Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Mkuu,
Kwanza kulikuwa na mpango wa kupiga Rami kutoka Bunju B hadi Msakuzi na kufika Mbezi Magufuli....

Pili kulikuwa na mpango wa stendi ya Njia za kusini kujengwa Mbagala....yani Dar kuwa na stendi kubwa mbili kama ilivyo Mwanza.

Ila hapa suala ni kwanini Mabasi yanaenda kupandishia watu Shekilango na vituo vya ndani....

Kuna barabara za ndani Mabasi hayaruhusiwi kupita....Mabasi yanafika mwenge kutafuta nini?
 
Kituo Chenyewe hakuna sehemu za kukaa, vituko vya binafsi kuna sehemu maalumu za kupumzika. Wanachojali ni mapato na si ustaarabu.
Pia jiji la Dar es salaam na ukubwa wake linahitaji Stand za Bus zaidi ya 3! Kigamboni, Mkuranga na Vingunguti...... aiji akilini mtu anaeishi Mbagala maji matitu bus aje apande Mbezi.....au yule anaekaa Masaki ya Pugu....aje Mbezi kupanda Bus la kwenda Lindi kwa mfano
 
Ebu wahurumie wananchi wewe, Kuna Ubaya gani ikiwa gari inalala Chanika,ikasema abiria aliyetoka nalo Mwanza ambaye anaishi Gongo la Mboto au Chanika asogezwe mpaka huko?

Unajua gharama ya mtu mwenye mizigo kutoka hapo stendi usiku saa nane kwenda Chanika au Mbagala au Kigamboni ni shilingi ngapi?.

Unataka watu wateseke eti ili wengine wafanye biashara kwenye miili yao!. Si wabadilishe aina za biashara?.
 
Nadhani ni marketing strategy wa wenye mabasi.
 
Abiria wengi wanaishi maeneo nje ya stendi. Hivyo mabasi yanaanza kwanza kuwachukua huko nje ndipo yaje stendi ya Magufuli. Ni njia moja ya kupata abiria wengi.
  • Abiria wanaoishi nje ya stendi ya Magufuli,,,wanatakiwa wafike stendi kwa mfumo wa usafiri wa ndani ya jiji....(Daladala,bolt,Bajaaj,boda)
  • Kwani unafkiri Ubungo ilikuwa karibu kwa kila mtu,,,watu wa Bunju,Chanika,Mbande,Kibada,Ununio,Mbweni,Kimbiji....ushawahi kaa hayo maeneo ,,,nayo yapo mbali kutoka Ubungo.
 
Kwahiyo kwa akili yako kama gari linaanzia safari zake Mbagala na kuishia Mbagala unataka basi hilo likiingia Mbezi stendi lishushe abiria wote hata kama basi linaenda Mbagala liende tupu liwaache abiria Mbezi kisa tu watu fulani wauze biashara zao?

Kumbuka Mbezi ni stendi kuu tu ambapo kila basi litapita hapo kushusha ama kupakia abiria kisha litaendelea na safari yake linapoishia.

Siku hizi biashara ni akili mabasi yameanza kuwafuata abiria huko huko kwenye makazi yao mfano yapo yanayoanzia safari Chanika, Kigamboni, Mbagala, Shekilango na maeneo mbalimbali.
 
Hakuna basi isiyoingua stand zote zinaingia stand ila hao wafanyabiashara wanachotaka ni kwamba hata kama inaelekea abiria wanakuoelekea iwaache hapo stand. Mimi naunga mkono basi kuanzia inakoanzia na abiria kama wapo na kuingia na kutoka na abiria ambao wanaelekea linapoelekea.
Kama ambavyo wao wanalalamika hara abiria basi kumwacha hapo wakati ana mizigo na linaelekea anakoelekea abiria naye anapata shida.
 
Mbona ndege huwa hamuombi mshushwe kwenu mnakubali kwenda airport? Utaratibu wa vituo ni muhimu sana, mkifanya shaghala baghala msilalamikie mfumo na utaratibu wa serikali.

Sasa Stand ya bus ya nini kama unaweza panda na kushuka popote?
Ww tumia akili ona aibu basi ndege aitport unafanisha na stend hata majina tu yanapishana ile inaitwa airport ...Hata pale airport kuna hotel zimejiongeza kutoa usumbufu kwa wateja wao wanao fika hapo wanamagari kabisa yanasubiri abiria.Siwezi kushuka magufuri wakati najua nikishuka shekilango hata bei ya bajaji kunipeleka ferry ni chini pia sitasbuka kubeba mizigo kutafuta sijui mwendo kasi..
 
Nadhani ni marketing strategy wa wenye mabasi.
Sasa wenye Mabasi hawatakiwi waachwe huru kiasi hiko....
Lazima wafuate utaratibu,,,
Mana sasa hayo Mabasi hadi Chanika na Vijibweni nisha yaona.....

Hatakama tupo Soko huru lakini lazima vitu vifanyke kwa utaratibu...
 
Mbona wakati ipo Ubungo shughuli zote zilikuwa zikifanyika pale? Tulikuwa tukila na kununua bidhaa kabla ya safari
 
Hapo unakosea, nadhani mabasi yanaweza kushusha huko kote kakini safari ikianza lazima gari iingie stendi na ikiisha inapita stendi kabla ya kuelekea huko kwingine.
Nadhani hilo ndio la muhimu.
 
Kwamba mimi ni mkazi wa Bunju halafu basi linatoka Arusha linapita njia ya Bagamoyo kwahiyo nisishuke Bunju bali nije hadi Magufuli stendi ndiyo nishuke halafu nianze kupambania usafiri wa kurudi Bunju ambapo nilipapita?

Hizi akili ni za kipumbavu kupita kiasi. Yaani mtu asishushwe kituo chake bali aletwe hadi Magufuli stendi kisa tu kuwanufaisha wafanyabiashara?
 
1. Kwani mtu anayeshuka uwanja wa ndege na anakaa Kunduchi huwa anafikaje nyumbani...?

2.Kwanini gari ziende Shekilango au Mnazi mmoja .....?
Kitu ambacho huelewi ni kwamba abiria wanaooelekwa urafiki au shekilango ni kama offer ya mwenye basi na sio sheria. Ni mwenye basi kumjali mteja wake na kumpunguzia gharama zisizo za lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…