Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Dar si ni kama wilaya ya ulambo tu kwa ukubwa!! Watu wa dar mkishuka stend kufika unakolalamikia ni mbali nauli buku 2 imezidi sana. Kuna watu tunashushwa stend ulambo kufika nyumbani elfu 8, halafu mnataka stendi kila wilaya wakati kigoma hata lami ni shida.
Usilinganishe dar na urambo. Na ni Jiji urambo ni Wilaya.
 
Tatizo ni tunabadili matumizi ya stand kutoka kwenye kurahisisha usafiri kwa watu wa mkoa husika kuwa:

1. Soko kwa wamachinga.
2. Nyenzo ya kubadili kakijiji kuwa mji.

Pakichangamka stand inapelekwa mbali. Sasa ikienda mbali vya kutosha lengo la kurahisisha usafiri linapotea maana unakuwa na stand mkoa X iliyo karibu na mkoa Y kuliko mkoa X.
Ni uvivu tu wa kufikiri wa wanasiasa, hasa kwa sababu wao sio watumiaji wa hizi stendi.
 
Hapo utakuwa unampangia mwenye basi Cha kufanya. Yeye kaamua kuwasaidia abiria wake basi.
Na mwenye bus anawajibika kwa waliompa leseni ya biashara!! Complain zozote abiria fikisha kwa wasimamizi (LATRA) na si kuwatumia wamiliki wa mabasi. Mbona zikitokea ajali wa kulalamikiwa ni latra eti hawadhibiti makosa ya waendesha mabasi
 
Kwenye biashara Kuna offer Kwa mteja ili kumvutia awe mteja wa kudumu Kutokana na offer. Mabasi yametumia hiyo gap kupata loyal customers. Ni mfumo wa kibiashara.
Sasa serikali itawashughulikia kwa kutoheshimu mkataba wa kikazi.
 
Unatoka zako kwenu Tukuyu na mikungu yako ya ndizi na viroba vya viazi mbatata wanakushushia Mikumi ujitafutie daladala za kufika kwenu Kibamba🤣
Hii yote wanafanya kwa vile wao hawapandi mabasi
 
Naongea km afisa wa mipango miji.
Sasa waambie waliokutuma tunataka stendi nyingine kubwa kabisa ya mabasi hapo Urafiki/Shekilango serikali ilipopanunua. Serikali itakapoanza kupaendeleza wajenge majengo ya maghrofa 30 halafu chini kwenye basements tunataka stendi kubwa zaidi ya ilivyokuwa ubungo.
 
Sasa waambie waliokutuma tunataka stendi nyingine kubwa kabisa ya mabasi hapo Urafiki/Shekilango serikali ilipopanunua. Serikali itakapoanza kupaendeleza wajenge majengo ya maghrofa 30 halafu chini kwenye basements tunataka stendi kubwa zaidi ya ilivyokuwa ubungo.
Haya ndo mawazo ya kujenga na si kugoma. Kugoma ni njia ya mwsho kabisa kama malalamiko yako hayajafanyiwa kazi kwa muda mrefu.
 

Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa mabasi angeivimbia serikali namna hiii?

Halafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa maslahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayohitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John Pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Kama wanaona biashara haiendi si wafunge biashara! Kuna mtu anawalazimisha kuendelea na bishara?
 
Kuna gari hailipi ushuru pale Mbezi?
Ajira gani iliyopotezwa ?

Au ndio nyie wauzaji wa bidhaa?
Ushuru mabasi yote yanalipa Vizuri tu wa kuingia na kutoka wawe wanaingia au hawaingii ushuru wao wa stendi Wenye mabasi walushalipa hao vibaka wataka mabasi lazima yaingie wao ni nani na inawahusu Nini wakati Wenye mabasi walishalipa ushuru wao wa kuingia na kutoka Kila basi wao ni LATRA au wamiliki wa stendi?
Huwezi lazimisha mteja aje haipo aninue chips mayai au majinya kunywa haipo hiyo
 
Na mwenye bus anawajibika kwa waliompa leseni ya biashara!! Complain zozote abiria fikisha kwa wasimamizi (LATRA) na si kuwatumia wamiliki wa mabasi. Mbona zikitokea ajali wa kulalamikiwa ni latra eti hawadhibiti makosa ya waendesha mabasi
Na LATRA wameruhusu stendi Shekilango na urafiki etc. Hivyo wamiliki wanafuata utaratibu.
 
Naongea km afisa wa mipango miji.

Umbali kutoka Stendi ya Moshi vijijini(Himo) to Moshi ni 35 Km
Umbali kutoka Bunju wilaya ya Kinondoni to Wilaya ya ubungo Mbezi luis stendi ni 33km.

Kutoka Mbagala kongowe wilaya ya temeke to Mbezi luis wilaya ya ubungo ni 35km
Kutoka Moshi mjini to Hai(boma ng'ombe stendi) 50km

Kuna magari yanaanzia wilayani pasipo kupitia makao makuu ya mkoa na moja kwa moja yanaenda mikoa au wilaya zingine.
 
kurasa zote nimesoma sijaona aliyeongelea sababu za mabasi kukwepa stendi ya mkoa
Mabasi yote yanayopita Morogoro road yanaingia stand ya mkoa, ishu n kwamba mabus yameamua kuangalia biashara zaidi na kumpa unafuu abiria.
Ww upo bunju na kuna bus lipo bunju, kwahy utaenda stand kuchukua bus lngin wakati tayar eneo lako kuna bus?
 
Imejengwa kwa mikopo yenye riba nafuu siyo pesa zako. Tunasubiri ushuke pale tupate kodi tukalipe deni. Nafananisha ndege na bus kwa kuwa vyote vina vituo maalumu vya kupakia na kushusha, hata hiace zina vituo maalumu vya kupakia na kushusha. Bus zingekuwa na msaada huo zisingelalamika kuomba kupandisha nauli, mafuta yakishuka mbona hawaombi kushusha nauli?? Ni uhuni tu.
Kumbe shida yako ni nauli.
 
Na LATRA wameruhusu stendi Shekilango na urafiki etc. Hivyo wamiliki wanafuata utaratibu.
Sahihi na LATRA Kuna wasomi na wako vizuri na wako sahihi

Hawawezi ingiliwa na wajinga machinga wa stendi ya Magufuli na vibaraka wao wanasiasa uchwara

LATRA,ni wataalamu wanasiasa uchwara wakae mbali waheshimu utaalamu

LATRA,Iko vizuri Tena mno wanasiasa uchwara tafadhali wakae mbali na utaalamu

Utaalamu uheshimiwe please
 
Back
Top Bottom