Wadogo zetu wa sasa wana ujasiri sana, sio waoga kabisa

Wadogo zetu wa sasa wana ujasiri sana, sio waoga kabisa

Niende moja kwa moja kwenda jambo la msingi.

Ninayezungumza hapa pia ni kijana sio kwamba ni mtu mzima sanaa kivile, hapana. Naanza kwa kusema hili; ili kuondoa ile dhana ambayo kwa sasa inalalamikiwa na vijana wengi mitandaoni kwamba "Wazee" na "Watu wazima waliofanikiwa" wanawaonea vijana kwa kuwasema sema na kuwanyanyasa kama hivi post ambazo kwasasa zimetapakaa mitandaoni [emoji116][emoji116][emoji116]

View attachment 2790127

Na hata hapa jukwaani kuna kijana mmoja juzi kati kaleta hoja kwamba "Mabroo" wamekuwa wakiwasakama tu ila hawatoi michongo yoyote pindi wanapoombwa kufanya hivyo, uzi huu ulioletwa na member Natafuta Ajira [emoji116][emoji116][emoji116]

Lakini kiukweli, vijana kwasasa wana tatizo la kujiamini kupitiliza kiasi kwamba tafsiri rahisi na ya haraka unayoweza kupata ni kwamba "Don't care". Sijui sababu ni nini hasa maana kunaweza kuwepo na zaid ya moja, mfano;

1. Kujikinai/kujikatia tamaa

Sababu ya kuleta hoja hii ni tukio nililokutana nalo ofisini kwangu juzi siku ya mechi ya Simba na Waarabu. Iko hivi;

Kwa mwezi mzima toka September kuna kijana wa chuo alikuja kuomba kufanya field, na baada ya kum-study nikagundua kuwa ni mtu ambaye alichelewa kuanza field na mpaka wakati huo hakuwa amepata.

Sababu ni nyingi lakini moja wapo ni ishu ya kipato mambo ya nauli alikuwa amelenga kupata hapa centre ambako atapanda gari 1 tu kwenda na kurud nyumbani kuepuka ghara nyingi za usafiri na hana mkopo shuleni, hivyo hana fungu la field toka bodi.

Nilimu-asses kwa namna nilivyotaka ili kujiridhisha kisha nikaona sio mbaya akatu-join afterall uhitaji wa mtu kama wake kwetu ungetupa manufaa katika namna fulani.

Basi bwana tukafanya kazi weee mpaka juzi kati ambapo akawa amemaliza field yake na vyuo vinafungua so anaenda kumaliza masomo yake.

So hii siku ya mwisho nikawa na mazungumzo nae kwa ajil ya tathimini mbali mbali kulingana na majukumu aliyokuwa nayo ofisini ili kupata feedback, lakini pia kuangalia namna gani ya kuingiza tathimini hizo katika Logbook yake ili ikasahihishwe na supervisor wake.

Sasa hii siku ndio ilikuwa inachezwa mechi ya Simba na Mwarabu, na mida kama hii ya 11 kwenda 12 ndio tulikuwa kwenye discussion. Sasa katikati ya mazungumzo, kwanza dogo full time kuchat chat.

Hii kitu nilishawahi kumuona nayo hata katika vikao vya kawaida vya ofisi na nikampa warning na kumfunza ni namna gani anapaswa kuwa ana-behave anapokuwa katika mazingira ya kikazi haswa kwenye vikao akiwa na sie seniours wake.

Sasa siku hii aliniacha hoi huyu bwana mdogo, ghafla katikati ya maongezi akainuka na kusema "Bosi, nafikiri hayo mengine nitatafuta muda mwingine tumalizie, mimi nataka niwahi kumuona Rais wa FIFA hapo Taifa maana muda umeenda sana na mechi itaanza sitaki kuikosa, unaonaje Boss?" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Honestly, nilipigwa na butwaa sana kwa hizi guts alizonazo huyu dogo, nikamtazamaa kisha nikasema sawa haina shida, unaweza kwenda.

Alipotoka ofisini nilijikuta nacheka sana lakini hakikuwa kicheko cha furaha bali ni mshangao na huruma pia. Nikajiuliza hivi ni mimi tu ndio nilikuwa fala linapokuja suala la kazi au? Hivi huu ni ujasiri au recklesness?

I was about to let him know kwamba we would love him to join us us next year akimaliza chuo maana mapungufu yale madogo madogo ningejua namna ya kum-shape maana bado ana mindset ya kitoto kama mwanafunzi, ila kwa hiki kilichotokea nikashindwa hata kufika huko kote.

Sasa hapa vijana unawaza, unasema hivi wanataka nini tena?

Anyway ni hayo tu, na by the way sio vijana wote wako hiv!
Mkuu naomba kuuliza. Muda wa kazi ni saa ngapi ofisini? Kwa nunavyojua saa 11 jioni kwa utaratibu wa Tanzania iyo ni overtime. Usije ukamrushia kijana lawama kumbe ni wewe haukuzingatia muda wa kazi.
 
Mkuu naomba kuuliza. Muda wa kazi ni saa ngapi ofisini? Kwa nunavyojua saa 11 jioni kwa utaratibu wa Tanzania iyo ni overtime. Usije ukamrushia kijana lawama kumbe ni wewe haukuzingatia muda wa kazi.
Huku kwenye details wala hata usihangaike nako..
NB
Huna maisha Ila unaleta habar za overtime, men!!!. Anyway hii haihusian na mada.
 
