Hornet
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 26,486
- 51,156
Sasa kodi walilipa kwa nani?
Au ndo wanaotembeza vinote kuwa washalipa?
Maana hadi maeneo ya Fire wameambiwa wasilipe kodi wajiandae
Soma polepole
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa kodi walilipa kwa nani?
Au ndo wanaotembeza vinote kuwa washalipa?
Maana hadi maeneo ya Fire wameambiwa wasilipe kodi wajiandae
Heritage sio majengo tu, ata characteristics za eneo husika.Nimekuuliza kuna heritage gani Kariakoo au zile nyumba nyingine zina nyufa, rangi imepauka, zimekarabatiwa zimerudiwa simenti, zinavuja mvua ikinyesha na mifumo ya umeme inasumbua ndio unaita heritage. Vitu vichafu ndio unataka viwe heritage.
Heritages za Dar zilijulikana vitu kama msikiti wa Kwamtoro, ikulu ya Magogoni, ukumbi wa Anatouglou, Karimjee na vitu kama hivyo. Sio fremu za maduka zilizochakaa. Yakibomoka au yakiungua watayaacha magofu?
Ata mkataba usiposema hivyo watawalipa.Kama mkataba unaeleza hivyo, itabidi waharakishiwe malipo yao kabla hawajaondoka.
Kuna commitments pia ambazo mtu ameingia kwenye biashara kwa sababu yakuelewa ana mkataba wa eneo la biashara. Sasa unapofupisha huo mkataba utalipa hizo hasara zake na fidia za loss of income for sizeable time.Haraka siku 90?
Ushakopa kujenga Jenga lako kiongozi?!Unaweza kuelezea makusanyo ya sasa ya NHC kwenye hayo majengo kupitia kodi ya pango. Na watakachopata baada ya hapo.
Si ajabu mradi wenyewe wakishavunja hayo maeneo mwekezaji ana miaka 20 ya kurudisha hela zake kabla ya NHC kupata chochote sasa hapo kuna faida gani ya serikali.
Hizi ndio baadhi ya PPP zenyewe ni ufisadi mtupu wa kuchukua prime areas kirahisi kwa uongo wa uwekezaji.
Halafu taasisi ambayo inadaiwa karibu tsh 2 trillion inaweza afford kupoteza mapato yake kishamba; baadae huo mzigo wamrushie mlipa kodi.
Jibu swali siku 90 siku chache?Kuna commitments pia ambazo mtu ameingia kwenye biashara kwa sababu yakuelewa ana mkataba wa eneo la biashara. Sasa unapofupisha huo mkataba utalipa hizo hasara zake na fidia za loss of income for sizeable time.
Kwenye mikataba yao waliyoisaini hakukua na hicho kipengele kilichorejelewa?Wafanyabiashara wa maduka kutoka soko la Kariakoo wamefika makao makuu na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupinga notice walizopewa na shirika hilo kwa kuwataka kuhama ndani ya siku 90 kupisha mwekezaji mpya katika eneo hilo.
Wafanyabiashara hao wamesema, wao hawapingi maendeleo lakini muda uliotolewa na NHC ni mfupi sana na wamemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati sakata hilo ili waweze kupata haki yao kwani muda waliopewa ni mfupi sana kwa wao kuhama kutokana wao kuwa na madeni na mikopo.
====
View attachment 2657014
NOTISI YA SIKU TISINI (90) YA KUSITISHA MKATABA WA UPANGAJI WA NYUMBA NA 005 KWENYE KIWANJA NA 23 KITALU NA 31 MTAA WA TANDAMTI NA SWAHILI
Tafadhali husika na somo hapo juu;
Unafahamishwa kuwa Shirika la Nyumba la Taifa limeanza rasmi utekelezaji wa Sera va Ubia na wawekezaji binafsi na taasisi mbalimbali ambayo ilizinduliwa rasmi mwezi Novemba 2022.
Hivyo basi Shirika la Nyumba la Taifa lina mpango wa kuanza ujenzi kwenye Kiwanja tajwa hapo juu ambapo wewe ni mpangaji, hivyo tunakutaarifu kwamba unapewa NOTISI ya siku tisini (90) kuanzia tarche 02/06/2023 mpaka tarehe 31/08/2023 kusitisha mkataba baina yako na Shirika la Nyumba la Taifa kwenye nyumba tajwa hapo juu.
Shirika limerejea kipengele namba 4.1 (c). (d) na 7.2 cha Mkataba wa Upangaji kinachompa mamlaka mpangishaji kuvunja mkataba ndani ya siku tisini (90) pale anapohitaji jengo lake kwa ajili ya matumizi mengine.
Kwa maelezo hayo, unapewa NOTISI ya siku tisini (90) ya kutakiwa kuhama katika nyumba unavoishi ili kupisha uendelezaji unaokusudiwa kufanyika katika kiwanja hicho.
Unaruhusiwa kuomba upangaji upya baada ya jengo jipya kukamilika kulingana na masharti ya kipindi hicho.
