Wafadhili watubane tu mpaka ifike mahala kununua kilo ya unga iwe ni mtihani halafu tuone hawa polisi, TISS na Jeshi kama wataendelea kulinda watawala

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Mimi naomba tu nchi wafadhali na mashirika ya fedha duniani, waungane wasitishe mikopo na misaada kwa asilimia 100 kama ambavyo umoja wa ulaya teyari umeonyesha mfano.

Uchumi uvurugike, tushindwe kununua hata kilo ya unga na hata mishahara iiwe shida kulipa, halafu tuone kama hivi vyombo vya dola vitaendelea kulinda watawala kwa gharama ya maisha ya watanzania kama walivyofanya kuanzia Oktoba 29 mpaka November 3, 2025.

Tena wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama wapigwe marufuku kuingia ulaya na Marekani na pia tusiuziwe silaha zozote kutoka ulaya na Marekani.

Tulikuwa tunawalaani makaburi kwa lipi kama na sisi leo tumegeuka makaburu?

Mnawezaje kuua raia mitaani kama mko kwenye kampeni ya kuua mbwa wenye vicha huku mkiwa ndio wenye dhamana ya ulinzi wa nchi na watu wake?

Inasikitisha na kukera sana!
 
Sasa mkuu tutakao umia ni sisi wanyonge, hao unaowataja wana mishahara na malupulupu
 
Wazo zuri sana hilo!

Na hao washenzi ndo watakuwa wa kwanza kupigika.
 
Sema Wazungu wakikuamulia lazima wakunyoe. Warusi tu ndo wanatamba kwasababu wao ni Wazungu ma genius

Unaweza kushanga wakaanza na vikwazo vya silaha halafu hapo hapo unasikia Malawi, Rwanda, Uganda, na Kenya wanaleta chokochoko, wakati ambapo meli za mabeberu zimepaki kuzuia silaha kuingia bongo.

Vikwazo huwa vinanawiri kwenye mazingira ya chaos
 
Bila wao kupatwa na Chochote hatuwezi fika muafaka kwenye hili jambo.

Kuna kitu watawala wanatakiwa wakipate, ndio wataona umuhimu wa kukaa mezani na kumaliza haya mambo.

Time will tell, Mungu ibariki Tanzania.
 
Eti landcruiser prado mbili zinapokelewa na waziri! Na kuna pikipiki sita mbioni

Waziri anasema hawa ndio washirika wetu wa maendeleo. Aibu.
wamechanganyikiwa hao mwarabu ni mtu wa ovyo sana hata hapo Gaza wameshidwa kupeleka msaada wa kibinadamu hao wanafiki waarabu muulize Ghadafi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…