Wadau yamenikuta, hawa Wanawake hawa…

Wadau yamenikuta, hawa Wanawake hawa…

Muache aende zake piga zako kimya, mke mtarajiwa anashikiwa akili na dada zake like for real? Aisee muache
[ Namna hii iliwahi kunikuta way back 2013 mke mtarajiwa anakubali kila anacho shauriwa na nduguze mara muda wa kuolewa bado mara hiki mara kile nikasema shi.t!!! Nikapotezea mpaka kesho.
 
Mimi nimekubali matokeo lakini namuona binti kama anataka tuendelee na kuwasiliana nikamwambia huo ujinga siufanyi aheshimu mawazo yake.

Ila katika kuwaza na kuwazua na kuunganisha nukta nikapa wazo au nimchane mdau nini ?!
Acha lipite baada ya muda utakuwa na amani sana kuliko ukizumgumza na jamaa halafu bado akamuoa watajiona wanakalove story fulani hivi kalikopitia majaribu.
 
Sijapeleka barua ila kwao wananifahamu na ilikuwa mwezi wa tatu nifanye jambo si unajua sisi Waislamu mambo yetu huwa si mengi.
Hapo ndipo ulipokosea, wazazi hawakutambui bila barua au mahari. Narudia tafuta elimu, tafuta hela kisha utampata mke wako, huyo si mkeo alikuwa ni wa kusafishia rungu tu
 
Sasa nimekaa hapa najiuliza je nipotezee nikubali matokeo au nimfate mdau nimwambie ukweli ?

Ushauri wenu tafadhali.

Mzee baba, iko hivi...mchuchu yoyote akizingua na akaamua kukuacha na akafuatana na mwanaume mwingine basi achana naye...

1. Wanawake huwa wana hatua zao na hatua hizo wameziweka katika vipindi, moja ya vipindi hivyo kipo hicho kimoja ambacho joto la kuolewa huwa linapanda, kama husomeki basi atakushushia kitu kizito kichwani hakuna rangi utaacha iona...

2. Nimekuwa nikiandika hapa na narudia tena kwako mzee, wachuchu wapo wengi sanaaaaa yaani wapo wengi mno. Mchuchu mmoja akizingua, na mzinguo ukiwa wa kiwango hichi cha kuleteana mazereu, piga chini tafuta mchuchu wa kuendana na wewe...

3. Usifanye kosa la kumfuata mwanaume mwenzio wakati uamuzi umefanywa na mchuchu wako...
 
Kwanini???.Hebu iga Hekima ya Kimahakama kutoa Hukumu baada ya kusikiliza pande zote mbili;Wewe umemsikia tu mlalamikaji unahitimisha kwa kusema kuwa dada na Ndugu zake hawana akili,je umewasikiliza na wao ukasikia wanajiteteaje?. Ukute mtoa Post ndo ana shida ndio maana hao Ndugu wa Binti wamemuunganishia kwa Mwanaume mwingine.
Sijakataa na inawezekana pia mtoa mada ana mapungufu yake, lakini mpaka mwanamke anafikia hatua ya kukubali kufanyiwa maamuzi yatakayogharimu maisha yake ni dhahiri kuwa kuna dosari kwenye mfumo wake wa akili.

Sipo hapa kutetea upande wowote.
 
Kwanini???.Hebu iga Hekima ya Kimahakama kutoa Hukumu baada ya kusikiliza pande zote mbili;Wewe umemsikia tu mlalamikaji unahitimisha kwa kusema kuwa dada na Ndugu zake hawana akili,je umewasikiliza na wao ukasikia wanajiteteaje?. Ukute mtoa Post ndo ana shida ndio maana hao Ndugu wa Binti wamemuunganishia kwa Mwanaume mwingine.
Hata mimi nimesoma hiyo komenti nikashangaa tu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Habari ya usiku huu.

Kijana mwenzenu yamenikuta aisee. Ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja.

Kuna binti nilikuwa nae na nilipanga kumuoa,lakini masiku ya hivi karibuni nimeona amebadilika hayuko kama zamani (hapa najua wakubwa wenzangu mmenielewa kwamba kitu kidogo anakasirika na kukuza mambo,nikajua hapa natafutiwa sababu ya kuachwa,machale yakanicheza mapema). Sababu binti namjua vilivyo,nikambana sana akaamua kufunguka hiyo ilikuwa juzi. Akasema ni kweli kuna mtu ameunganishiwa na ndugu zake yaani dada zake na wameanza kuwasiliana na kwa mujibu wake huyo muhusika hakumwambia kama ana mtu na binti amekubali kuolewa na huyo mtu.

Lakini katika kuunganisha doti nahisi huyo muhusika(yaani muoaji) nina mfahamu kabisa. Sasa nimekaa hapa najiuliza je nipotezee nikubali matokeo au nimfate mdau nimwambie ukweli ?

Ushauri wenu tafadhali.
Achana nae, fanya yako. Huyo ni mbwa kama wa miguu minne. Hutaweza kummiliki wakati amekwisha lamba ya upande wa pili.
 
Hapo ndipo ulipokosea, wazazi hawakutambui bila barua au mahari. Narudia tafuta elimu, tafuta hela kisha utampata mke wako, huyo si mkeo alikuwa ni wa kusafishia rungu tu
Nimekuelewa vyema kaka.
 
Ulokuwa huna akili ni weyee.Watu wanaangalia maslahi huyo kijana washamuona hana mpango yeye yuko katika penzi wenzako wako katika noti na maslaha ,mapenzi ya mdomo yamekwisha na weye kijana tafuta kazi ufanye mapenzi hayalazimishwi hao wake wapo kibao ndio kwanza wanazaliwa .
Povu lako chukua mwenyewe staki mabalaa😂😂 shame!!
 
Habari ya usiku huu.

Kijana mwenzenu yamenikuta aisee. Ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja.

Kuna binti nilikuwa nae na nilipanga kumuoa,lakini masiku ya hivi karibuni nimeona amebadilika hayuko kama zamani (hapa najua wakubwa wenzangu mmenielewa kwamba kitu kidogo anakasirika na kukuza mambo,nikajua hapa natafutiwa sababu ya kuachwa,machale yakanicheza mapema). Sababu binti namjua vilivyo,nikambana sana akaamua kufunguka hiyo ilikuwa juzi. Akasema ni kweli kuna mtu ameunganishiwa na ndugu zake yaani dada zake na wameanza kuwasiliana na kwa mujibu wake huyo muhusika hakumwambia kama ana mtu na binti amekubali kuolewa na huyo mtu.

Lakini katika kuunganisha doti nahisi huyo muhusika(yaani muoaji) nina mfahamu kabisa. Sasa nimekaa hapa najiuliza je nipotezee nikubali matokeo au nimfate mdau nimwambie ukweli ?

Ushauri wenu tafadhali.
Yote ya nn mkuu. Ukishaona mambo yamefikia huko huwa haina haja ya kutafuta reconciliation. Utaumia bure na pengine kufikia maamuzi ya ajabu. Haya na mambo ya kugive up easily bila kuwaza.
 
Kuna watu mna mada za kijinga hadi unajiuliza huyu ni mwanaume kweli?

Mtu anakwambia kabisa anamtu mwingine wewe unajidai unamfikiria sijui ndugu wamefanyaje sijui namjua huyo mtu

pumbavu ningekuwa hapo ungekula mueleka mmoja kama wa Jamaa wa clouds
 
Mkuu hapo hauana chako beba maumivu somga mbele tena anza kumkalia kimya uone atakavyojuta tafuta mwanamke wa kuziba upweke haraka.
 
Back
Top Bottom