Pia soma: Wapangaji nyumba za NHC Kariakoo walalamika notisi za kuhama bila mazungumzo, wadai NHC wamempa dili mwekezaji mpya kimyakimya
Kwa post uliyo quote ulitakiwa kujustify sababu kuacha hela rahisi kutoka kwenye hizo cashcows ambazo zipo tayari na nini watakachopata kwenye ubia; hiyo ndio concern.Ushakopa kujenga Jenga lako kiongozi?!
Unajua inachukua muda gani kuservice mortgage hata ya Milioni 100 tu kwa mwenye kipato cha mshahara wa walau mil.2 kwa mwezi?!
Tusipende kubeza kila kitu, unadhani NHC aachiwe miaka mingapi ili aweze kupata fedha ya kutosha kujenga Kariakoo, Mburahati, Mwenge, Tegeta, Posta, wakati huo huo akajenge na Mbarali, Ludewa, Njombe, Kahama, Ngara nk?!
Tuwaheshimu sana, na kamwe tusiamini kuwa wao ni wajinga mno, kiasi hicho kwamba hata yote tunayoyaona sisi humu wao hawaoni hata Moja. Often hatuna ukweli wote mezani, taarifa tunafanikiwa kuzipata hazitoshi kutusaidia kufanya au kupima usahihi wa maamuzi yanayofanyika.
Let's be Humble...hata katika kukosoa..lazima tukubali hatujui kila kitu.
Hivi wewe kama umechukua deni la tsh billion moja kwa miaka miwili; halafu mtu anakupa miezi mitatu kufanya biashara huo muda unatosha.Jibu swali siku 90 siku chache?
Ni kweli lazima tuangalie namna gani tutapata faida, na ikiwa faida inayopatikana, ukiweka gharama za usumbufu, muda tutakaokaa bila kuingiza chochote kupisha ujenzi na gharama nyingine zote ni lazima ziwe pungufu ya faida tutakayoipata katika kipindi cha muda mfupi wa kati na mrefu ili mradi uwe wenye tija.Kwa post uliyo quote ulitakiwa kujustify sababu kuacha hela rahisi kutoka kwenye hizo cashcows ambazo zipo tayari na nini watakachopata kwenye ubia; hiyo ndio concern.
Halafu ni kwa sababu ni shirika la serikali muhimu pia kuonyesha social benefits za kufanya hivyo.
Vinginevyo hawa ni watu ambao washavunja majengo kadhaa ambayo kwa mwaka yalikuwa na uwezo wakuingiza mapato ya billion mpaka tatu.
Baada ya kuvunja hayo majengo miaka sita saba sasa na kuyaacha hayo maeneo hakuna kitu na kupoteza mapato karibu ya tsh 12 billion over the years. Wakati huo huo wanamadeni ya karibu tsh 1.5 ambayo awawezi gharamia yote kwa sababu ya mapato yao hafifu. Kwakuwa hayo madeni yana government guarantee inabidi walipa kodi wayalipe.
Leo wanaenda vunja maeneo mengine ambayo pengine combined income ni tsh 5 billion kwa mwaka. Kwa PPP ya miaka 20 bila ya kupata chochote, ndani ya muda huo wanapoteza tsh 100 billion potential income ambayo ilikuwepo.
Ni watu wanae-mu-enjoy huyu mama na hadithi zao ambazo hazina kichwa wala miguu; uwekezaji wa hasara halafu wana madeni ambayo awawezi lipa kwa uwekezaji mmbovu, bado wanaruhusiwa kupoteza mapato kishamba.
Binafsi biashara yoyote ya serikali itakayo binafsishwa provided nchi inapata good terms it’s about time; hakuna kitu wanaweza simamia huko serikalini.
Kwani kuna mtu kakatazwa kufanya biashara?Hivi wewe kama umechukua deni la tsh billion moja kwa miaka miwili; halafu mtu anakupa miezi mitatu kufanya biashara huo muda unatosha.
Mbona mna maswali ya kitoto.
Kwa hio Majengo ya NHC makuuu kuu toka mwaka 50 yaachwe, Jengo lina Frame 3 liachwe wakati linaweza bomolewa na kuwekwa Frame 72 na Appaetment 40? Zitakazoingiza Takriban Bilioni kwa mwaka badala ya milioni 2?Kuna sehemu nyingi za kujenga majengo ya kisasa na mazuri.
Kuna video nimeitafuta ya muda sijaipata wale wazungu walioenda tembelea kariakoo na kuporwa. Hiyo sio sehemu salama kwa sasa.
Lakini ikiboreshwa kwenye ulinzi hivyo hivyo ni kitengo cha utalii. Hawa wageni hawana shida ya kwenda malls kwao zipo za kumwaga kila kona. Ila street markets ni sehemu ya utalii sehemu kubwa duniani pia.
Sio kila kitu lazima ukibadili, halafu msukumo wa NHC ni kwa sababu ya eneo kuwa prime areas; lakini hawajali historia ya sehemu kubaki kama ilivyo.
Forodhani Zanzibar zamani ilikuwa ya wenyeji tu, sasa ni moja ya sehemu must see kwa watalii.
Embu tuache huu ushamba wa kuona eneo likiwa na maslahi tu basi livunjwe.
