Wadau Huyu Fei Toto Mnamuonaje??

Wadau Huyu Fei Toto Mnamuonaje??

Hili suala la Feisal ni bora kuliko Mkude leo limenifanya nimekesha, nikimuangalia kwa umakini huyu Dogo.

Nilichogundua.. Fei Toto anahitaji kukaa na Mkude katika timu moja kwa misimu zaidi ya mitatu ili ajifunze.

Watani zangu Hajar Sibonike kyata Frank Wanjiru Vyamavingi Guasa Amboni Ulimakafu n.k tupeni Feisal tumpike, then akiiva tunawarudishia.
Fei yupo timu pekee inayoweza kuendeleza kipaji chake. Kama anataka misumari aende Simba.
Bahati nzuri hilo kaliona.
 
Mkuu Fei toto ni mzuri ndiyo ila huwezi mbeza mkude maana anauwezo pia anaeperience kumzidi toto mimi nadhani ukitoa ushabiki basi Fri toto na mkude wanaweza tengeneza combination kali stars
 
Fei yupo timu pekee inayoweza kuendeleza kipaji chake. Kama anataka misumari aende Simba.
Bahati nzuri hilo kaliona.
Kama mlivuokuza cha Mwashiuya na Mkomola.. Au sasa mnavyokuza cha golikipa wetu wa Serengeti Boys.
Mwambie Fei atumie akili.Mwache Mkude atumie nguvu.
Hahahahaha
 
taifa stars kwa sasa inahitaji vijana wengi kama ilivyo timu moja hapa nchini sijui wanaiita yanga ingawa mi sio mshabiki wa matimu yenu.huyu dogo fiesal ni kipaji kizuri ila asibwetek
 
Mkuu Fei toto ni mzuri ndiyo ila huwezi mbeza mkude maana anauwezo pia anaeperience kumzidi toto mimi nadhani ukitoa ushabiki basi Fri toto na mkude wanaweza tengeneza combination kali stars
Nimebaini kwamba wengi waliojadili swala hili wametumia ushabiki zaidi kuliko hoja madhubuti. Hata chanzo cha uzi wenyewe kimeegemea kwenye ushabiki. Ubora wa kiungo haupimwi kwa uwezo wa kiungo mwengine, bali kwa jinsi anavyotimiza sifa zote za kuwa kiungo. Hakuna yeyote kati ya wachangiaji aliyeonyesha ukamilifu wa yeyote kati ya viungo hao, wala udhaifu wake. Mathalani, kusema udhaifu wa Fei ni utoto, kwa vipi? Anaramba pipi kiwanjani? Au anaposema udhaifu wake ni Uzanzibari, kivipi? Cannavaro ni Mzanzibari, ni udhaifu gani alikuwa nao kutokana na Uzanzibari wake ambao pia tunauona kwa Fei? Kuonekana hayuko serious ndiyo mtindo wa uchezaji wake unaomtofautisha na wengine. Aangaliwe Roberto Carlos alivyokuwa akicheza nafasi ya beki kisha afananishwe na Marcelo. Huyu Marcelo ataonekana hayuko seriois, lakini ndio mtindo wake, huwezi kuuita kuwa ndio udhaifu. Aidha, wanaodai kwamba Fei ni laini kwa hivyo hataweza mechi ngumu waangalie mbali zaidi. Mathalan, mashindano ya Chalenji ya mwaka jana haya kuwa magumu? Mbona alibaki kuwa Robo ya kiungo cha timu yake, mpaka timu za Ligi Kuu Bara zikaanza kummezea mate? Matumizi ya akili kuliko nguvu ni hitaji muhimu kwa timu yoyote, kama ilivyo kwa matumizi ya kasi, uwezo wa kumiliki mipira, uchezaji mipira ya juu, n.k. Si lazima sifa hizo zote zimilikiwe na mchezaji mmoja, muhimu ni kuwa na muunganiko wa sifa hizo ndani ya timu nzima. Kadhalika kusema umri mkubwa ndio udhaifu wa Mkude ni ushabiki usioleta tija kwenye hoja yenyewe. Anayesema hivyo afafanue kwanza wapi uzoefu na umri vinakataana. Maana umri wa Mkude sidhani kama unazidi wa Christiano Ronaldo au Messi, na hadi sasa hawajakataliwa na Timu zao za Taifa kwa sababu ya umri. Jambo jengine ambalo mashabiki waliochangia mada hii wanapaswa kujua ni kwamba uoni wao kama washabiki si lazima uwe ndio uhalisia wa kitaalamu, ingawa hata hao wataalamu nao wanatofautiana mawazo kulingana na mfumo na falsafa wanazopendelea kutumia.
Yote kwa yote, wanaombeza Mkude mbele ya Fei wanapaswa kusibiri mpaka Fei awe ametimiza muda kama wa Mkude kwenye kandanda ya ushindani ndiyo waweze kutoa tathmini zao. Na wanaombeza Fei kwa sababu ndio kwanza anachipukia waelewe kwamba kitendo cha wao kutumia nguvu kubwa kumtetea Mkude kinaashiria jinsi uwezo wa Fei ulivyo mkubwa.
 
Ni wa kawaida sana tena mpira wake ni wa mchangani, anahitaji more experience.Usipnde sana kusikiliza mawaidha ya mashabiki wa kibongo kwani wengi wao ni mabumbumbu wa mpira na hawana upeoo wa kujuwa uzuri wa mchezaji, wengi wao wanaiga tu kusifia wachezaji. Mtu akisema Ngassa ni mchezaji mzuri basi kila mtu atasema hivyo hivyo wakati si ukweli.
 
Sasa mbona hawa ni nafasi mbili tofauti??
Mkude ni holding midfielder...
Fei toto ni attacking midfield...
 
Usilinganishe mwanga na Giza. Si makosa yako unaongozwa na hisia
Ushaambiwa Jumapili mtakapocheza chukua peni na karatasi halafu nakili pass anazopiga Mkude kwenda mbele na nyuma zipi ni nyingi.
 
Kw hizo mechi ulizo mtaja uwez kumuona Fei toto.....

Fei toto ni fundi haswa ila koch Zahera anakosea kumchezesha namba 6 Fei n mzuri akiwa Namber nane toka akiwa Jku, na hata Zanzibar Herrors, ndo maaba ata juzi aliitumia vyema nafasi yake.....

Anaujua, anakamilisha majukumu yake ila cha zaid ana ladha na si utoto kitu ambacho wengi wanataman ila uwezo awana.
 
Back
Top Bottom