Wadau Huyu Fei Toto Mnamuonaje??

Wadau Huyu Fei Toto Mnamuonaje??

Fei atakuja kuwa middle mkubwa na mwenye uwezo kama hatalewa visifa vidogo hv.. sio kwamba amekuwa na uwezo wa kuaminiwa sana kuzidi MKUDE... haya ni matusi.
Alicheza vzr Kiungo?Sikumfuatilia mtu mmoja mmoja nilikuwa nafuatilia timu nzima.Ila pale katikati kipindi cha pili vijana wa stars walipadhibiti na zile touch kama Barca.
 
Mkude kalifanyia nini hili Taifa??? na Simba kacheza miaka 7 ubingwa Mara mbili..ujue anazidiwa medali na Makapu...
Kwa hiyo Makapu ni muhimu kuwapo Stars kuliko Samata, kwa kuwa Genk haijawahi kuchukua ubingwa wa Belgium?
 
Huyu kijana alipoingia, alileta uhai Katika timu ya Taifa, tulishinda lakini timu Yetu walicheza kama wameokotana
 
Fei Toto ni mchezaji mzuri lakini hawezi Kuwa mzuri zaidi ya Mkude.
Mkude ana uzuri gani? Sema ni mzuri akiwa huko kwenu simba! Ni wakawaida sana! Feisal ndio kwanza anaanza kudhihirisha uwezo wake, baada ya miaka 2 atakuwa mbele huko! Huyo Mkude kila akifanya majaribio anafeli.... Ndio mjue wakawaida.
 
Hili suala la Feisal ni bora kuliko Mkude leo limenifanya nimekesha, nikimuangalia kwa umakini huyu Dogo.

Nilichogundua.. Fei Toto anahitaji kukaa na Mkude katika timu moja kwa misimu zaidi ya mitatu ili ajifunze.

Watani zangu Hajar Sibonike kyata Frank Wanjiru Vyamavingi Guasa Amboni Ulimakafu n.k tupeni Feisal tumpike, then akiiva tunawarudishia.
Tuachie mchezaji wetu tatizo ninaloona kwake ni kucheza kwa nguvu matokeo yake anatengeneza kadi na faulo nyingi. Tumpe muda kwani kuanza kumfananisha na mkude sio haki kwa muda huu faisal pana mengi ya kufanya mpaka awe amekwivya. Nikimkumbuka humud huwa nasikitika sana.
 
Kwa hiyo Makapu ni muhimu kuwapo Stars kuliko Samata, kwa kuwa Genk haijawahi kuchukua ubingwa wa Belgium?
Belgium unaongelea dunia ya kwanza...Mechi ya jumapili na Stand chukua pen na karatasi hesabu pass za pembeni na nyuma anazopiga Mkude ni nyingi kuliko za mbele...
 
Tuachie mchezaji wetu tatizo ninaloona kwake ni kucheza kwa nguvu matokeo yake anatengeneza kadi na faulo nyingi. Tumpe muda kwani kuanza kumfananisha na mkude sio haki kwa muda huu faisal pana mengi ya kufanya mpaka awe amekwivya. Nikimkumbuka humud huwa nasikitika sana.
Dah.. Huyu Mtalamu Humud alipotea kimzaha mzaha.
 
Mkude ana uzuri gani? Sema ni mzuri akiwa huko kwenu simba! Ni wakawaida sana! Feisal ndio kwanza anaanza kudhihirisha uwezo wake, baada ya miaka 2 atakuwa mbele huko! Huyo Mkude kila akifanya majaribio anafeli.... Ndio mjue wakawaida.
Usilinganishe mwanga na Giza. Si makosa yako unaongozwa na hisia
 
Toto ana udambwi-udambwi Zaid ya hapo kwa Mkude ataisoma no. Ingawaje naona umri unakimbia Pamoja na akina nyon na yondan
 
Back
Top Bottom