Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Nimekuuliza kuna heritage gani Kariakoo au zile nyumba nyingine zina nyufa, rangi imepauka, zimekarabatiwa zimerudiwa simenti, zinavuja mvua ikinyesha na mifumo ya umeme inasumbua ndio unaita heritage. Vitu vichafu ndio unataka viwe heritage.

Heritages za Dar zilijulikana vitu kama msikiti wa Kwamtoro, ikulu ya Magogoni, ukumbi wa Anatouglou, Karimjee na vitu kama hivyo. Sio fremu za maduka zilizochakaa. Yakibomoka au yakiungua watayaacha magofu?
Heritage sio majengo tu, ata characteristics za eneo husika.

Street market market ni character kama ni popular basi worth protecting.

Hakuna jengo lisilo succumb to elements overtime. Hayo majengo yote unayoyajua wewe ni maarufu duniani au maeneo yote ambayo mandarin yake inalindwa yanafanyiwa cosmetics upgrade ili yaendelee kuwepo. Sasa sio lazima kitu kinachohitaji upgrade tu kivunjwe.

Notredome Cathedral bado ipo kwenye matengenezo kwa sababu iliungua, Big Ben imeshakutana na misuko suko ya kila aina; hata nyuma za kawaida tu huko kwa wenzetu kama ni Tudor listed (iliyojengwa zama hizo) uruhusiwi kuondoa thatched roof wala kubadili structure. Wewe eneo pekee tu maarufu uoni umuhimu wa kulinda characteristics zake libakize umaarufu wake.
 
Kama mkataba unaeleza hivyo, itabidi waharakishiwe malipo yao kabla hawajaondoka.
Ata mkataba usiposema hivyo watawalipa.

Mkataba wa kibiashara pia una implied terms (vitu ambavyo havipo kwenye mkataba) mfano tamaduni za ufanyaji mambo katika sector husika hayo mambo ata yasipoandikwa kwenye mkataba mahakama inayatambua kama sehemu ya mkataba na ni legal binding terms.

Unapompangisha biashara eneo na yeye akatumia huo mkataba kuchukua mikopo kwa sababu ya hiyo biashara huku akielewa ana eneo la biashara, akaenda kununua inventory kubwa kwa sababu anaelewa hapo anawateja. Siku ukikurupukaa ukauvunja wakati mtu katengeneza madeni kwa sababu ya huo mkataba utalipa fidia ata kama hilo jambo halipo kwenye mkataba. Zinaitwa ‘contract implied terms’; customary ni moja wapo ambayo wataitumia huko mahakamani kuangalia taratibu za biashara zilivyo pia.
 
Fupa hili.

Baaaandariiiiiii Kamata hao shiiikaaaaa haoooo

Wafanyakazi wa Kariakoo wanajiweza na walishaonyesha Uwezo wao wa kukabiliana na nderemo za Sirikali.....Waendelee kupambana!

Naipenda Dar-Es-Salaam kaza buuuuuti kamata haooooo

Chagua kwa Uangalifu 2025
 
Huu ni ujinga tunataka kuuendekeza, wakisikilizwa, tutasafiri nchi mzima kuhamasisha yeyote mwenye kioengele na serikali aombe raisi aingilie Kati,

Huu utakuwa utoto wa hali juu, nchi imekuwa kama kikundi Cha walevi ngomani, kila mtu anaamua achezeje. Kila mtu Raisi aingilie kati, na haya unayasikia tunapokaribia uchaguzi... Hebu tuache upuuzi kama watanzania. Ni swala la kukemewa kabisa na kila mwenye akili timamu
 
Unaweza kuelezea makusanyo ya sasa ya NHC kwenye hayo majengo kupitia kodi ya pango. Na watakachopata baada ya hapo.

Si ajabu mradi wenyewe wakishavunja hayo maeneo mwekezaji ana miaka 20 ya kurudisha hela zake kabla ya NHC kupata chochote sasa hapo kuna faida gani ya serikali.

Hizi ndio baadhi ya PPP zenyewe ni ufisadi mtupu wa kuchukua prime areas kirahisi kwa uongo wa uwekezaji.

Halafu taasisi ambayo inadaiwa karibu tsh 2 trillion inaweza afford kupoteza mapato yake kishamba; baadae huo mzigo wamrushie mlipa kodi.
Ushakopa kujenga Jenga lako kiongozi?!

Unajua inachukua muda gani kuservice mortgage hata ya Milioni 100 tu kwa mwenye kipato cha mshahara wa walau mil.2 kwa mwezi?!

