Wafanyakazi wa ndani si watumwa wawe wanaheshimiwa kama binadamu aliye huru

Wafanyakazi wa ndani si watumwa wawe wanaheshimiwa kama binadamu aliye huru

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Kutokana na hali ya maisha wafanya kazi wa ndani wengi hukaa kwa waajiri wao. Hii hutokana na waajiri wengi kutomudu kulipa wafanyakazi kima cha chini cha mshahara. Pia kuepuka usumbufu. Fikiria mfanyakazi anaishi Mbagala awahi usafiri kufika Mbezi ili muajiri amkabidhi watoto na yeye awahi kazini si rahisi.

Kutokana na hali ya maisha si wengi pia wanaomudu kumpatia mfanyakazi quarter yake ya kuishi au hata chumba chake tu awe na faragha. Wengi wetu hulaza wafanyakazi kwenye chumba kimoja na watoto au sebuleni.

Hawa wafanyakazi wengi wana umri wa miaka 18+. Kibaiolojia umri huu binadamu anakuwa ameshapevuka. Kuna wale wanao chunguza begi au sanduku la mfanyakazi. Akikuta picha zake za marafiki wa jinsia tofauti wanakua wakali.

Kumbuka hapo umevunja haki ya faragha. Kila binadamu anahitaji sehemu ya kujistirI. Hii ni moja ya tofauti zetuna wanyama.

Kila binadamu ana haki ya kupenda na kupendwa. Kama hajaingilia ndoa yako maisha yake ya mapenzi haya kuhusu. Unaweza kumpa muongozo kama mzazi au kaka/dada mkubwa.

Wafanyakazi wa ndani si watumwa ni binadamu huru.
 
Kwani si wanaume huwa tunashida nao! Ni nyinyi tu akina mama ndio huwamnashida nao sisi wala hatuna shida nao ila tu tunaelewa kuwa hakuna beki tatu tasa..!

Sasa nenda kichwakichwa uone maana nzima ya huo usemi..😅

Wanaume hapo twateta kiroho hakuna kupiga kelele..😎
 
Unalosema ni kweli aisee, wafanyakazi wengi hulipwa 45000 na wanapigishwa kazi balaa. Hapo pia kuna matusi ya mama mwenye nyumba na viburi vya watoto.

Kwanza kila itu inabidi apangiwe, ikitokea akajulikana ana mpenzi wengine huwatandika viboko yani hawana haki
 
Unalosema ni kweli aisee, wafanyakazi wengi hulipwa 45000 na wanapigishwa kazi balaa. Hapo pia kuna matusi ya mama mwenye nyumba na viburi vya watoto. Kwanza kila itu inabidi apangiwe, ikitokea akajulikana ana mpenzi wengine huwatandika viboko yani hawana haki
Ukiheshimu sheria za ajira, mfanyakazi anakuwa na siku za mapumziko kila wiki. Hizi siku anakuwa huru kufanya mambo yake yasiyohusiana na kazi.
 
Wanawake ndo adui wa kuu wa wafanya kazi wa ndani.....mke wangu anatimua wafanya kazi kila baada ya miazi miwili mitatu eti hataki mazoea nao.

Nashindwa kuwakalili majina kila mda kidogo naona mpya, huyu mama (mke wangu) Ana roho mbaya sijapata kuona ningekua sijazaa nae ningemkimbia.
 
Wamama ndio wana shida na hao wadada sie wababa hata majina hatuwajuagi kama alivosema jamaa juu hapo...

