Wafanyakazi Namera Group of Industries wagomea mabadiliko ya jina la Kampuni hadi walipwe stahiki zao

Wafanyakazi Namera Group of Industries wagomea mabadiliko ya jina la Kampuni hadi walipwe stahiki zao

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Wafanyakazi wa Kampuni ya Namera Group of Industries (T) LTD kilichopo Gongolamboto, Dar es Salaam wamefanya mgomo na kukusanyika nje ya kiwanda hicho wakilalamikia hatua ya mwajiri wao kubadilisha jina la kampuni hiyo bila kuwalipa stahiki zao na kuvunja mikataba yao ya awali.

Wafanyakazi hao wamedai kuwa mwajiri amekuwa akifanya mabadiliko ya usimamizi na jina la kampuni kutoka Namera kwenda Nida (Nida Text Mills) bila kuingia nao makubaliano ya wazi au kuvunja mikataba ya zamani.

Wakizungumza nje ya geti la kiwanda hicho, baadhi ya wafanyakazi wameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili:



Abdallah Juma Hamisi: Alieleza kuwa tangu awali walipokea taarifa kutoka kwa viongozi wa chama cha wafanyakazi (TUICO) kuhusu mabadiliko ya jina la kampuni. Wafanyakazi walitaka mkataba wa zamani wa Namera uvunjwe na walipwe stahiki zao kabla ya kusaini mkataba mpya na kampuni mpya ya Nida, lakini uongozi umegoma kufanya hivyo na kubandika tangazo la mabadiliko hayo tarehe 31.

Fregodi Julius Mohamed: Alibainisha kuwa mabadiliko hayo yanafanana na "kulazimishwa" bila maridhiano ya pande zote mbili. Aliongeza kuwa mwajiri wao hana ushirikiano na wafanyakazi, na amekuwa akitengeneza sheria zake bila kujali maslahi yao. Pia, alieleza kuwa kiwandani hapo hakuna viwango vilivyowazi vya mishahara kwani hakuna mfanyakazi anayejua kiwango chake halisi cha mshahara wa mwezi.

Rehema Julius Msabaha: Mfanyakazi huyo aligusia changamoto ya mazingira magumu ya kazi, ikiwemo ukosefu wa usafi wa mazingira kama vile vyoo vichafu ambavyo ni hatari kwa afya ya wafanyakazi, hususan wanawake. Aliongeza kuwa mwajiri amekuwa akiepuka kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na wafanyakazi wake.

=====================================​
Alipotafutwa Meneja wa kiwanda hicho, anayefahamika kwa jina la Frederick, na kuelezwa kuhusu madai hayo, alisema kuwa hawezi kuyazungumzia kwa wakati huo.
 
Katika suala la uwekezaji Tz naona serikali inaangalia zaidi kodi kutoka kwa mwekezaji ila hushindwa kuangalia namna gani pia wananchi wana neemeka kutokana na huo uwekezaji.

UKiingia viwandan huko watu wanapelekeshwa kama wanyama
 
Back
Top Bottom