TANZIA Wafanyakazi Wawili wa Ofisi ya CAG wafariki dunia
Tuombe Spika wa BUNGE, aruhusu ripoti ya CAG ijadiliwe kwa dharura kipindi hiki bungeni ili jambo hili liishe...vinginevyo ni kweli vielelezo muhimu vitapotea alafu mtaakuja kuambiwa waliokuwa navyo walishafariki...inahuzunisha sana wazalendo wetu kufariki huku taarifa zao zikiwa zimejaa utata na yanayosemwa mitandaoni...
 
Jamhuri iwe macho!

Hii ni JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA ndio jina la kwanza kuzaliwa kabla ya chama na serikali haijakuwepo!!

Yaani ilianza jamhuri ndio vyama vya siasa na serikali vikafuata!!

Hata hao mawaziri na marais ndio walifuatia baada ya JAMHURI ! JAMHURI ni kubwa kuliko mtu wala kikundi au genge LOLOTE!!!

Naomba JAMHURI iingilie kati ujinga huo kama upo!

Mungu IBARIKI TANZANIA nchi yetu niipendayo SANA!
 
Taarifa kamili hii hapa.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Bw. Charles E. Kichere anasikitika kutangaza kifo cha Bw. Geofrey Lawrence Makonyu, Mkaguzi Kitengo cha Walipa Kodi Wakubwa ambae amefariki akiwa Yaounde nchini Cameroon akiwa katika majukumu ya kikazi.
View attachment 2605320
Marehemu Geofrey Lawrence Makonyu
Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe.

====

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles E Kichere anasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi-Divisheni ya Ufanisi, Marehemu Ndimwaga Shitindi kilichotokea leo Jumapil, Aprili 30, 2023 katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma akiwa kwenye matibabu. CAG na Watumishi wote tunaungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Marehemu Ndimwaga kuomboleza msiba huu.

View attachment 2605539
Marehemu Ndimwaga Shitindi

Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe.
Mambo yameanza Sasa.
 
Huyu ndiye aliyefichua uozo wa makamba .............
Muwe mnatoa taarifa za kweli na kuepusha upotoshaji wa kiting. Huyo mwanaume Alikuwa Ukaguzi wa Kodi kwa walipa Kodi wakubwa na huyo mwingine Ukaguzi wa Ufanisi. Ni kwa namna gani kaguzi hizo zinahusiana na masuala ya ufisadi yanayoongelewa. Tuache kuwaumiza wafiwa kwa Maneno ya kipuuzi. Watumishi Hawa wamefariki kama waty wengine wanavyofariki ni upuuzi na ujinga.
 
Mama, kijana wako Makamba ana tuhuma nyingi sana huku mtaani. Magufuli alipogundua alihusika na kifo cha Filikunjombe alimtema haraka sana, mtu aliyezoea kuua anaishi na laana daima.
 
SPIKA wa Bunge kwa heshima na unyenyekevu mkubwa watanzania tunakuomba ruhusu ripoti ya CAG ijadiliwe bungeni huku mtaani hali ni mbaya sana, habari zinazoendelea kusambaa kuhusu vifo vya watumishi wa CAG ni mbaya saana.

Ombi la watanzania ruhusu ripoti ijadiliwe kwa dharura ili kuwaweka huru watanzania wanaohoji juu ya vifo vya watumishi wa CAG..

Hofu kubwa ya watanzania kufikia Novemba ushahidi wa maafisa wa CAG utakuwa umepotea kwa sababu huwezi kujua hao waliofariki walikagua maeneo gani na ushahidi na vielelezo wanavyo wao.
 
Stuka ndugu yangu, hii nchi ni kama kichuguu, inaliwa ikimwagiwa maji, jikite kuwatafutia wajukuu zangu riziki (wanao).
 
Back
Top Bottom