MAFYEKEO KUTOKA MAJUMBANI MWAO.
Wengine wamekuwa wakisupply vyakula kwa wamiliki wa nguruwe kwa kukusanya mabaki ya vyakula kwa kila mama ntilie maeneo yale na wamekuwa wakiuza mapaka kwa 5K kwa ndoo moja na wanauwezo wa kukusanya ndoo mpaka 10 kwa siku.
Hii kazi kwa masharobaro inakuwa ngumu ila amini hapa unaweza kupata mtaji wa maisha
NIMEJITOLEA KUKOMBOA FIKRA ZA VIJANA WENZANGU.
BIASHARA NAMBA 4 NA 5 NITAWEKA KULINGANA NA RETWEET NA MAWAZO YENU JUU YA HIZO.
Kwa nondo na part 2 nyingine kama hizi ntaweka part 2 baadae.
Madarasa mengine kama haya kama #buku10challenge yanapatikana tweeter Luqman mohamedy