tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Leo katika kipindi cha uchambuzi wa magazeti kupitia redio ya Wasafi FM, imeelezwa kwamba wale wafanyabiashara walioporwa mabilioni ya fedha na kikosi kazi kilichoundwa na Mwendazake, sasa watarudishiwa fedha zao rasmi. Hii ni moja ya hatua za kuponya maumivu na uharibifu uliofanywa na serikali ya awamu ya 5 chini ya Mwendazake.
Katika taarifa hiyo, imeelezwa yupo mfanyabiashara mmoja aliyeporwa jumla ya Tsh 3.5 bilion na kumpelekea kufilisika kibiashara. Mh mama Samia hataki kuongoza nchi yenye watu waliopondeka mioyo kutokana na kunyanyaswa na serikali iliyopita. Ndio maana anafanya jitihada zote kuhakikisha anatibu majeraha na makovu yote yaliyosababishwa na serikali iliyopita ili nchi isonge mbele bila kinyongo.
MAONI YANGU
Namkubali sana Mh mama Samia kwa ujasiri wake huu ijapokuwa kuna baadhi ya wanaCCM hawapendi kuona watanzania wenzao wakiishi maisha bora katika nchi hii. Sote ni mashahidi jinsi wafanyabishara walivyokuwa wakiporwa fedha na akina Sabaya na Makonda (wateule wa Mwendazake) bila kuchukuliwa hatua zozote, hadi baadhi ya wafanyabiashara wakaamua kuikimbia nchi. Ukweli wa jambo hili umeanza kudhihirika wazi baada ya baadhi ya wafanyabiashara kuwafungulia mashataka wahalifu hawa wawili waliokuwa vipenzi wa Mwnedazake.
Nawasilisha.