Listen I am not against kuamisha watu kabisa.Ni kweli lazima tuangalie namna gani tutapata faida, na ikiwa faida inayopatikana, ukiweka gharama za usumbufu, muda tutakaokaa bila kuingiza chochote kupisha ujenzi na gharama nyingine zote ni lazima ziwe pungufu ya faida tutakayoipata katika kipindi cha muda mfupi wa kati na mrefu ili mradi uwe wenye tija.
Ila ni ukweli ambao haupingiki, maiengo mengi ya NHC ni urithi wa Msajili. Kati ya hayo mengi yanahitaji mapitio na maboresho; miundombinu ya maji na umeme katika majengo haya imepitwa na wakati au imeharibika vibaya.. na mengine ubora wa jengo lenyewe umefikia mwisho, yaani yamezeeka. Na ndio maana Hata NHC haiwekezi fedha nyingi kwenye majengo hayo.
Nadhani ni kipindi cha Mzee Magufuli yalifanyiwa mapitio na shirika na mengi yakawekwa sokoni kwa utaratibu wa PPP. Kwa hiyo swala hili liko justified kabisa. Mengi ukiyapima kwa usalama sio salama kwa matumizi kabisa.. especially kwa matumizi ya familia nyingi au hata maduka na biashare nyingine nyingi zilizovamia majengo ambayo mengi were built for residential uses.
Lakini case ninayojaribu kuijengea hoja ni, je ni sahihi, Mtu kupewa notisi ya siku 90 na akatae kwa kisingizo cha kuwa na mkopo benki?! Je miezi mitatu(3) kuhamisha duka ni kazi ngumu sana, au?! Na tamko la kisiasa tukiruhusu likiangia hapa, je ni wapi we will draw a line?! Ni wapi tutasema hapa Rais Asiingilie kati?!
Nilipoona mzanzibar anakuwa.DG wa NHC.Halafu mtu anatoka kuongoza NGO ndogo tu eti anakuja kuongoza NHC.Mwarabu atapewa.hivyo viwanja. YAANI MAGUFULI MTANGANYIKA TUTAKUKUMBUKA.TUNAKUKUMBUKA.
Sasa unaweza shangaa hiyo machinga complex hawa wakiamia huko pakachangamka shopping ni habit.Kwa hio Majengo ya NHC makuuu kuu toka mwaka 50 yaachwe, Jengo lina Frame 3 liachwe wakati linaweza bomolewa na kuwekwa Frame 72 na Appaetment 40? Zitakazoingiza Takriban Bilioni kwa mwaka badala ya milioni 2?
Kama huoni hii opportunity Kariakoo haikuhusu, ni eneo la Biashara lile wanatakiwa watu wanaofikiria kibiashara ndio wafanye Decisions, hata hao wanaolalamika kutolewa wanaomba tu Extension ya Muda kuonesha na wao wanafikiri kibiashara.
Na biashara haifati majengo kamwe, Majengo ndio hufuata biashara, mpaka kesho Machinga Complex pamedoda, unafikiri Serikali ikijenga majengo Nje ya Kkoo basi kutachangamka na kua na Biashara?
Yawezekana ni Mimi sijui, ila ukweli ni kuwa 90 days is way overdue... Huko kwingine unakokusema hakuna mahali wazaidisha 60 days.Listen I am not against kuamisha watu kabisa.
Lakini watu kama wanaona kuna ulazima wa kufanya hivyo wafanye responsibly.
Uwezi kuwapa watu notice ya three month ambayo maisha yote wameishi eneo moja. Ipo hivyo duniani kote kwenye nyumba za serikali.
Ndio maana utaratibu ni huwa kujenga nyumba mpya kwanza ata huko swekeni; halafu unampa mtu option ya kuamia huko au unachukua nyumba yako.
Pili watu huwa wanatoa compensation ukitaka kuhama tunakulipa kiasi kadhaa ukakodi na kufidia investment zako au tunakupa miezi kadhaa rent free ujipange. Hao ni kwa residential tenants.
Lakini kutoa wafanyabiashara is a different ball game, kwa sababu kuna loss of business income akipoteza huo mkataba; so watafidiwa tu wakienda mahakamani.
Kwa sababu ata huyo bank manager akiitwa kama shahidi atakwambia kama hiyo biashara baada ya mwaka tungejua itaamishwa tusingewapa mkopo wa miaka minne. Bado huyo mkopaji pengine kaweka nyumba dhamana kupata mkopo so s/he has a lot loose.
Hapo anachohitajika ni mwanasheria mzuri tu wa mikataba ya kibiashara kwa muda huo waliowapa NHC watalipa tu compensation.
Tanzania Hatuna Mitaji watu wanapiga winga, hawakai kwengine tofauti na mapapa wa kkoo walipo.Sasa unaweza shangaa hiyo machinga complex hawa wakiamia huko pakachangamka shopping ni habit.
Kuna watu wanapendelea kufanya manunuzi yao katika mazingira tofauti. Ukiangusha shopping mall wanatafuta street market nyingine na kukuacha udode na mjengo wako wa kisasa.