KERO Wafanyabiashara ya chakula acheni kurudisha mabaki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna wauza chips zaidi ya mmoja nimewashuhudia wakiulizwa chips ni za moto basi wao wanazipima joto kwa mkono nyuma ya kiganja ...tatizo wengi ya wauza chips ni watu washamba wa vijijini wana tabia za uchafu wa asili wanashindwa kujua jema na baya.
Nimewahi kuona muuza juice anachokonoa sikio halafu akaenda kukata matunda ya kuweka kwenye blender kutengeneza juice bila hata kunawa mikono.
 
Pole mkuuni uchafu uliopitiliza halafu wenyewe hawajali,hawajistukii
 
Juzi kati nilikuwa mgahawa Fulani nikabakiza chapati na ilikuwa ya mwisho. Mteja akapiga simu akaambiwa imebaki moja, nikaashangaa ila nikauchuna tu.
Usikute hata ulizokula zilibakishwa na mwingine na wewe ukabakisha moja ikanunuliwa na mteja wa tatu.
 
Nimeshtushwa sana khaaa
 
Naongezea hapo vyombo pia vinaoshwa na maji machafu sana.
Maji ya kuoshea vyombo hua hayamwagwi, ni hayo hayo kuanzia asubuhi mpaka usiku. Sahani inaoshwa kuondoa ule uchafu kisha inafutwa na kitaulo/kitambaa kichafu mchezo umeisha.
 
Kuna Siku moja nilikuwa natoka Mazinde Juu.. pale Mombo kwenye Nyama Choma (pale magari yanayoenda Arusha na Sehem mbali mbali za Mkoa Wa Kilimanjaro ) yana posi mama nikiwa naagiza Nyama niliona kuna dogo anakusanya mabaki toka kwenyr sahani zilizokuwa na Nyama makombo. Nilifikiri labda wanakusanya for Dogs- niliagiza Mbavu za Mbuzi... walipoleta nyama yote aina ata mfupa mmoja😁 Ugomvi ule uliisha kesho yake baada ya Bwana afya wa Wilaya na Wahusikanwengine kuingilia kati , nilirudishiwa pesa yangu na ilikubalika kuwekwa mbali dust bin ya makombo ... ambalo lilikuwepo pale mpaka upanuzi wa barabara ulipovunja pale ila kwa sasa sijui wanafanyaje. So kuwa makini unapoagiza Nyama choma pale Mombo kabla ya kufika Liverpool Hotel. Pale Same Dogo alinipa Nyama ingine na aliomba msamaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…