Ni kawaida ya vijana wengi hasa hawa ambao wako chuoni kwanza hawa wazi wakishamaliza chuo nini kinafuata, wao wanajua wakimaliza chuo watapata kazi tu laiti wangejua kuna watu wamemaliza chuo miaka na miaka hatujapata kazi hata izo intern kuzipata ni changamoto wasingeleta upuuzi kwenye field zao, wengi wao kwanza field anaona kama kujichosha
Ni kwel mkuu. Na mbaya zaid hawaelewi ukiwaeleza haya masuala. Wanaona kwakua wewe hukupata ajira soon baada ya kumaliza bas hilo ni juu yako wao wana pia wana bahat zao..simple...!!
 
Hata huku kwenye ishu za biashara na ujasiriamali kuna madogo wengi sana wazinguzi. Kuna dogo mmoja alifungua duka dogo la nguo sasa kwenye mwezi wa 8 wakati biashara ya jezi ndo imezidi kupamba moto nikaona ngoja dogo nimpige jeki angalau na yeye auze jezi apige hela. Nikamshauri na kumwambia akimbizane na msimu halafu kama hela hana apite dukani kwangu achukue hata 100pcs na kuziuza aniletee tu changu akishauza. Kesho yake namuuliza dada wa dukani kama dogo alifika akajibu hapana. Baada ya siku kadhaa nikakutana na dogo barabarani akaniambia "Bro usijali nikipata muda nitapitia hizo jezi"... mimi kama kawaida nikamwambia aache upuuzi nilitaka kumsaidia ila nimefuta huo msaada. Tunavyoongea duka lake kashafunga hali ngumu.
 
Mambo ni mengi mnoo hawa madogo. Mengi sana.Ujue mpaka unajiuliza "hiv ni shida zangu au zake?".
 
Ni hivi na hawa vijana wa leo wale waliopambana kwa misimamo yao,na wakafika nafasi za juu kikazi, wanahakikisha wanaleta vijana wa mitazamo yao kufanya nao kazi,
Mara ngapi unaenda usaili wa kazi unakutana na vijana wadogo tu wanakusaili na mi mvi yako na pia kukupiga chini...
Elimu ya sasa imebadilika sana na kuwafundisa vijana kujiamini na kujielewa kuliko elimu ya zamani ya nidhamu ya uoga...
Nenda na wakati, hawa ndio wana uwezo wa kuleta mawazo na mbinu mpya za mafanikio ya kampuni...
Ukijikuta unafanya kazi sehemu ambapo kuna mtindo au mfumo wa kusema,
"We always do it this way"
Hapo ujue unaenda kudumazwa akili na kufanywa "bot" wa kuitika "Ndio Bosi"
 
Hakuna mahali popote elimu ilipobadilika mkuu.Elimu ni ile ile toka ilipoachwa na mkoloni, fahamu unachokiongea usije ukaonekana sio!.

Mabadiliko mengi ya leo ni social engineering zaidi...Na wengi wenu vijana sio kwamba mnajiaminnkwa maana ya kuwa na CONFIDENCE bali ni watu RECKLESS mliojizira HAMJALI na tena mmekosa SOCIAL ETHICS linapokuja suala la kazi. Jitazamen madogo.

Kumsail ma kumpiga mtu mzima chini wala haina maana mtu anajiamin, ni suala lanutaratibubtu kufuatwa. Na bado lichabya yote hayo, badobuna weza ukamkataa mtu kwa adabu na heshima ,huhitaji huko unaokokuona wewe ndio kujiamini.

KWakifupi vijana mmejaa EGO wala sio CONFIDENCE.
 
Mbona hujam quote mtu mkuu, relax kuwa na amani. Naeleea hilo ndio maana juu nikaanza na angalizo kuwa sio vijana wote. But pia umeona shuhuda za watu huko juu kwamba wamekutana sana na kesi zinazofanana na hizo kwahiyo kwa upande mwingine niko sahihi nikitumia uwingi "vijana" maana ni wengi mnoo wenye changamoto hizi
Nilikuwa nimem-quote mtu, itakuwa errors za system ya JF.

Unaendelea kufanya circular argumentum tu?

Kwasababu wawili, watu wamekuunga mkono kwamba kwa pamoja mnahitimisha vijana wote tupo hivyo.

Narudia tena, msitumie mifano ya hao wachache walionekana kuwa kwaza kutuhukumu vijana wote.

Ndio maana kuna usaili, ukiona huyu hafai labda hana maadali mazuri lakini ana maarifa stahili na mwingine kinyume chake, mtaamua nani mumchukue.

Nikasema tuhukumuni kwa merits based approach.

Kuna wadau juu hapo, wametoa sifa kwa mabinti kuwa wapo vizuri kwenye kazi mbona hili hamlioni kama ni contradiction na hoja yenu?

Itoshe kusema, mti wenye matawi dhaifu ni matokeo ya mizizi isiyokuwa imara.

Kama wazazi na waandamizi mnajukumu na kukijengea uwezo kizazi hiki ili kiwe bora kama mlivyojengwa ninyi.

Au ninyi mizizi ndio siyo imara, matokeo yake tunayaona kwenye matawi sisi?
 
Ni kwel mkuu. Na mbaya zaid hawaelewi ukiwaeleza haya masuala. Wanaona kwakua wewe hukupata ajira soon baada ya kumaliza bas hilo ni juu yako wao wana pia wana bahat zao..simple...!!

Sijui huwa wanawazaga nini ila hapo juu nimeona wengi wanawatetea vijana wakike wakipata kazi wanakuwa weredi kazini lakin nishakutana na hao viumbe ndio wasiojielewa kabisa tena ukikutana na wale ambao kwao kidogo vijisent vipo ndio kabisa yani kwenye akili yake anawaza kula bata tu kuzurura zurura mlimani city sijui beach
 
Back
Top Bottom