Wadau yamenikuta, hawa Wanawake hawa…

Wadau yamenikuta, hawa Wanawake hawa…

Yaani unashindwa kufanya maamuzi kwa jambo dogo kama hilo??? Acha kutsnia wanaume wenzako
 
Usilazimishe Mwanamke awe upande wako, Hapo hata kama unaona kosa ni la Nani au Nani ila kama na Mwanamke pia kakubadilikia basi Mpe nafasi aende na Wewe Fanya yako.

Ukianza kazi ya upelelezi au kuanza kumfata mhusika basi hapo unajitafutia Majuto!
 
Habari ya usiku huu.

Kijana mwenzenu yamenikuta aisee. Ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja.

Kuna binti nilikuwa nae na nilipanga kumuoa,lakini masiku ya hivi karibuni nimeona amebadilika hayuko kama zamani (hapa najua wakubwa wenzangu mmenielewa kwamba kitu kidogo anakasirika na kukuza mambo,nikajua hapa natafutiwa sababu ya kuachwa,machale yakanicheza mapema). Sababu binti namjua vilivyo,nikambana sana akaamua kufunguka hiyo ilikuwa juzi. Akasema ni kweli kuna mtu ameunganishiwa na ndugu zake yaani dada zake na wameanza kuwasiliana na kwa mujibu wake huyo muhusika hakumwambia kama ana mtu na binti amekubali kuolewa na huyo mtu.

Lakini katika kuunganisha doti nahisi huyo muhusika(yaani muoaji) nina mfahamu kabisa. Sasa nimekaa hapa najiuliza je nipotezee nikubali matokeo au nimfate mdau nimwambie ukweli ?

Ushauri wenu tafadhali.
Unadhan ukikwambia ukweli itasaidia nn?? Kifupi binti hana msimamo na mpaka kufikia hapo inaonesha dhahiri binti moyo wake ushageuka na hauko upande wako tena mwanamke akishafikia hatua hiyo usijaribu kumlazimisha kugeuza moyo wake tena yatakukuta makubwa zaid. Huyo tayari sio wako mwache aende jipange upya kutafuta mwingine wako wengi sanaaa
 
Mungu ameamua kukuonyesha mapema kabisa tabia ya huyo mpenzi wako,mshukuru Mungu kwa hilo jambo kisha elekeza nguvu,maarifa na maombi katika kutafuta hela,huyo hakufai hata kama ungekuja kumuoa angekuja tu kudanganyika tu,

Good luck.
Kweli unachosema.
 
Mkuu ukitajiwa Madada au Wazazi jua fika wametajwa tu kama kisingizio ili kubalance lawama..

Ila kiukweli Maamuzi ni ya mhusika mwenyewe. Utakuta hata hao madada hamna wanachokijua kinaendelea.
Hili linaweza kuwa kweli ndiyo maana kuna muda nawaza au niwapigie ndugu zake na mama yake au nikaushe tu.
 
Mkuu ukitajiwa Madada au Wazazi jua fika wametajwa tu kama kisingizio ili kubalance lawama..

Ila kiukweli Maamuzi ni ya mhusika mwenyewe. Utakuta hata hao madada hamna wanachokijua kinaendelea.
And huo ni ukweli. Wazazi huwa ni kisingizio. A.k.a wabebeshwa lawama. Ukweli ni kwamba ukishaona hizo swag wala usihangaike kumtafuta muhusika tena
 
Hili linaweza kuwa kweli ndiyo maana kuna muda nawaza au niwapigie ndugu zake na mama yake au nikaushe tu.
Kwani ulishapeleka barua ya uchumba na kukubaliwa au ulishatioa mahari? Narudia achana na huyo dada mfute katika maisha yako

Kwani ukiwapigia ndugu zake itakusaidia nini. Utoto tupu unatuletea, rudi shule ukasome, umeingilia vitu vimekuzidi umri
 
Dalili zinaonesha kama huna hela hivi, ikiwa kweli achana naye, tafuta hela utakuja kunishukuru.
Hahahaha hapana kabisa watoto wa kike huwa wanashikwa sana masikio.

Ila ngoja niendelee kutafuta pesa kaka.
 
Kwani ulishapeleka barua ya uchumba na kukubaliwa au ulishatioa mahari? Narudia achana na huyo dada mfute katika maisha yako

Kwani ukiwapigia ndugu zake itakusaidia nini. Utoto tupu unatuletea, rudi shule ukasome, umeingilia vitu vimekuzidi umri
Shukrani kwa ushauri wako mzuri kaka.

Nilitaka kuhakikisha tu,maana dogo anaendelea kunitafuta mpaka usiku wa manane anapiga simu.
 
And huo ni ukweli. Wazazi huwa ni kisingizio. A.k.a wabebeshwa lawama. Ukweli ni kwamba ukishaona hizo swag wala usihangaike kumtafuta muhusika tena
Hili la kumtafuta nimeshaliacha ila yeye ndiyo ananitafuta.
 
Mimi nimekubali matokeo lakini namuona binti kama anataka tuendelee na kuwasiliana nikamwambia huo ujinga siufanyi aheshimu mawazo yake.

Ila katika kuwaza na kuwazua na kuunganisha nukta nikapa wazo au nimchane mdau nini ?!
Be a gentleman and move on..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom