KERO Wafanyabiashara ya chakula acheni kurudisha mabaki

KERO Wafanyabiashara ya chakula acheni kurudisha mabaki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kifupi hakuna sehemu nzuri ya kula zaidi ya nyumbani kwako.

Hakuna mfanyabiashara yoyote wa chakula (awe mdogo au mkubwa) ambae hafanyi "manuva" kwenye uandaaji wa chakula ili ku maximize profit.

Mfano:
1. Vitu vilivyoharibika kama nyanya, karoti, hoho nk havitupwi kamwe.
2. Vitu vilivyobaki kama wali, kuku, nyama nk kesho vinaungwa upya
3. Vitu vilivyo expire hakuna anaetupa.
4. Maji yanayosafishia vyombo usiombe ukayaona
5. Nk
Mkuu hali inatisha sana, basi bora watu wale matunda wakiwa sehemu za movements then wakale vyakula majumbani mwao, Coz matunda ndo usalama upo kwa 100% (Matunda ambayo hayajakatwa)
 
Kuna hii tabia ya kurudisha mabaki ya mteja kwenye chakula Kwa wafanyabiashara hasa wa maeneo ya kawaida japo huwa hatuoni ila utakutana nayo tu.

Juzi Kuna mtu kasema aliwahi shuhudia mama ntilie anarudisha mchuzi uliobakishwa na mteja kwenye sufuria ya mboga nikakumbuka visa vyangu, silagi Kwa mama ntilie ila chips haziepukiki.

Pia soma: Huwa unakagua usafi sehemu unayoenda kupata chakula?

Eneo la kwanza ni Mikocheni karibu na hospital kubwa sana, wakati nakula chips mayai kufungua katikati nakuta nzi wamenasa ilibidi njikaze tu kuwaondoa nsije tupa chakula na nna njaa.

Eneo la pili Ubungo mitaa ya hosteli ndanindani kwenye hotel kama nyota tatu, nikiwa na rafiki ikaagizwa chips mayai na nyama, wakati nakula katikati nakuta mifupa midogomidogo ya kuku ilikwishaliwa liwa imenasia, na pieces za kabichi, means mteja akibakisha wao wanatoa kile kilichobaki wanarudisha kwenye kisafi wanachanganya.

Juzijuzi Tena Niko Magomeni, kwenye chips tu pembeni ya main Rosa, chips mayai nakula katikati nashangaa naona ugumu kufosi naibuka na toothpick kama tatu zimelala katikati ya mayai. nkitafuta nakuata vipande vya nyama.

Sijawahi kutana na haya mambo mtaani kwetu ila maeneo yenye biashara ndo nakutana nayo.

Mbona mnatufanyia hivi, imagine mtu unahangaika tangu asubuhi hata kunywa maji hukumbuki, unaamua kupoza tumbo unaletewa vyakula vilivyorudishiwa mabaki?

What if huyo aliekula hapo akabakisha ana maradhi yanayoambukizwa Kwa mate kama hepatitis?
What if akiwa anakula kapiga chafya vikarukia humo?
What if wamewekeana sumu au madawa?

Mteja anatoa pesa kamili Kwa kile anachostahili hata mkimwaga hayo mabaki shida yenu Iko wapi, si unauza kama ulivyoplan? Kwanini mnarisk Maisha ya wengine kutafuta extra profit toka kwenye kilekile mlichozalisha. Mnapata hasara mkimwaga ilhali kishalipiwa?
Mnaua biashara za wengine pia.

Badilikeni!!
Juzi kati nilikuwa mgahawa Fulani nikabakiza chapati na ilikuwa ya mwisho. Mteja akapiga simu akaambiwa imebaki moja, nikaashangaa ila nikauchuna tu.
 
Kiepe yai si kinaandaliwa unaona mkuu, au ushuani mambo ni tofauti??

Migahawa yote ninayokula msosi naona jinsi wanavyopakua, chipsi nazo hivyo hivyo naona kila hatua.

Kitu siwezi kula ni zile broiler zao, zile hata zimeremete vipi siwezi kula.
 
Juzi kati nilikuwa mgahawa Fulani nikabakiza chapati na ilikuwa ya mwisho. Mteja akapiga simu akaambiwa imebaki moja, nikaashangaa ila nikauchuna tu.
So yako ilobaki ndo hiyo ilotajwa?
Wakairudisha mahali pake
Ndivyo wanavyofanya
 
Maafisa afya hawafanyi kazi zao, inawezekana kudhibiti usafi kwa wauza chakula
Kabla hatujawalaumu hao maafisa afya kwanza tujiulize wako wangapi? Wamepewa nyenzo gani za kuwawezesha kuwafikia wauza chakula wengi mara kwa mara? Vipi wanalipwaje ukilinganisha na umuhimu wa kazi yao ili wasitamani rushwa?
 
Jamani eeh kuna watu huwa wananunua hayo mabaki kulishia mbwa wao wauzieni wao badala ya kulisha binadamu wenzenu vitu vichafu.
Watu wengi wenye migahawa/mama ntilie hua wanaenda sokoni jioni kununua vile vitu vilivyoharibika kama nyanya zilizopondekapondeka, viazi, mboga za majani zilizonyauka nk kwa bei ya hasara. Hivyo ndio hutumia kupikia.
 
Wauza vyakula wamekua wachafu sana serikali imelala na chombo chake cha kufuatilia afya vimelala ...watu wanalipwa mishahara for nothing....hata sehemu wanazo kaanga kuku kuna mbinu wanaitumia ...yaani wewe umechagua kipande cha kuku wakaange kumbe wanaweka vingine ndani ya mafuta wanakutolea kile wanachotaka wao kiuzwe tofauti na ulicho chagua.
Na hiyo Ili kutengeneza faida?
Aisee
 
Watu wengi wenye migahawa/mama ntilie hua wanaenda sokoni jioni kununua vile vitu vilivyoharibika kama nyanya zilizopondekapondeka, viazi, mboga za majani zilizonyauka nk kwa bei ya hasara. Hivyo ndio hutumia kupikia.
Nina dogo langu moja . Hata umpeleke wapi hali nje ya nyumbani.
 
Ukienda kwa mama ntilie.
Akikuambie MBOGA NIKUCHANGANYIE.
ndugu yangu hapo utawekewa na ubwabwa uliobakk kwa mwenzio.
kuna mwingine nimemuona chakula kimebaki mezani kachukua kijiko kile kile kamalizia.
Hyo ya kurudisha mboga wala sikatai KWELLLL
Wao hawaoni kinyaa lakini?
 
Hizi adha tunakutana nazo sana sisi bachelor sana sana.

Mfano kuna kihoteli kimoja ni hapa mtaani niliweka oda ya chakula mchana na usiku nikawapatia na hotpot langu special kwaajir ya kuweka chakula changu pekee.

Picha linaanza siku ya kwanza mchana naletewa chakula mfuniko wa hotpot una alama alama ya vidole vya maji machafu, nikajifariji ni mfuniko pekee, ile nimemaliza kula tu tumbo likaanza kuunguruma nikajifariji labda maji ya kunywa.

Kesho tumbo likanisumbua nikafahamu ni madonda tumbo yameamka maana huwa nina tatizo hilo nikapotezea ila nikatoa ahadi jioni nitaenda kufuata chakula mwenyewe nijionee uandaaji hadi uhifadhi wa chakula.

Jioni nimefika eneo la tukio, kwanza hotpot langu limetupwa chini hapo kuanzia mchana halikuoshwa linasubilia mida ya chakula ndipo lioshwe.

Basi nikawaambia waniandalie chakula changu niondoke ile hotpot limechukuliwa likasuuzwa kwenye maji flani yalikuwa yameisha badili rangi na kuanza kuwa ya brown kisha kukung'utwa na kuwekewa chakula mfuniko wake, kwa vile yule mdada alikuwa busy kuweka chakula akamuomba boda boda mmoja amsaidie kuuosha aiseee 🤧🤧🤧

Yaani nilishikwa na hasira haswa isingekuwa na utu rohoni siku hiyo tungetukanana nikasogea pembeni kidogo na kuwaacha waendelee ya uchafu wao....

Nilivyotoka hapo aiseee ......
 
Kuna wauza chips zaidi ya mmoja nimewashuhudia wakiulizwa chips ni za moto basi wao wanazipima joto kwa mkono nyuma ya kiganja ...tatizo wengi ya wauza chips ni watu washamba wa vijijini wana tabia za uchafu wa asili wanashindwa kujua jema na baya.
Bado hujasema wale wauza nyama choma yaani wanashika nyama kw amkono wanakata kwa mkono wanaweka kwenye sahani ya mteja kwa mkono😤 ni huzuni.
 
Elimu inahitajika sana kwa wafanyabiashara hususani wa chakula! Kuna tabia ya kulamba ulimi kupakaza mimate kwenye vidole kisha kufungua mfuko wa nylon na kukuwekea bidhaa kama nyanya ,bamia ,carrot ,hoho etc

Kuna tabia ya kupuliza mifuko ya nylon na kufunga karanga ,miwa ,ubuyu ,korosho etc ,elimu inahitajika sana ni chanzo cha magonjwa ya TB ,Hep B etc

Wanaobakisha wali ,mchuzi wa supu ,maharage ,mboga za majani huwa wanaurudisha kwenye sufuria na kuwapa wateja wengine.

Mara nyingi nanua sehemu ambayo sufuria la supu naliona live na wateja wanaona ,so inakuwa ngumu kurudishia ila wale wanaoliweka sufuria ndani halionekani silagi kabisa hapo.

Mimi kwa mama lishe nakunywa supu tu na chapati ila ugali wali sili kabisa ,kama nasikia njaa bora niagize chips kavu na kipaja kimoja basi.
 
Back
Top Bottom