bitimkongwe
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 7,794
- 7,551
Umeshaamka kutoka kwenye usingizi mzito? Au ulikuwa nje ya nchi na hukuwa na muda wa kusoma mambo yaliyokuwa yanatokea humu nchiniHivi inamaana waliteuliwa tu baadhi ya wafanyabiashara alafu wakaporwa fedha zao na wengine kama Bakhresa na Mo Dewji wakaachwa ili hali ndiyo mabilionea wakubwa!!
Hii inaingia akilini kweli?mimi naamini wengi wapiobananishwa ni wakwepa Kodi wazuri na vilevile kama kweli walinyang'anywa Mali yao halali mbona hawakuishitaki serikali mahakamani ili warudishiwe Mali zao walizochuma kihalali?
Bado nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa walionewa!!
Hivi umesahau kwamba Mo alitekwa nyara na jamaa zaake wakatangaza dau la bilioni moja na nusu pale atakapopatikan? Ule mchezo wa kuigiza?
Kama ni kweli walikwepa (na inawezekana sana) kwa nini hakuna ofisa wa TRA aliyepelekwa mahakamani kwa kusaidia au kuruhusu ukwepaji huo wa kodi?