Wameuawa au wamefariki? na kama wanaushahidi si utakuwa ndani ya taarifa ya CAG
 
Stuka ndugu yangu, hii nchi ni kama kichuguu, inaliwa ikimwagiwa maji, jikite kuwatafutia wajukuu zangu riziki (wanao).
wajukuu watakuta taifa limebaki mifupa mitupu kama wazee wetu kina Nyerere na Karume wangeruhusu nchi kuliwa hivi tusingekuta chochote.
 
Mliweka precedence mbaya sana nyie chawa, kipindi watu wanakufa enzi za JPM mlikua mnabisha mnasema sijui ni mabeberu na wapinzani ndio wanawaua kunichagua serikali so hakukuwahi fanyika uchunguzi serious wowote iwe Filikunjombe, Ben Saanane, Tundu Lissu n.k

Sasa unadhani awamu hii itakua accountable kuchunguza vifo wakati precedence mlishaiweka huko nyuma.

Nadhani iwe funzo kwamba ukiona mwenzio ananyolewa....... Maana enzi zile wapinzani wanamalizwa mkiona kama wanamchafua tu Rais au Makonda au Sabaya ila Leo hii ndio mmeamini Sasa kuwa mafisadi hayana huruma na uhai wa mtu?
 
Hii nchi kuongozwa na Wanawake bado sana,sisi wanawake wetu wamezoea majungu na umbea basi.Hiyo mihimili inapaswa ishikwe na wanaume,labda miaka 50 mbele tukiondoka kwenye Hybrid Democracy(Autocracy & Democratic state) ya sasa kwenda kwenye Democracy ya kweli ndiyo tufikirie kuongozwa na Wanawake, assuming kuwa tutakuwa na jamii iliyo elimika na kustaarabika.
 

Kubadilisha ratiba sio rahic hawa.
 
Wananchi tunataka tujulishwe vyanzo vya vifo vya hao watumishi wa NAO,

Hili sio la kuliacha lipite kimya kimya hapana aisee!

Watuambie kulikoni?
Labda mwendazake amefufuka , kingekuwa kipindi chake ungesikia kelele kila kuna
 
wacha uzushi wewe hiyo democracy ya kweli umeiona wapi? Unakariri vitu ambavyo huna uhakika navyo.

Wanawake wataendelea kuongoza nchi hii ukipenda au usipende. Ikiwa unaona shida endelea mbele mpaka Burundi.
 
Mafisadi sio watu wa kuwachekea na sasa wameingia jikoni, kazi tunayo!! Mpaka uchunguzi wa waliotajwa na CAG unamalizika na hatua kuchukuliwa dhidi yao, makaburi mengi yatajaa mizoga!!

Serikali inalichukulia poa suala hili la mafisadi waliotajwa kwenye report ya CAG, lakini ni vyema kama wale Wote watu muhimu kwenye hiyo taasisi ya ukaguzi akiwemo CAG mwenyewe wakati huu wakapewa ulinzi!!. Msingoje mpaka mkaambiwa ofisi za CAG zimepigwa bomu kuharibu ushahidi ndio muanze kuzinduka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…