Tusipende kubeza kila kitu, unadhani NHC aachiwe miaka mingapi ili aweze kupata fedha ya kutosha kujenga Kariakoo, Mburahati, Mwenge, Tegeta, Posta, wakati huo huo akajenge na Mbarali, Ludewa, Njombe, Kahama, Ngara nk?!

Tuwaheshimu sana, na kamwe tusiamini kuwa wao ni wajinga mno, kiasi hicho kwamba hata yote tunayoyaona sisi humu wao hawaoni hata Moja. Often hatuna ukweli wote mezani, taarifa tunafanikiwa kuzipata hazitoshi kutusaidia kufanya au kupima usahihi wa maamuzi yanayofanyika.

Let's be Humble...hata katika kukosoa..lazima tukubali hatujui kila kitu.
 
Kuna commitments pia ambazo mtu ameingia kwenye biashara kwa sababu yakuelewa ana mkataba wa eneo la biashara. Sasa unapofupisha huo mkataba utalipa hizo hasara zake na fidia za loss of income for sizeable time.
Jibu swali siku 90 siku chache?
 
Wafanyabiashara wa maduka kutoka soko la Kariakoo wamefika makao makuu na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupinga notice walizopewa na shirika hilo kwa kuwataka kuhama ndani ya siku 90 kupisha mwekezaji mpya katika eneo hilo.

Wafanyabiashara hao wamesema, wao hawapingi maendeleo lakini muda uliotolewa na NHC ni mfupi sana na wamemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati sakata hilo ili waweze kupata haki yao kwani muda waliopewa ni mfupi sana kwa wao kuhama kutokana wao kuwa na madeni na mikopo.

====

View attachment 2657014
NOTISI YA SIKU TISINI (90) YA KUSITISHA MKATABA WA UPANGAJI WA NYUMBA NA 005 KWENYE KIWANJA NA 23 KITALU NA 31 MTAA WA TANDAMTI NA SWAHILI

Tafadhali husika na somo hapo juu;

Unafahamishwa kuwa Shirika la Nyumba la Taifa limeanza rasmi utekelezaji wa Sera va Ubia na wawekezaji binafsi na taasisi mbalimbali ambayo ilizinduliwa rasmi mwezi Novemba 2022.

Hivyo basi Shirika la Nyumba la Taifa lina mpango wa kuanza ujenzi kwenye Kiwanja tajwa hapo juu ambapo wewe ni mpangaji, hivyo tunakutaarifu kwamba unapewa NOTISI ya siku tisini (90) kuanzia tarche 02/06/2023 mpaka tarehe 31/08/2023 kusitisha mkataba baina yako na Shirika la Nyumba la Taifa kwenye nyumba tajwa hapo juu.

Shirika limerejea kipengele namba 4.1 (c). (d) na 7.2 cha Mkataba wa Upangaji kinachompa mamlaka mpangishaji kuvunja mkataba ndani ya siku tisini (90) pale anapohitaji jengo lake kwa ajili ya matumizi mengine.

Kwa maelezo hayo, unapewa NOTISI ya siku tisini (90) ya kutakiwa kuhama katika nyumba unavoishi ili kupisha uendelezaji unaokusudiwa kufanyika katika kiwanja hicho.

Unaruhusiwa kuomba upangaji upya baada ya jengo jipya kukamilika kulingana na masharti ya kipindi hicho.

Pia soma: Wapangaji nyumba za NHC Kariakoo walalamika notisi za kuhama bila mazungumzo, wadai NHC wamempa dili mwekezaji mpya kimyakimya
Kwenye mikataba yao waliyoisaini hakukua na hicho kipengele kilichorejelewa?
 
Ushakopa kujenga Jenga lako kiongozi?!

Unajua inachukua muda gani kuservice mortgage hata ya Milioni 100 tu kwa mwenye kipato cha mshahara wa walau mil.2 kwa mwezi?!

Tusipende kubeza kila kitu, unadhani NHC aachiwe miaka mingapi ili aweze kupata fedha ya kutosha kujenga Kariakoo, Mburahati, Mwenge, Tegeta, Posta, wakati huo huo akajenge na Mbarali, Ludewa, Njombe, Kahama, Ngara nk?!

Tuwaheshimu sana, na kamwe tusiamini kuwa wao ni wajinga mno, kiasi hicho kwamba hata yote tunayoyaona sisi humu wao hawaoni hata Moja. Often hatuna ukweli wote mezani, taarifa tunafanikiwa kuzipata hazitoshi kutusaidia kufanya au kupima usahihi wa maamuzi yanayofanyika.

