Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Mi kuna machinga nilikuwa nachukua mzigo kwake,hivyo nampa pesa ye anazunguka kwenda kuchukua mzigo.Ukimuuliza asemi,siku nilienda na vijana wangu watatu ambapo yeye hakuwaona.Hivyo nilivyomkabidhi pesa akaondoka,vijana wangu wakamfuatilia mpaka wakajua maduka yote aliyoingia.Tangia siku hiyo hajaniona na majamaa wa madukani washanizoea hats bila pesa wananipa mzigo au wanatuma mkoani.
Mkuu hii ulifanya ni intelligence ya hali ya juu sana.
 
Charity ahsante sana, majibu yako yametusaidia wengi, tutazama huko machimboni, tuanze mdogo mdogo hatimaye na sisi tuanze kwenda china, barikiwa sana, lkn pia mleta mada ubarikiwe tumejifunza mengi kupitia thread hii
 
Mi ninachokifanya naenda nai nafunga Mzigo wangu nikifika dukani nauza jumla na reja reja bei sawa na dar nahakikisha kila pc1 inatoa efu 4 na nasafari kila wiki kwa sehemu niliyopo nategemewa na wenye maduka na wanaouza kwa kutembeza muhimu fanya utafiti wa eneo ulilopo na kujua aina ya nguo zenye mzunguko mkubwa maana biashara si kupamba duka bali bidhaa zitoke.....
K/koo siku izi wanamix copy na og na wanakuuzia bei moja.. @honort hope nimekupa idea

Huko Nairobi nako mngetupa majina ya machimbo mngetusaidia zaidi sana
 
Nimepata maswali mengi pm nijibu tu hapa kwa faida ya wengi sababu wengi wao ni wanataka kuanza biashara

Aina ya biashara
Fanya utafiti juu ya biashara unayotaka kufanya like km uko dar tembelea maeneo hata hapo kkoo jifunze vitu vidogo mf unataka kuuza nguo za watoto ziko design nyingi kuna ronya quality kidogo, quality ya Kati na ile quality kabisa pita madukani jifanye kuuliza hata bei soma lebo baada ya muda utajua kutofautisha. hii itakusaidia unaponunua ununue bidhaa inayoenda na pesa na isikupe tabu katika soko lako.

Aina ya wateja
Chagua aina ya wateja wako like maskini, hali ya Kati au matajiri!! Hii itakusaidia kujua watu unaodeal nao na hapo juu umeshapita kuangalia quality na bei sababu kila bei na quality ya nguo ina kundi lake katika Jamii

Location
Location ni muhimu sababu kila kundi katika
Jamii linapatikana sehemu husika so chagua kundi linaloendana na mazingira husika.

Aina za nguo
Kuna aina nyingi za nguo unaweza chagua aina unayotaka Kama vile nguo za watoto kipato cha Kati, nguo za heshima kipato cha Kati, nguo za kimalaya kipato cha Kati... Hii itakusaidia kupata kundi moja kwa wakati mmoja na kwa bei zinazolingana ina maana mteja akija kwako hatoki kirahisi.

Anza biashara
Ukifanya hizo key point kiufasaha anza biashara yako hutapata shida yoyote.

Mtaji.
Wengi wameniuliza kuhusu mtaji sh ngapi
Kwa mie mtaji ni pesa yoyote uliyo nayo as long as unahitaji kuingia kwenye kufanya biashara na si kujaribu biashara.

Mf
Mi nilikosa mtaji kabisa ilikua mwaka 2013 Oct na nilianza na laki na nusu na mzigo wangu wa Kwanza kufunga hapo kkoo ilikua urembo cheni, hereni, bangili na lipsick na huo mzigo niliuza kwa kutembeza na ulizaa 375000 na kupitia huo mzigo nikipata oda nyingi sana za nguo... Kwa pesa hio hio ilinilazimu nitumie usafiri wa kutoka moja kati ya wilaya za mpkani mwa tz mpk dar

Hapo nimetoa mfano tu wa mliouliza kuhusu mtaji.. Anza na ulichonacho kwa mfanyabiashara hakuna hela ndogo.
Muhimu fanya utafiti hata kama umeelekezwa kabla ya kununua fanya utafiti wewe mwenyewe iwe kkoo,, Uganda au nairobi.

Kwa Wale mlioniuliza pm naona nimewajibu
wote kwani kujibu mmoja mmoja siwezi..
Dada samahn naomba namba yako.
 
Back
Top Bottom