Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Mwenyezi Mungu akuongezee charty.

Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah! .
 
Weye ni nomaa Mkuu ulitumia akili ya kuzaliwa kicomandoo commando.

Mi kuna machinga nilikuwa nachukua mzigo kwake,hivyo nampa pesa ye anazunguka kwenda kuchukua mzigo.Ukimuuliza asemi,siku nilienda na vijana wangu watatu ambapo yeye hakuwaona.Hivyo nilivyomkabidhi pesa akaondoka,vijana wangu wakamfuatilia mpaka wakajua maduka yote aliyoingia.Tangia siku hiyo hajaniona na majamaa wa madukani washanizoea hats bila pesa wananipa mzigo au wanatuma mkoani.
 
Dada charty nimefuata maelekezo yako yote nimeenda kwa wachina nimeshindwa kupata mzigo na cash ninayo naambiwa bei Amby sio kabixa naomb nisaidie plz najarb kukupm nimeshindwa naomb nicheki 0743668001
Its all about business Nina shida plz naomb msaada
 
Wakuu samahanin san <br />naomba mtu au watu amabo wanauzoefu na biashara ya vifaa vya simu(phone accessories) kutoka kenya au Zanzibar kwa bei ya jumla vifaa hvyo ni km vile mics,system chargers, screen touches, glass protectors, earphones, phone covers,chargers,USB cables,carbons, speakers, motherboard,memory cards, flash, battery, nk. nahitaji kujua bei ya jumla kwa hayo maeneo mawili(kenya na zanzibar) na wapi ni nafuu zaid na maeneo ambayo ni dominant kwa kuuza hvyo vifaa kwa bei ya jumla msaada plzzz wakuu<br /> cont: +255769939879<br />whatsapp na voice call online 24/7
 
Mwenye kujua chimbo la albam za picha plz anisaidie.
 
Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!
Pole, asante
 
Hahhahah sasa wewe mie mkali wa hizi kazi tokea nipo chuo kitamboo nimeivuruga sana hiyo k.koo hahah hadi leo nipo yaani na sibanduki ng'ooo inabidi tuwasaidie wenzetu bana maana haya maisha mtu akikuongezea jero kwenye product ni kubwa sanaaaa.Na hivi vyuma vimekaza acha tu na wenyewe wale.Ila si unajua mjini wasioujua bado wengi utawapata tu maana hawapo humu JF .

Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000,8000,12000 lipo maeneo ya nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee msimbazi kota,karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa congo na aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka congo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k,25k,28k,30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh,pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy
Charty bidhaa kama T-shirt za manga au hot basic kwa jumla bei simpo ninaweza kupata maeneo gani mkuu?

Nataka nipate mzigo then niziprint halafu niziingize sokoni..
Tatizo machimbo ya bei rahisi ndo siyafahamu..
Na jeans na raba Pia kama unafahasmu..
 
Karibuni ndugu zanguni,tupeane mbinu za kupata mzigo wa jumla kwa bei nafuu hapo kariakoo na kuonesha bei ya jumla binafsi nina mpango wa kuuza kwa mnada wa kutembeza kwa gari vitu kama vitenge,nguo za kiume,za kike,za watoto jinsia zote,viatu aina zote yebo yebo za watoto vingine nitaviacha dukani.

Tushauriane jinsi ya kupata mzigo nafuu nimejaribu kufika soko la manzese nimekuta viatu vya mtoto yebo nzuri kabisa sh 1000 wakati kariakoo 3500 sasa nimekuja mahali hapa nipate kujua za kupata mzigo mzuri kwa ujumla

Ahsante kwa kutoa muda wako

USHAURI;Tujitahidi kuwafata wateja mahali walipo kutatua shida zao wao watupe pesa

UKIPENDA PESA JUA NA KUZITAFUTA
 
Nasubiri maeneo ya nguo zote za mtumba na mazaga zaga yoteeeee
 
Back
Top Bottom