Wadada wa siku hizi sielewi wanawezaje kuendesha biashara zao ndogo kwenye fremu za gharama kubwa

Wadada wa siku hizi sielewi wanawezaje kuendesha biashara zao ndogo kwenye fremu za gharama kubwa

Nawaza hivyo pia ama kuna watu wanawaweka mjini ,,,, ! Haiingii akilini frem mtu alipe 2.m au 1.5m tena mwaka akauze pochi 10, vichupi kadhaa na bra ! Haimlipi hata kidogo
Umewaza katika angle ya mabaya sometimes watu hawana biashara moja tu kuna watu wamewekeza katika kilimo au real estate mikoani na wanapata pesa nyingi tu kwa kumtazama unaweza kufikiria kuwa anapata pesa kupitia kuuza poda ama K na duka ni kiini macho
 
Jmosi iliyopita nilikuwa ARUSHA na NDUGU Yangu ametoka nje...akaantoa nje shika 200"000 we tutumie br. Nkaweka 40 kushoto kwanza

wakaja madada wazuri wastaarabu akawapa ofa zikazungushwa fly. ...na savanna ...mmmh nilipoona awalewi nkastop kunywa pombe nkahisi awachrlewi kutupiga.

Moja akanifwata kiustaarabu nimependa upendo wenu naonba namba yako nkampa


asbh nkakutana na msg .mmefika salama...NDIO.... Can I tell u something mmmh nkazima kwa mda nkataman ntoe na betri

baadae straight akaandika kaka na biashara Yangu naonba msaada WA capital ........

nkamjibu sorry si tunapita TU Wala atuna uwezo WA kumpa mtu mtaji

kama kula kunywa MPAKA tuondoke ok

ajajibu MPAKA tumeondoka......

so imagine anakutana na famba anampa hela anakula mzigo mwezi mzima

Hawa sio mbona
Hahahahaha….hatari Mkuu…ungeacha mtaji hapo..
 
Kuna jengo kubwa sana jipya pale sinza mall mkono wa kulia kama unaelekea mwenge biashara za pale uwa sielewi watu wanapataje faida make niliwai kushinda pale week mfullizo huoni wateja wakija kuchukua bidhaaa ghorofa ya pili na ya tatu ila watu daily wapo
Au labda ni majini , ninyi mnaona ni watu kumbe ni vibwengo flani wanahudumia ulimwengu usionekana kwa macho ya kawaida
Hii kwa Dar hata mimi nimeshuhudia sana na nikakosa majibu kabisa
😂😂😂😂
 
Unakuta,

Mdada kakodi fremu kodi 1m, kaweka vigauni na madela, ukipiga hesabu yake vigauni kama 7, na Madela 15 jumla haifiki mtaji wa 1M anashinda hapo kila siku.

Mashoga zake wanamtembelea hapo ni mwendo wa kuagiza misosi na vinywaji ki pub cha jiran, nje kapaki IST yake safi kabisa, jioni huyo anaenda kwake, unakuta biashara ngumu lakini anakomaa hivyo hivyo, kuna nini nyuma ya pazia? Au ndo masponsa?

Unakuta mdada kakodi fremu kaweka vyupi pc kadhaa, bra pc kadhaa na pochi kama 10 tu kamaliza. Anashinda hapo biashara hamna na ukimuona mdada mwenyewe high class. Ama kweli dunia ina mambo!

Unakuta mdada kafungua saloon, anashinda ti huko na mashoga zake lakini hakuna kinachofanyika humo ndani na still life going on.

Hasa maeneo haya ya mijini unakuta mdada kafungua let's say bakery, hamna movement zozote lakn kila siku yumo, na kodi ikiisha italipwa ya mwaka. Kuna nini behind?

Kuna mahali nina kiofisi mjini mjini hivi, Jirani yangu ni mdada wa makamo 40's ni zile types za wadada ambao hawazeeki, full kupendeza, sunglasses n.k. Tuwaite mishangazi.

Ni jirani nikimaanisha fremu zetu zimefatana. Kachukua frem mbili kavunja kati ikawa moja kubwa, kaweka mini supermarket nzuri ya kisasa mzigo wa kutosha, kafunga Ac, milango aluminium, pana muonekano mzuri. Hana mfanyakazi anauza yeye mwenyewe, pia ana harrier hizi wanaziita matako ya nyani, hamna biashara kabisa. Kwa siku ameuza sana haizidi laki moja, nadhani watu wanapaogopa kulingana na muonekano wanahisi vitu ni bei Sana.

Mashoga zake wanakuja ni kujiagizia pombe tu na vyakula, akijisikia hata saa 8 mchana anafunga anaondoka, weekend anafunga muda wowote ule.

Mifano ni mingi iliyo hai, wanawake na hizi biashara ni kama geresha, au ni pakuzugia tu wana migodi yao wanayochimba pesa (mabwana ).
Weee hujui? Zaidi ya biashara, Yeye ana tobo na tigo! Wewe una nini?
 
Madanga zao ndio watanunua
Sidhani kama ni Madanga tu au madawa ya kulevya ,kuna kitu cha siri cha ziada kinafanyika kwenye hivyo vifremu
Madawa yenyewe wabongo wangapi wanapesa ya kuhimili addiction ya madawa narcotics na yalivyo expensive ,?
Madanga wangapi wana pesa ya kuhonga na kuwafanya watu wawe na life style kama hiyo Tz hapa ?
Jibu ni no
 
Kuna mwanangu mmoja amesomea Computer science sasa anafanya kazi online akiwa home. Ila kaajiriwa 🇺🇸 sasa wana mtaani wanamsema kuwa muuza ngada sijui anafuga majini waswahili akili zao kama tumbili wakiwa maskini.

Mwanangu anaingiza $75,000 kwa mwaka sasa unataka akae kijiweni na watu wasio na njia ya maisha.

Hao wenye maduka wasio na bidhaa wengi wao wahindi sababu anakimbia kodi kubwa. TRĄ wakiona mzigo umejaa dukani kodi yako lazima iwepo juu.

Ishi mjini kwa akili kubwa usiishi mjini ukajifanya wewe babkubwa.
 
MIMI JAPO KUWA NA NAKAZI ZANGU ILA NA ROBOT LA FOREX AMBALO MDA WOTE LIPO SOKONI KWA MWEZI KUNIPA USD 750 MPAKA 350 NI KAWAIDA.SASA WENZANGU WANASHANGAA HUYU JAMAA PESA ZA POMBE NA SAFARI ANATOA WAPI.

DUNIA INAMAMBO MENGI
 
Ukweli unauma ila unaponya. Hapa ilitakiwa "IRS" ya bongo ihusike kufuatilia hizi mambo, lakini wadau hususan wahusika wanaona ni kama kufuatiliana hivi😀😀😀

Wadau wengine wametaja money laundering, ila mi najua kuna biashara kongwe inaendelea ndani ya hizo biashara.

Kuna kamanzi tunapiga nacho mishe, kalinionyesha chats zake na rafiki yake wa kike mmoja wa wamiliki wa hizo fremu, nikasema duuuh!!!!

Hatusemi wote wanafanya money laundering au biashara kongwe, ila wapo wanaozugia hizo fremu hapa town.
 
Back
Top Bottom