Mimi naomba tu nchi wafadhali na mashirika ya fedha duniani, waungane wasitishe mikopo na misaada kwa asilimia 100 kama ambavyo umoja wa ulaya teyari umeonyesha mfano.
Uchumi uvurugike, tushindwe kununua hata kilo ya unga na hata mishahara iiwe shida kulipa, halafu tuone kama hivi vyombo vya dola vitaendelea kulinda watawala kwa gharama ya maisha ya watanzania kama walivyofanya kuanzia Oktoba 29 mpaka November 3, 2025.
Tena wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama wapigwe marufuku kuingia ulaya na Marekani na pia tusiuziwe silaha zozote kutoka ulaya na Marekani.
Tulikuwa tunawalaani makaburi kwa lipi kama na sisi leo tumegeuka makaburu?
Mnawezaje kuua raia mitaani kama mko kwenye kampeni ya kuua mbwa wenye vicha huku mkiwa ndio wenye dhamana ya ulinzi wa nchi na watu wake?
Inasikitisha na kukera sana!