Hata home kila anaekuja miezi mitatu hafiki naoana nakuja mwingine mi sishindi hapo sielewi masikia tu huhu mjeuri na unajua wamama walivyo utetee beki tatu hapo unanzisha vita ya nyuklia
 
Mulwanaka umeuaa,, hapo namhala ng'wichane huna mke au wewe ni chitombi ndio maana mama hataki wakae muda mrefu kwa kuhofia kwamba utawapembua! Ila chunguza afya za watoto wako huo mchanyato wa watumishi wa ndani siyo mzuri kabisa!
Hapana mie sio kchitombi kama unavyo liweka mimi ni gentleman najeheshimu sana ila Yule mama mke angu Ana gubu anaishi kwa kutojamini anavisilani vyake tu ......ila sina jinsi tulisha zaa ila anatesa sana watumishi wandani na siwezi kuingilia ntapewa tuhuma nzito
 
Kuna dada nimemuuliza hapa ofisini kasema tatizo wengi wanakuwa kwenye foolish age! Ukimuachia huru na mwanaume kazi hazifanyiki tena kutwa kucha kukimbizana na mapenzi!

Hoja ingine kasema, mara nyingi wanawachukua hawa mabinti kwa wazazi wao kwa ahadi kuwa watawatunza kama watoto wao ikiwemo kuwaepusha na ngono! So, show inasimamiwa hapo coz akipata mimba wazazi wanaanza na wewe waliyekukabidhi mtoto.
 
Kulingana na maisha yetu baadhi ya watanzania. Hakuna mtu anaefaidi kama dada wa kazi au kaka wa kazi. Ni baadhi sio woote.
Unakuta dada wa kazi mshahara ni kati ya elfu 30 mpaka elfu 50.

Anakula milo mitatu, anaoga maji, umeme bure wakat mwingine mavazi ama taulo za kihihufadhi(pedi) anapewa bure akitibiwa matibabu bure kama vile anabima.

Japo sio wafanyakazi woote wanafanyiwa hivi ila ukitathimini mfanyakazi wa ndani anaepata stahiki kama hizo anaweza mpita hata askari, mwalimu au boda boda kwa kipato.

Naomba kutanguliza kumladhi kwa kada nilizo zitaja hapo juu. Nimefanya reference tuu kitokana na vipato vyao vya mwezi.
 
Wanawake ndo adui wa kuu wa wafanya kazi wa ndani.....mke wangu anatimua wafanya kazi kila baada ya miazi miwili mitatu eti hataki mazoea nao, nashindwa ku wakalili majina kila mda kidogo naona mpya, huyu mama (mke angu) Ana roho mbaya sijapata kuona ningekua zija zaa nae ningemkimbia
Pole sana, hawa wenzetu hawapendani.
 
Kulingana na maisha yetu baadhi ya watanzania. Hakuna mtu anaefaidi kama dada wa kazi au kaka wa kazi. Ni baadhi sio woote.
Unakuta dada wa kazi mshahara ni kati ya elfu 30 mpaka elfu 50.
Anakula milo mitatu, anaoga maji, umeme bure wakat mwingine mavazi ama taulo za kihihufadhi(pedi) anapewa bure akitibiwa matibabu bure kama vile anabima.

Japo sio wafanyakazi woote wanafanyiwa hivi ila ukitathimini mfanyakazi wa ndani anaepata stahiki kama hizo anaweza mpita hata askari, mwalimu au boda boda kwa kipato.

Naomba kutanguliza kumladhi kwa kada nilizo zitaja hapo juu. Nimefanya reference tuu kitokana na vipato vyao vya mwezi.
Mkuu acha kukejeli hao watoto wewe ungependelea bint yako au Dada ako afanye hiyo kazi. kuna kazi ambazo sio mtu kwamba anapenda ni hali ya maisha wewe kama uko vizri husisahao wenzako hayo maisha wanayatafuta
 
Thubutuu sikwawa fanyakzi wa ndani weee wanavyo fungiwa hivyo yani hatakuwapata ningum sana utavizia weee
Ukiheshimu sheria za ajira, mfanyakazi anakuwa na siku za mapumziko kila wiki. Hizi siku anakuwa huru kufanya mambo yake yasiyohusiana na kazi.
 