Let's be Humble...hata katika kukosoa..lazima tukubali hatujui kila kitu.
Kwa post uliyo quote ulitakiwa kujustify sababu kuacha hela rahisi kutoka kwenye hizo cashcows ambazo zipo tayari na nini watakachopata kwenye ubia; hiyo ndio concern.

Halafu ni kwa sababu ni shirika la serikali muhimu pia kuonyesha social benefits za kufanya hivyo.

Vinginevyo hawa ni watu ambao washavunja majengo kadhaa ambayo kwa mwaka yalikuwa na uwezo wakuingiza mapato ya billion mpaka tatu.

Baada ya kuvunja hayo majengo miaka sita saba sasa na kuyaacha hayo maeneo hakuna kitu na kupoteza mapato karibu ya tsh 12 billion over the years. Wakati huo huo wanamadeni ya karibu tsh 1.5 ambayo awawezi gharamia yote kwa sababu ya mapato yao hafifu. Kwakuwa hayo madeni yana government guarantee inabidi walipa kodi wayalipe.

Leo wanaenda vunja maeneo mengine ambayo pengine combined income ni tsh 5 billion kwa mwaka. Kwa PPP ya miaka 20 bila ya kupata chochote, ndani ya muda huo wanapoteza tsh 100 billion potential income ambayo ilikuwepo.

Ni watu wanae-mu-enjoy huyu mama na hadithi zao ambazo hazina kichwa wala miguu; uwekezaji wa hasara halafu wana madeni ambayo awawezi lipa kwa uwekezaji mmbovu, bado wanaruhusiwa kupoteza mapato kishamba.

Binafsi biashara yoyote ya serikali itakayo binafsishwa provided nchi inapata good terms it’s about time; hakuna kitu wanaweza simamia huko serikalini.
 
Ni kweli lazima tuangalie namna gani tutapata faida, na ikiwa faida inayopatikana, ukiweka gharama za usumbufu, muda tutakaokaa bila kuingiza chochote kupisha ujenzi na gharama nyingine zote ni lazima ziwe pungufu ya faida tutakayoipata katika kipindi cha muda mfupi wa kati na mrefu ili mradi uwe wenye tija.

Ila ni ukweli ambao haupingiki, maiengo mengi ya NHC ni urithi wa Msajili. Kati ya hayo mengi yanahitaji mapitio na maboresho; miundombinu ya maji na umeme katika majengo haya imepitwa na wakati au imeharibika vibaya.. na mengine ubora wa jengo lenyewe umefikia mwisho, yaani yamezeeka. Na ndio maana Hata NHC haiwekezi fedha nyingi kwenye majengo hayo.

Nadhani ni kipindi cha Mzee Magufuli yalifanyiwa mapitio na shirika na mengi yakawekwa sokoni kwa utaratibu wa PPP. Kwa hiyo swala hili liko justified kabisa. Mengi ukiyapima kwa usalama sio salama kwa matumizi kabisa.. especially kwa matumizi ya familia nyingi au hata maduka na biashare nyingine nyingi zilizovamia majengo ambayo mengi were built for residential uses.

Lakini case ninayojaribu kuijengea hoja ni, je ni sahihi, Mtu kupewa notisi ya siku 90 na akatae kwa kisingizo cha kuwa na mkopo benki?! Je miezi mitatu(3) kuhamisha duka ni kazi ngumu sana, au?! Na tamko la kisiasa tukiruhusu likiangia hapa, je ni wapi we will draw a line?! Ni wapi tutasema hapa Rais Asiingilie kati?!
 
Yawezekana wakawa Wana HOJA lakini huwezi goma kuhama kwenye nyumba isiyo Yako.

Utatolewa kwa nguvu na aibu.

Hata lile soko walikuwa wengi sana kuwahanisha wangeleta kelele wakaona walitie kiberiti, an easy way to Deal with humans.

Wahame kabla hawajala hasara kubwa
 
Kuna sehemu nyingi za kujenga majengo ya kisasa na mazuri.

Kuna video nimeitafuta ya muda sijaipata wale wazungu walioenda tembelea kariakoo na kuporwa. Hiyo sio sehemu salama kwa sasa.

Lakini ikiboreshwa kwenye ulinzi hivyo hivyo ni kitengo cha utalii. Hawa wageni hawana shida ya kwenda malls kwao zipo za kumwaga kila kona. Ila street markets ni sehemu ya utalii sehemu kubwa duniani pia.

Sio kila kitu lazima ukibadili, halafu msukumo wa NHC ni kwa sababu ya eneo kuwa prime areas; lakini hawajali historia ya sehemu kubaki kama ilivyo.

