KERO Wafanyabiashara ya chakula acheni kurudisha mabaki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mkuu hali inatisha sana, basi bora watu wale matunda wakiwa sehemu za movements then wakale vyakula majumbani mwao, Coz matunda ndo usalama upo kwa 100% (Matunda ambayo hayajakatwa)
 
Juzi kati nilikuwa mgahawa Fulani nikabakiza chapati na ilikuwa ya mwisho. Mteja akapiga simu akaambiwa imebaki moja, nikaashangaa ila nikauchuna tu.
 
Kiepe yai si kinaandaliwa unaona mkuu, au ushuani mambo ni tofauti??

Migahawa yote ninayokula msosi naona jinsi wanavyopakua, chipsi nazo hivyo hivyo naona kila hatua.

Kitu siwezi kula ni zile broiler zao, zile hata zimeremete vipi siwezi kula.
 
Juzi kati nilikuwa mgahawa Fulani nikabakiza chapati na ilikuwa ya mwisho. Mteja akapiga simu akaambiwa imebaki moja, nikaashangaa ila nikauchuna tu.
So yako ilobaki ndo hiyo ilotajwa?
Wakairudisha mahali pake
Ndivyo wanavyofanya
 
Maafisa afya hawafanyi kazi zao, inawezekana kudhibiti usafi kwa wauza chakula
Kabla hatujawalaumu hao maafisa afya kwanza tujiulize wako wangapi? Wamepewa nyenzo gani za kuwawezesha kuwafikia wauza chakula wengi mara kwa mara? Vipi wanalipwaje ukilinganisha na umuhimu wa kazi yao ili wasitamani rushwa?
 
Jamani eeh kuna watu huwa wananunua hayo mabaki kulishia mbwa wao wauzieni wao badala ya kulisha binadamu wenzenu vitu vichafu.
Watu wengi wenye migahawa/mama ntilie hua wanaenda sokoni jioni kununua vile vitu vilivyoharibika kama nyanya zilizopondekapondeka, viazi, mboga za majani zilizonyauka nk kwa bei ya hasara. Hivyo ndio hutumia kupikia.
 
Na hiyo Ili kutengeneza faida?
Aisee
 
Watu wengi wenye migahawa/mama ntilie hua wanaenda sokoni jioni kununua vile vitu vilivyoharibika kama nyanya zilizopondekapondeka, viazi, mboga za majani zilizonyauka nk kwa bei ya hasara. Hivyo ndio hutumia kupikia.
Nina dogo langu moja . Hata umpeleke wapi hali nje ya nyumbani.
 
Ukienda kwa mama ntilie.
Akikuambie MBOGA NIKUCHANGANYIE.
ndugu yangu hapo utawekewa na ubwabwa uliobakk kwa mwenzio.
kuna mwingine nimemuona chakula kimebaki mezani kachukua kijiko kile kile kamalizia.
Hyo ya kurudisha mboga wala sikatai KWELLLL
Wao hawaoni kinyaa lakini?
 
Hizi adha tunakutana nazo sana sisi bachelor sana sana.

Mfano kuna kihoteli kimoja ni hapa mtaani niliweka oda ya chakula mchana na usiku nikawapatia na hotpot langu special kwaajir ya kuweka chakula changu pekee.

Picha linaanza siku ya kwanza mchana naletewa chakula mfuniko wa hotpot una alama alama ya vidole vya maji machafu, nikajifariji ni mfuniko pekee, ile nimemaliza kula tu tumbo likaanza kuunguruma nikajifariji labda maji ya kunywa.

Kesho tumbo likanisumbua nikafahamu ni madonda tumbo yameamka maana huwa nina tatizo hilo nikapotezea ila nikatoa ahadi jioni nitaenda kufuata chakula mwenyewe nijionee uandaaji hadi uhifadhi wa chakula.

Jioni nimefika eneo la tukio, kwanza hotpot langu limetupwa chini hapo kuanzia mchana halikuoshwa linasubilia mida ya chakula ndipo lioshwe.

Basi nikawaambia waniandalie chakula changu niondoke ile hotpot limechukuliwa likasuuzwa kwenye maji flani yalikuwa yameisha badili rangi na kuanza kuwa ya brown kisha kukung'utwa na kuwekewa chakula mfuniko wake, kwa vile yule mdada alikuwa busy kuweka chakula akamuomba boda boda mmoja amsaidie kuuosha aiseee 🤧🤧🤧

Yaani nilishikwa na hasira haswa isingekuwa na utu rohoni siku hiyo tungetukanana nikasogea pembeni kidogo na kuwaacha waendelee ya uchafu wao....

Nilivyotoka hapo aiseee ......
 
Kuna wauza chips zaidi ya mmoja nimewashuhudia wakiulizwa chips ni za moto basi wao wanazipima joto kwa mkono nyuma ya kiganja ...tatizo wengi ya wauza chips ni watu washamba wa vijijini wana tabia za uchafu wa asili wanashindwa kujua jema na baya.
Bado hujasema wale wauza nyama choma yaani wanashika nyama kw amkono wanakata kwa mkono wanaweka kwenye sahani ya mteja kwa mkono😤 ni huzuni.
 
Elimu inahitajika sana kwa wafanyabiashara hususani wa chakula! Kuna tabia ya kulamba ulimi kupakaza mimate kwenye vidole kisha kufungua mfuko wa nylon na kukuwekea bidhaa kama nyanya ,bamia ,carrot ,hoho etc

Kuna tabia ya kupuliza mifuko ya nylon na kufunga karanga ,miwa ,ubuyu ,korosho etc ,elimu inahitajika sana ni chanzo cha magonjwa ya TB ,Hep B etc

Wanaobakisha wali ,mchuzi wa supu ,maharage ,mboga za majani huwa wanaurudisha kwenye sufuria na kuwapa wateja wengine.

Mara nyingi nanua sehemu ambayo sufuria la supu naliona live na wateja wanaona ,so inakuwa ngumu kurudishia ila wale wanaoliweka sufuria ndani halionekani silagi kabisa hapo.

Mimi kwa mama lishe nakunywa supu tu na chapati ila ugali wali sili kabisa ,kama nasikia njaa bora niagize chips kavu na kipaja kimoja basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…