Kazi anazo zifanya embu tiririka hapa tulinganishe
Kulingana na maisha yetu baadhi ya watanzania. Hakuna mtu anaefaidi kama dada wa kazi au kaka wa kazi. Ni baadhi sio woote.
Unakuta dada wa kazi mshahara ni kati ya elfu 30 mpaka elfu 50.

Anakula milo mitatu, anaoga maji, umeme bure wakat mwingine mavazi ama taulo za kihihufadhi(pedi) anapewa bure akitibiwa matibabu bure kama vile anabima...
 
Kuna dada nimemuuliza hapa ofisini kasema tatizo wengi wanakuwa kwenye foolish age! Ukimuachia huru na mwanaume kazi hazifanyiki tena kutwa kucha kukimbizana na mapenzi!

Hoja ingine kasema, mara nyingi wanawachukua hawa mabinti kwa wazazi wao kwa ahadi kuwa watawatunza kama watoto wao ikiwemo kuwaepusha na ngono! So, show inasimamiwa hapo coz akipata mimba wazazi wanaanza na wewe waliyekukabidhi mtoto.
Kwani haya hayawezi kufanyika kwa maongezi? Unamueleza athari za mapenzi bila mipango. Mtu anaekupenda hatafanya mapenzi yenu yawe siri na mkuwaeleza watu wazima wanaweza kuwaongoza.

Mpe pia muda wa mapumziko na ikiwezekana muone mpenzi wake.
 
Mimi huwa nawapenda sana maana wana nifaraiji sana kwakweli nime watafuna mpka basi nani watam balaaa wanajua kupenda hao alafu kwanza hawajui hata kuchuna
Hii inaitwa unyanyasaji wa ki ngono. Umempata kimapenzi huyu binti kwakua ni mfanya kazi wako.

Maisha ni siri ya Mungu, pamoja na uwezo ukionao ulishawaza mtoto wako anaweza kuwa mfanya kazi wamtu siku moja na akafanyiwa haya unayofanyia wengine.

Hii ndiyo ethics za kazi, kufanya mambo sahihi hata pale ambapo huonekani.
 
Wanyanyasaji wa wafanyakazi wa ndani ni wanawake, na watoto wanaodekezwa.Kama kuna Mwanaume naye anaingia katika kundi hili la wanyanyasaji wa mabinti wa kazi, huyo ana matatizo,na ni aibu kumjumuisha kwenye kundi la wanaume.
 
Wanawake ndo adui wa kuu wa wafanya kazi wa ndani.....mke wangu anatimua wafanya kazi kila baada ya miazi miwili mitatu eti hataki mazoea nao.

Nashindwa kuwakalili majina kila mda kidogo naona mpya, huyu mama (mke wangu) Ana roho mbaya sijapata kuona ningekua sijazaa nae ningemkimbia.
Pole sana ndugu.
Usile sumu kisa tu umeishaiweka kwenye chakura.

Usipo shituka mapema atakuharibia na hao watoto ulio zaa nae maana nao wataiga tabia zake.
 
Kuna dada nimemuuliza hapa ofisini kasema tatizo wengi wanakuwa kwenye foolish age! Ukimuachia huru na mwanaume kazi hazifanyiki tena kutwa kucha kukimbizana na mapenzi!

Hoja ingine kasema, mara nyingi wanawachukua hawa mabinti kwa wazazi wao kwa ahadi kuwa watawatunza kama watoto wao ikiwemo kuwaepusha na ngono! So, show inasimamiwa hapo coz akipata mimba wazazi wanaanza na wewe waliyekukabidhi mtoto.
Mbona ilo ni jambo dogo. Kama unajua hivyo ukimfikisga hom tu unampereka kwenye vituo vya trust ama hospital wanamuwekea njiti ili asiweze kubeba ujauzito. Kwan uwez mchunga kila siku ila unaweza kuzuia asibebe mimba
 
Back
Top Bottom