wanaume pia wapo kwenye kundi la kunyanysa wafanyakazi wa ndani, sema tofauti na sisi wanawake, wao huwanyanyasa kingono, unakuta baba mtu mzima anatembea na katoto ambako ni sawa na mjukuuu wake, na hili nilishashuhudia jamani niliishi nyumba moja sinza huyo baba ni mtu mzima sana mkewe alishafariki alikuwa anaishi na watoto wake tu, basi akaleta housegirl, kale kabinti kalikuwa kadogo kwa kweli kwenye 15years hivi, ila alianza kutembea na kale katoto na mbaya zaidi watoto wooote wanaenda shule wanabaki wawili tu aisee nilikuaga nasikia uchungu sana kwa kale ka binti ingawa kenyewe kalikuwa kanaonekana kama kana furahia yale maisha