Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Mimi nahitaji viblauzi vya shifon vya kina dada vya mtumba baro moja ambavyo ni quality naweza kupata wapi?
 
Wakuu mwenyekujua hizi cup zinapaikana wapi hapo K/Koo
1f96d72ae3d9794e0cf1f690e1ee9e0c.jpg


8ae22eb58f42c9bc56795a9950a7a91e.jpg
Mtaa wenye stationary ya Tahafif unashuka nao moja kwa moja hayo maduka ya hapo karibu na soko la Kariakoo maduka ya kulia na kushoto utapata.
 
tofauti ya vijora na madera ni ipi?

Tofauti ipo, vijora kuna ambavyo vipo wazi mbele na vinakuwa na kigauni chake cha ndani pia kinaweza kuwa na kamba yake ya kufungia kiunoni. Aina nyingine ya kijora kimezibwa moja kwa moja na kuna vya shifon na cotton pia vinakuwa na kamba yake ya kiunoni
 
Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah! .
Adante sana mkuu wewe kweli syo mchoyo hasa hapo kwenye viatu nimekuelewa
 
Back
Top Bottom