Forodhani Zanzibar zamani ilikuwa ya wenyeji tu, sasa ni moja ya sehemu must see kwa watalii.

Embu tuache huu ushamba wa kuona eneo likiwa na maslahi tu basi livunjwe.
Kwa hio Majengo ya NHC makuuu kuu toka mwaka 50 yaachwe, Jengo lina Frame 3 liachwe wakati linaweza bomolewa na kuwekwa Frame 72 na Appaetment 40? Zitakazoingiza Takriban Bilioni kwa mwaka badala ya milioni 2?

Kama huoni hii opportunity Kariakoo haikuhusu, ni eneo la Biashara lile wanatakiwa watu wanaofikiria kibiashara ndio wafanye Decisions, hata hao wanaolalamika kutolewa wanaomba tu Extension ya Muda kuonesha na wao wanafikiri kibiashara.

Na biashara haifati majengo kamwe, Majengo ndio hufuata biashara, mpaka kesho Machinga Complex pamedoda, unafikiri Serikali ikijenga majengo Nje ya Kkoo basi kutachangamka na kua na Biashara?
 
Ni kweli lazima tuangalie namna gani tutapata faida, na ikiwa faida inayopatikana, ukiweka gharama za usumbufu, muda tutakaokaa bila kuingiza chochote kupisha ujenzi na gharama nyingine zote ni lazima ziwe pungufu ya faida tutakayoipata katika kipindi cha muda mfupi wa kati na mrefu ili mradi uwe wenye tija.

Ila ni ukweli ambao haupingiki, maiengo mengi ya NHC ni urithi wa Msajili. Kati ya hayo mengi yanahitaji mapitio na maboresho; miundombinu ya maji na umeme katika majengo haya imepitwa na wakati au imeharibika vibaya.. na mengine ubora wa jengo lenyewe umefikia mwisho, yaani yamezeeka. Na ndio maana Hata NHC haiwekezi fedha nyingi kwenye majengo hayo.

Nadhani ni kipindi cha Mzee Magufuli yalifanyiwa mapitio na shirika na mengi yakawekwa sokoni kwa utaratibu wa PPP. Kwa hiyo swala hili liko justified kabisa. Mengi ukiyapima kwa usalama sio salama kwa matumizi kabisa.. especially kwa matumizi ya familia nyingi au hata maduka na biashare nyingine nyingi zilizovamia majengo ambayo mengi were built for residential uses.

Lakini case ninayojaribu kuijengea hoja ni, je ni sahihi, Mtu kupewa notisi ya siku 90 na akatae kwa kisingizo cha kuwa na mkopo benki?! Je miezi mitatu(3) kuhamisha duka ni kazi ngumu sana, au?! Na tamko la kisiasa tukiruhusu likiangia hapa, je ni wapi we will draw a line?! Ni wapi tutasema hapa Rais Asiingilie kati?!
Listen I am not against kuamisha watu kabisa.

Lakini watu kama wanaona kuna ulazima wa kufanya hivyo wafanye responsibly.

Uwezi kuwapa watu notice ya three month ambayo maisha yote wameishi eneo moja. Ipo hivyo duniani kote kwenye nyumba za serikali.

Ndio maana utaratibu ni huwa kujenga nyumba mpya kwanza ata huko swekeni; halafu unampa mtu option ya kuamia huko au unachukua nyumba yako.

Pili watu huwa wanatoa compensation ukitaka kuhama tunakulipa kiasi kadhaa ukakodi na kufidia investment zako au tunakupa miezi kadhaa rent free ujipange. Hao ni kwa residential tenants.

Lakini kutoa wafanyabiashara is a different ball game, kwa sababu kuna loss of business income akipoteza huo mkataba; so watafidiwa tu wakienda mahakamani.

Kwa sababu ata huyo bank manager akiitwa kama shahidi atakwambia kama hiyo biashara baada ya mwaka tungejua itaamishwa tusingewapa mkopo wa miaka minne. Bado huyo mkopaji pengine kaweka nyumba dhamana kupata mkopo so s/he has a lot loose.

Hapo anachohitajika ni mwanasheria mzuri tu wa mikataba ya kibiashara kwa muda huo waliowapa NHC watalipa tu compensation.
 
