zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Yes ni wakwepa Kodi lakini hupaswi kuchukua Hela kwenye akaunti ya mtu inapaswa umpe ratiba ya kulipa au mpige fine Ili afanye biashara huku anakulipa hata kama itachukua miaka 5. Ila hii ya kuzoa Kila kitu hapana maana biashara inakufa kabisa.Hivi inamaana waliteuliwa tu baadhi ya wafanyabiashara alafu wakaporwa fedha zao na wengine kama Bakhresa na Mo Dewji wakaachwa ili hali ndiyo mabilionea wakubwa!!
Hii inaingia akilini kweli?mimi naamini wengi wapiobananishwa ni wakwepa Kodi wazuri na vilevile kama kweli walinyang'anywa Mali yao halali mbona hawakuishitaki serikali mahakamani ili warudishiwe Mali zao walizochuma kihalali?
Bado nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa walionewa!!
Ni kama yule mzungu alivyodaka ndege zetu ulidhani ni ustaarabu? Sasa ndege isiporuka Mapato ya kulipa yatatoka wapi? Au imagine China waje kuchomoa pesa zetu zote BOT kisa wanatudai mikopo kadhaa unadhani itakuaje?
Hakuna mtu asiyekwepa Kodi au kudaiwa mkopo Cha msingi mbane akulipe ila sio kukomba pesa kwa akaunti bila utaratibu.