Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Haya hima hima tuliamshe tuliamshe dude. Hakuna kulala maisha haya, ni kusaka pesa tirelessly ili uzeeni our weekend starts on Monday. 😀 Luckily tushapata na mwenyeji huko mtz mwenzetu Danhappy... hopefully atatupa muongozo murua.

-Kaveli-
Sawa sawa mkuu na hivi vyuma vimekaza ni lazima kupambana.
 
Tafta hela uende china. Kuna masoko yao kule vitu bei cheap kweli. Kuna vijana walianza kdgo kdgo tu this day wanafanya vizuri kweli. Just know ur niche.

Vitu vingine in china the prices are lower kuliko hata hapo Kariakoo.
Sasa nauli tu ya kwenda kule si mtaji unaisha kabisa. Na mzigo unasafirishwaje sasa kuja Tz ? Vp ushuru pia?
 
Hongera aisee mana ni wagumu kusema hata uwachinje[emoji3][emoji3][emoji3]

Sent from my Fire2 3G using JamiiForums mobile app
[emoji1] [emoji1] Wabongo bhana, mi nilikuja Bongo kuchukua mitumba. Nilirudi na pesa zangu maana kila niliyekuwa namwambia shida yangu ya kupata chimbo anatabasamu kwanza akijesemea moyoni tayari nshapata dili.
 
Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!
Safi leo nina mteja wangu wa musoma ngoja niingie machimbo ya magaun maana kk wanatuuzia bei za juu kumbe ukiingia machimbo unakula faida safi sana.
 
[emoji1] [emoji1] Wabongo bhana. Mi nilikuja Bongo kuchukua mitumba. Nilirudi na pesa zangu maana kila niliyekuwa namwambia shida yangu ya kupata chimbo anatabasamu kwanza akijesemea moyoni tayar nshapata dili.
Sasa unadhani watakwambia halafu wakale wapi? Pia wenye mizigo wanataka madalali.
 
Nimekuja kugundua wenye mitaj midogo wanafaidika mana kwenda china tu mtaji huo
Nipe maelezo basi hapo,kwenda China tu ni mtaji imekaaje hiyo. Ukifika huko unaweza pata vibarua na kupata pesa za kununua mizigo?
 
Sasa nauli tu ya kwenda kule si mtaji unaisha kabisa. Na mzigo unasafirishwaje sasa kuja Tz ? Vp ushuru pia?

Kuna shipping agents wanaokutumia vitu vyako huku bongo na kukutolea bandarini (door to door)....Kama Silent Ocean na wengine.

Mzigo Unaulipia charges kwa cbm (cubic meters) inategemea na aina ha bidhaa hyo ina include shipping, agency na taxes. Ila kikubwa ukifika kule inakua na nguvu zaidi unaweza chagua bidhaa unayotaka hata ku negotiate price na wachina masokoni kwao face to face. The more unanunua mzigo kwingi the more discount u get hence the more profit u get ukija uza huku.

Ili umake good money kweli uone unapiga hela kweli uwe na kitu kama 10 M hivi hyo mzgo tu. (Unaweza ukaanza less than that ila mimi naona kuanzia 10 M kuendelea ndio kweli naweza nikasema huyu mtu ana make hela)
 
Mi kuna machinga nilikuwa nachukua mzigo kwake,hivyo nampa pesa ye anazunguka kwenda kuchukua mzigo.Ukimuuliza asemi,siku nilienda na vijana wangu watatu ambapo yeye hakuwaona.Hivyo nilivyomkabidhi pesa akaondoka,vijana wangu wakamfuatilia mpaka wakajua maduka yote aliyoingia.Tangia siku hiyo hajaniona na majamaa wa madukani washanizoea hats bila pesa wananipa mzigo au wanatuma mkoani.
Una akili sana mkuu
 
Back
Top Bottom