Sio kila mtu alizaliwa kwenye shida kwamba usipomsaidia atafeli maisha. Kuna boss mmoja nilienda field, akaja binti mwingine kufanya field akapangiwa kazi ambayo hapendi na hajasomea ila anaweza ifanya. Akaomba abadilishiwe kitengo na yule boss akachukia eti binti kadharau field wakati kuna watu wanaitaka.
Kumbe binti kaja kufanya kazi fulani kupata uzoefu sababu baba yake anafanya kazi kama ile. Alipoona atapotezewa muda akaenda kufanya field ofisi ya baba yake. Kuwa boss sio lazima usikilizwe kila muda na ujifanye mungu mtu na kupenda machawa. Likewise anaweza kuja kijana ukamletea umungu mtu akaondoka kufanya mambo yake na akakuzidi ukabaki na sonona.
Huu uzi una watumwa kwelikweli. Eti boss akikuongelesha hutakiwi kuondoka, na akikutongoza hutakiwi kukataa si ndio?