Wadau wapendekeza Elimu ya Msingi kuishia darasa la 6

Kama vipi tuchukue waingereza warudi tu watutawale na elimu nzuri watupe mbona hivi
 
Mimi ninachokiona ni kuwa wanaamua Sasa kuitanua elimu ya msingi, Yaani baads ya kuishia drs la 6, Sasa mtoto atasoma hadi kidato Cha nne.. Hii ina maana kuwa elimu ya msingi itaanzia drs la 1- kidato Cha nne, na ndiyo maana wameondoa drs moja hapo ili kupunguza mzigo. Kuhusu mtihani watafanya kidato Cha nne Kama tathmini ya kumpima mwanafunzi.. Kosa ninaloliona hapo ni ktk lugha ya kujigunzia,kuchagua tahasusi mtoto akimaliza tu elimu ya msingi, pia ni Kosa.
 
Huu mpango umewashirikisha wenye nchi lakini?
Au bafo tunaendelea kuamini kaba Viongozi ndo wana akili mbadala zaidi ya wenye nchi?
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukos maarifa,mtoto wa darasa la sita atachagua nini,mnataka kuiua nchi ili wenye nacho waendelee kutamba.
Mtoto wa miaka 13 hajui masomo gani anataka kuchukuwa? elimu gani wanayotoa darasa la saba? wakati watoto wa Kenya tu hapo miaka 12 wako chuo kikuu miaka 8 na 4 kwisha wako mitaani wanatafuta maisha sisi tunapiga miaka 13 7-4-2 na quality zero halafu unataka kushindana? mtoto yuko primary mpaka anabeba mimba maana miaka 14 yuko primary hata haogopi tena lazima tubadilike miaka michache lakini quality. Jirani zetu wa Kenya kwa sababu wanatutangulia mwaka watoto zao wako sokoni wakati wa kwetu bado wako shuleni wakitoka nafasi zimejaa.
 
la msingi kama Mwandishi nguli na mbobezi ni vyema sasa ukaanzisha harakati za kuhakikisha elimu ya Tanzania inakuwa ni kiingereza msingi mpaka chuo kikuu au kiswahili mpaka chuo kikuu, tusimamie kimoja katika hivyo na kuwekeza huko.
Mkuu nyau wangu, Nangu Nyau , hii inahitaji specialization, mimi nimejikita kwenye developmental news, watu wa educatinal news wapo watalifanyia harakati.
P
 
Huu mpango umewashirikisha wenye nchi lakini?
Au bafo tunaendelea kuamini kaba Viongozi ndo wana akili mbadala zaidi ya wenye nchi?
Wenye nchi wako busy ku comment kwenye picha za Zari huko sheria ikipita ndio utaona ehhh kuna nini tena kimetokea ni kama yale ya tozo yanapitishwa watu wako busy Fiesta...na betting
 
Mkuu nyau wangu, Nangu Nyau , hii inahitaji specialization, mimi nimejikita kwenye developmental news, watu wa educatinal news wapo watalifanyia harakati.
P
Kuna haja ya kujiuliza kwani shida hapa ni lugha au kufahamu unachojifunza? Germany, Russia, Korea, China, Turkeym Finland sijui Japan hawa wanajifunza kwa English? hizi nchi wanatoa elimu kwa lugha zao na English ni somo tu tuache kudhani mtoto akiongea kizungu ndio ana akili watoto wapimwe kwa kuweza kujieleza na ufahamu wa mambo lugha ni chachu maana kama kuongea tu English ndio kipimo chetu basi safari ndefu tunayo. Hapo India tu wanatumia lugha yao na herufu zao hata Israel lakini English ni somo tu kama masomo mengine.
 
Nikuulize Kenya hawapati mimba????Na hiyo elimu ya Kenya inatuzidi nini???Ukienda Kenya asilimia kubwa ya Wanawake wa Kenya wanakuja kuolewa lakini wanakuwa walishazaa kitambo.
 
😭😭😭😭😭😭
 
Lakini wanaongea Kiingereza fasaha tofauti na sisi hao wote uliowataja.
 
Nikuulize Kenya hawapati mimba????Na hiyo elimu ya Kenya inatuzidi nini???Ukienda Kenya asilimia kubwa ya Wanawake wa Kenya wanakuja kuolewa lakini wanakuwa walishazaa kitambo.
Elimu ya Kenya inatuzidi nini? kweli unataka nikujibu hapa au unafanya utani. Nadhani jiulize wakati tunataka kuruhusu ajira free EA Tanzania walisema nini? bado hatuko tayari kushindana na wa Kenya sasa waulize wanasiasa walikuwa wanamaanisha nini.
 
Lakini wanaongea Kiingereza fasaha tofauti na sisi hao wote uliowataja.
Wafaransa hawaongei, Wa Japan lugha yao tu Spain lugha yao na hata wa Italy yao na wakiongea English wengi wao bora wewe ila Germany wanaongea sababu ni somo muhimu kwao. Lakini hata hapa yuko Wema sepetu ana English maridadi sana lakini kichwani zero.
 
Wenye nchi wako busy ku comment kwenye picha za Zari huko sheria ikipita ndio utaona ehhh kuna nini tena kimetokea ni kama yale ya tozo yanapitishwa watu wako busy Fiesta...na betting
Unaweza kunieleza lini Bunge letu liliwahi kutunga sheria?

Natumaini umelielewa swali langu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…