Nilipoona mzanzibar anakuwa.DG wa NHC.Halafu mtu anatoka kuongoza NGO ndogo tu eti anakuja kuongoza NHC.Mwarabu atapewa.hivyo viwanja. YAANI MAGUFULI MTANGANYIKA TUTAKUKUMBUKA.TUNAKUKUMBUKA.

nikuulize nyumba za NHC zilikuwa za watu gani? na nani alifanya dhambi ya kuwadhulumu ? waulize NHC hizo jyumba zote wanazomiliki walizijenga wao? kama huna jibu nakupa jibu ukae ukijua, nyumba za NHC zilijengwa na wahindi miaka 1914 na nyingine zimejengwa kabla ya miaka hiyo,hakuna nyumba hata moja NHC walijenga, aliyefanya dhambi ya kudhulumu nyumba hizo ni NYERERE, akawakabidhi NHC akuwadhulumu waafrica bali aliwanyag'anya wahindi kwa nguvu ni hii ndio dhambi ya dhuluma inaitafuna tanzania
 
Kwa hio Majengo ya NHC makuuu kuu toka mwaka 50 yaachwe, Jengo lina Frame 3 liachwe wakati linaweza bomolewa na kuwekwa Frame 72 na Appaetment 40? Zitakazoingiza Takriban Bilioni kwa mwaka badala ya milioni 2?

Kama huoni hii opportunity Kariakoo haikuhusu, ni eneo la Biashara lile wanatakiwa watu wanaofikiria kibiashara ndio wafanye Decisions, hata hao wanaolalamika kutolewa wanaomba tu Extension ya Muda kuonesha na wao wanafikiri kibiashara.

Na biashara haifati majengo kamwe, Majengo ndio hufuata biashara, mpaka kesho Machinga Complex pamedoda, unafikiri Serikali ikijenga majengo Nje ya Kkoo basi kutachangamka na kua na Biashara?
Sasa unaweza shangaa hiyo machinga complex hawa wakiamia huko pakachangamka shopping ni habit.

Kuna watu wanapendelea kufanya manunuzi yao katika mazingira tofauti. Ukiangusha shopping mall wanatafuta street market nyingine na kukuacha udode na mjengo wako wa kisasa.
 
Listen I am not against kuamisha watu kabisa.

Lakini watu kama wanaona kuna ulazima wa kufanya hivyo wafanye responsibly.

Uwezi kuwapa watu notice ya three month ambayo maisha yote wameishi eneo moja. Ipo hivyo duniani kote kwenye nyumba za serikali.

Ndio maana utaratibu ni huwa kujenga nyumba mpya kwanza ata huko swekeni; halafu unampa mtu option ya kuamia huko au unachukua nyumba yako.

Pili watu huwa wanatoa compensation ukitaka kuhama tunakulipa kiasi kadhaa ukakodi na kufidia investment zako au tunakupa miezi kadhaa rent free ujipange. Hao ni kwa residential tenants.

Lakini kutoa wafanyabiashara is a different ball game, kwa sababu kuna loss of business income akipoteza huo mkataba; so watafidiwa tu wakienda mahakamani.

Kwa sababu ata huyo bank manager akiitwa kama shahidi atakwambia kama hiyo biashara baada ya mwaka tungejua itaamishwa tusingewapa mkopo wa miaka minne. Bado huyo mkopaji pengine kaweka nyumba dhamana kupata mkopo so s/he has a lot loose.

Hapo anachohitajika ni mwanasheria mzuri tu wa mikataba ya kibiashara kwa muda huo waliowapa NHC watalipa tu compensation.
Yawezekana ni Mimi sijui, ila ukweli ni kuwa 90 days is way overdue... Huko kwingine unakokusema hakuna mahali wazaidisha 60 days.

Pili NHC ni landlord kama wewe na Mimi tunapopangisha ndio maana anakwenda kwa kufuata sheria, Swala la biashara yako na wewe kukaa sana kwangu havina uhusiano na property yangu, ndio maana makampuni makubwa yanajenga ofisi au yanaingia kwenye makubaliano ya long term lease.

Yaani unilipe kila mwezi halafu uniambie nikikutoa nakuharibia biashara, ungejua Hilo ungekuja mezani ukaniambia nataka kukaa hapa at least kwa miaka 10 ningekupa my stance, pay me this much au hapana tafuta kwingine natarajia.kuvunja in 6 years.

Shida yetu tunapenda sana kuoperate kila kitu kwa the exception rule. Hapana sio sahihi.
 
Sasa unaweza shangaa hiyo machinga complex hawa wakiamia huko pakachangamka shopping ni habit.

Kuna watu wanapendelea kufanya manunuzi yao katika mazingira tofauti. Ukiangusha shopping mall wanatafuta street market nyingine na kukuacha udode na mjengo wako wa kisasa.
Tanzania Hatuna Mitaji watu wanapiga winga, hawakai kwengine tofauti na mapapa wa kkoo walipo.
 
Back
Top Bottom