Wadogo zetu wa sasa wana ujasiri sana, sio waoga kabisa

Mkuu naomba kuuliza. Muda wa kazi ni saa ngapi ofisini? Kwa nunavyojua saa 11 jioni kwa utaratibu wa Tanzania iyo ni overtime. Usije ukamrushia kijana lawama kumbe ni wewe haukuzingatia muda wa kazi.
 
Mkuu naomba kuuliza. Muda wa kazi ni saa ngapi ofisini? Kwa nunavyojua saa 11 jioni kwa utaratibu wa Tanzania iyo ni overtime. Usije ukamrushia kijana lawama kumbe ni wewe haukuzingatia muda wa kazi.
Huku kwenye details wala hata usihangaike nako..
NB
Huna maisha Ila unaleta habar za overtime, men!!!. Anyway hii haihusian na mada.
 
Ni kwel mkuu. Na mbaya zaid hawaelewi ukiwaeleza haya masuala. Wanaona kwakua wewe hukupata ajira soon baada ya kumaliza bas hilo ni juu yako wao wana pia wana bahat zao..simple...!!
 
Hata huku kwenye ishu za biashara na ujasiriamali kuna madogo wengi sana wazinguzi. Kuna dogo mmoja alifungua duka dogo la nguo sasa kwenye mwezi wa 8 wakati biashara ya jezi ndo imezidi kupamba moto nikaona ngoja dogo nimpige jeki angalau na yeye auze jezi apige hela. Nikamshauri na kumwambia akimbizane na msimu halafu kama hela hana apite dukani kwangu achukue hata 100pcs na kuziuza aniletee tu changu akishauza. Kesho yake namuuliza dada wa dukani kama dogo alifika akajibu hapana. Baada ya siku kadhaa nikakutana na dogo barabarani akaniambia "Bro usijali nikipata muda nitapitia hizo jezi"... mimi kama kawaida nikamwambia aache upuuzi nilitaka kumsaidia ila nimefuta huo msaada. Tunavyoongea duka lake kashafunga hali ngumu.
 
Mambo ni mengi mnoo hawa madogo. Mengi sana.Ujue mpaka unajiuliza "hiv ni shida zangu au zake?".
 
Ni hivi na hawa vijana wa leo wale waliopambana kwa misimamo yao,na wakafika nafasi za juu kikazi, wanahakikisha wanaleta vijana wa mitazamo yao kufanya nao kazi,
Mara ngapi unaenda usaili wa kazi unakutana na vijana wadogo tu wanakusaili na mi mvi yako na pia kukupiga chini...
Elimu ya sasa imebadilika sana na kuwafundisa vijana kujiamini na kujielewa kuliko elimu ya zamani ya nidhamu ya uoga...
Nenda na wakati, hawa ndio wana uwezo wa kuleta mawazo na mbinu mpya za mafanikio ya kampuni...
Ukijikuta unafanya kazi sehemu ambapo kuna mtindo au mfumo wa kusema,
"We always do it this way"
Hapo ujue unaenda kudumazwa akili na kufanywa "bot" wa kuitika "Ndio Bosi"
 
Hakuna mahali popote elimu ilipobadilika mkuu.Elimu ni ile ile toka ilipoachwa na mkoloni, fahamu unachokiongea usije ukaonekana sio!.

Mabadiliko mengi ya leo ni social engineering zaidi...Na wengi wenu vijana sio kwamba mnajiaminnkwa maana ya kuwa na CONFIDENCE bali ni watu RECKLESS mliojizira HAMJALI na tena mmekosa SOCIAL ETHICS linapokuja suala la kazi. Jitazamen madogo.

Kumsail ma kumpiga mtu mzima chini wala haina maana mtu anajiamin, ni suala lanutaratibubtu kufuatwa. Na bado lichabya yote hayo, badobuna weza ukamkataa mtu kwa adabu na heshima ,huhitaji huko unaokokuona wewe ndio kujiamini.

KWakifupi vijana mmejaa EGO wala sio CONFIDENCE.
 
Nilikuwa nimem-quote mtu, itakuwa errors za system ya JF.

Unaendelea kufanya circular argumentum tu?

Kwasababu wawili, watu wamekuunga mkono kwamba kwa pamoja mnahitimisha vijana wote tupo hivyo.

Narudia tena, msitumie mifano ya hao wachache walionekana kuwa kwaza kutuhukumu vijana wote.

Ndio maana kuna usaili, ukiona huyu hafai labda hana maadali mazuri lakini ana maarifa stahili na mwingine kinyume chake, mtaamua nani mumchukue.

Nikasema tuhukumuni kwa merits based approach.

Kuna wadau juu hapo, wametoa sifa kwa mabinti kuwa wapo vizuri kwenye kazi mbona hili hamlioni kama ni contradiction na hoja yenu?

Itoshe kusema, mti wenye matawi dhaifu ni matokeo ya mizizi isiyokuwa imara.

Kama wazazi na waandamizi mnajukumu na kukijengea uwezo kizazi hiki ili kiwe bora kama mlivyojengwa ninyi.

Au ninyi mizizi ndio siyo imara, matokeo yake tunayaona kwenye matawi sisi?
 
Ni kwel mkuu. Na mbaya zaid hawaelewi ukiwaeleza haya masuala. Wanaona kwakua wewe hukupata ajira soon baada ya kumaliza bas hilo ni juu yako wao wana pia wana bahat zao..simple...!!

Sijui huwa wanawazaga nini ila hapo juu nimeona wengi wanawatetea vijana wakike wakipata kazi wanakuwa weredi kazini lakin nishakutana na hao viumbe ndio wasiojielewa kabisa tena ukikutana na wale ambao kwao kidogo vijisent vipo ndio kabisa yani kwenye akili yake anawaza kula bata tu kuzurura zurura mlimani city sijui beach
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…