Wadau yamenikuta, hawa Wanawake hawa…

Wadau yamenikuta, hawa Wanawake hawa…

najiuliza je nipotezee nikubali matokeo au nimfate mdau nimwambie ukweli ?
Mkuu hao viumbe wakishageukia upande mwingine nyosha mikono juu mshukuru Mungu kwa yote.

Kwa kifupi potezea hata ungemweleza ukweli jamaa haitosaidia zaidi utaonekana mnafiki.

Penzi ni upofu hasa likiwa changa!! Tuishi nao kwa akili!!
 
Mkuu hao viumbe wakishageukia upande mwingine nyosha mikono juu mshukuru Mungu kwa yote. Kwa kifupi potezea hata ungemweleA ukweli jamaa haitosaidia. Penzi ni upofu hasa likiwa changa!! Tuishi nao kwa akili!!
Nakuelewa vizuri sana kaka. Mimi nimeonyesha msimamo huo.
 
Kiukweli mimi sina shida na mambo kama haya huwa yanatokea sana,kama mmoja wetu huko juu alivyo elezea.

Kingine hata binti mwenyewe anakubali sina shida ni ishu tu za madada.
[emoji23][emoji23][emoji23], Kujua km una shida au hauna shida ni Mpaka tusikie na upande wa pili wanasemaje kuhusu jambo hili.
 
Habari ya usiku huu.

Kijana mwenzenu yamenikuta aisee. Ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja.

Kuna binti nilikuwa nae na nilipanga kumuoa,lakini masiku ya hivi karibuni nimeona amebadilika hayuko kama zamani (hapa najua wakubwa wenzangu mmenielewa kwamba kitu kidogo anakasirika na kukuza mambo,nikajua hapa natafutiwa sababu ya kuachwa,machale yakanicheza mapema). Sababu binti namjua vilivyo,nikambana sana akaamua kufunguka hiyo ilikuwa juzi. Akasema ni kweli kuna mtu ameunganishiwa na ndugu zake yaani dada zake na wameanza kuwasiliana na kwa mujibu wake huyo muhusika hakumwambia kama ana mtu na binti amekubali kuolewa na huyo mtu.

Lakini katika kuunganisha doti nahisi huyo muhusika(yaani muoaji) nina mfahamu kabisa. Sasa nimekaa hapa najiuliza je nipotezee nikubali matokeo au nimfate mdau nimwambie ukweli ?

Ushauri wenu tafadhali.
Huyo ni mwenyeji au mzaliwa wa Pwani au Dar
 
Mpaka hapo unataka ushauri????njoooni mchukue mioyo yetu mtaishi vyema kabisa,hakuna mbugila yeyote kukusumbua
 
Mpaka hapo unataka ushauri????njoooni mchukue mioyo yetu mtaishi vyema kabisa,hakuna mbugila yeyote kukusumbua
Unajua sisi wengine hili ndiyo linatutokea kwa mara ya kwanza,kwahiyo tunataka ushauri ili kupata ukomavu na kujizatiti zaidi.
 
Sawa kaka,ila hata bibie mwenyewe anakiri ya kuwa sina shida yoyote.
Mhhhh!!!!,Sasa Mbona unamsemea?,Kungekuwa na uwezekano na yeye angeshiriki mjadala huu angejisemea mwenyewe,lkn ndio hivyo inakuwa ngumu.
 
Mhhhh!!!!,Sasa Mbona unamsemea?,Kungekuwa na uwezekano na yeye angeshiriki mjadala huu angejisemea mwenyewe,lkn ndio hivyo inakuwa ngumu.
Haya nimeyanukuu toka kwake sababu nilivyoona amebadilika ilinibidi nionane naye ana kwa ana,tukaonana katika mazungumzo hayo akasema hayo.
 
Back
Top Bottom